Unywaji wa pombe na tatizo la Figo

Unywaji wa pombe na tatizo la Figo

Daa tarehe 1 Jan 2024 ilikuwa pigo kwa mshkaji wangu niliyempoteza kutokana na Tatizo la Figo ikiwa ni kutokana na kunywa pombe kupindukia.

Kwa kweli ningekuwa na nguvu ya kumzuia mtu asinywe pombe kupindukia ningefanya, na sijajua kwanini Kuna wimbi la vijana kufeli Figo zao kipindi hiki ilihali zamani ulevi ulikuwepo lakini hakukuwa na shida kama hizi.
Pombe fake zimejaa sana mitaani
 
Mimi nilishaapa, nyapu ndio itaniua sio ujinga mwingine wowote.

Na nikifia kwenye nyapu ni sawa na nzi kufikia kwenye kidonda, ni raha mustarehe.

Mwanaume kufia kwenye eneo la vita you die with dignity.

Mwanaume unauawaje na pombe kama sio utaahira? Mimi hayo madude yakishindwa kazi yashindwe kwa sababu zao wenyewe ila sio kwa sababu ya pombe.
Kila mtu atakufa kwa tamaa yake mwenyewe. Hakuna tamaa nzuri zote mbaya
 
Kutokunywa maji lita 3 itoe hapo. Hakuna sehemu unatakiwa unywe maji kiasi hicho. Mwili una respond wenyewe unapokuwa na kiu. Unapokuwa na kiu kunywa maji.
Kunywa maji mengi ni kuzichosha figo vile vile na maji yanaondoa mwilini nutrients zingine kama Calciums.
Kunywa maji pale mwili unaporespond uhaba wa maji mwilini kwa kuhisi kiu tu.
Sahihi kabisa
 
Alafu wakifa wanasema pombe..kuna hizi mboga mboga na matunda zina full pesticides, sema watu hawaoni hilo, hanywi pombe but kila siku anakula mboga za majani na matunda.
Maisha ya sikuhizi hatari sana. Unasema ule matunda pekee, nayo mbegu zilizotumika ndio hizo za kisasa. Kuna siku nilinunua tikitimaji linaonekana limeiva vizuri tu, lakini halikuwa na ladha ya utamu uliozoeleka wa tikiti. Lipolipo tu kama nilikuwa nakula karatasi, nikaishia kulitupa lote!
 
Daa tarehe 1 Jan 2024 ilikuwa pigo kwa mshkaji wangu niliyempoteza kutokana na Tatizo la Figo ikiwa ni kutokana na kunywa pombe kupindukia.

Kwa kweli ningekuwa na nguvu ya kumzuia mtu asinywe pombe kupindukia ningefanya, na sijajua kwanini Kuna wimbi la vijana kufeli Figo zao kipindi hiki ilihali zamani ulevi ulikuwepo lakini hakukuwa na shida kama hizi.
Unatakataasisii ya jk
Walipwe nanani mshaharaaaa??
 
Umejuaje pombe ndio chanzo?

Vidababishi vingine
-Chumvi kupiga kiasi
-kukaa na mkojo muda mrefu
-energy drink
- High blood pressure
-Drug abuse
-Herbal medicine
-kutokunywa maji Lita 3
-pombe na sigara
Hospital ndo walisema hivyo ,manake alifikia hatua anakunywa pombe za kienyeji,smart gin, Serengeti lite etc yeye hachagui na kazi aliyokuwa nayo ni nzuri tu yenye kumfanya awe mlevi
 
Sio figo tu ,na maini pia watu wanateketea sana
Mnaona sifa kunywa pombe kali ,tena unakuta mazoba flani yanachanganya hivyo vivywaji kabisa bila kujua side effects ya kuchanga ya contents za vinywaji vyenye chemical ingredients tofauti tofauti ni kutengeneza sumu na kuoverload figo na maini
Sijui huu ulimbukeni na ushenzi watanzania walijitokeza wapi .
Pombe ya aina yoyote ni hatari kwa afya yako
Yani wanachanganya pombe zenye ingredients tofauti kama vile wako maabara aisee
 
Back
Top Bottom