Unywaji wa pombe na tatizo la Figo

Unywaji wa pombe na tatizo la Figo

Sio figo tu ,na maini pia watu wanateketea sana
Mnaona sifa kunywa pombe kali ,tena unakuta mazoba flani yanachanganya hivyo vivywaji kabisa bila kujua side effects ya kuchanga ya contents za vinywaji vyenye chemical ingredients tofauti tofauti ni kutengeneza sumu na kuoverload figo na maini
Sijui huu ulimbukeni na ushenzi watanzania walijitokeza wapi .
Pombe ya aina yoyote ni hatari kwa afya yako
Kwenda zako
 
Daa tarehe 1 Jan 2024 ilikuwa pigo kwa mshkaji wangu niliyempoteza kutokana na Tatizo la Figo ikiwa ni kutokana na kunywa pombe kupindukia.

Kwa kweli ningekuwa na nguvu ya kumzuia mtu asinywe pombe kupindukia ningefanya, na sijajua kwanini Kuna wimbi la vijana kufeli Figo zao kipindi hiki ilihali zamani ulevi ulikuwepo lakini hakukuwa na shida kama hizi.
Zamani walikuwa wanakunywa pombe za kienyeji zilizotengenezwa kwa mahindi, mtama, au ulezi, ambazo zilikuwa kama chakula.

Kiukweli ukinywa pombe za kisasa kwa muda mrefu lazima utapata shida kama siyo figo, basi kisukari!
 
Fikiria unatunza ini lako weeeee,huku ukinywa vinywaji laini laini ila mwisho unagongwa na treni....what a waste.
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
Au unamuhimiza bodaboda akimbie uwahi job, anakuingiza kwenye tairi ya Fuso.
Afadhali ufe kwa ajali kwa maana hautakuwa umegharamika kwa matibabu. Wakati unauguza figo hata kupata usingizi ni shida. Muda unaotumika kuutibu huo ugonjwa through dialysis pia ni mwingi.

Epukeni ujinga
 
Afadhali ufe kwa ajali kwa maana hautakuwa umegharamika kwa matibabu. Wakati unauguza figo hata kupata usingizi ni shida. Muda unaotumika kuutibu huo ugonjwa through dialysis pia ni mwingi.

Epukeni ujinga
Na ni expensivie sana hizo dialysis services , ni familia ngapi au watu wangapi wenye uwezo wa kugharamia hiyo dialysis ambayo ni pesa ndefu kwa mwezi ?
Watu hawatumii akili kabisa
Watu wanatengeneza vifo vyao wenyewe ,ni ujinga
 
Na ni expensivie sana hizo dialysis services , ni familia ngapi au watu wangapi wenye uwezo wa kugharamia hiyo dialysis ambayo ni pesa ndefu kwa mwezi ?
Watu hawatumii akili kabisa
Watu wanatengeneza vifo vyao wenyewe ,ni ujinga
Stupidity is like a disease. Someone thinks kutibu ugongwa wa figo ni sawa na kutibu homa
 
Wakuu kiufupi kwa maisha ya sasa hatuwezi kutoboa,,,,, haijalishi wewe ni mnywaji pombe ama la

Kuna visababishi vingi Sana vya magonjwa yasiyoambukizwa hususan figo, ini nk.

1. Pombe
Hii itabaki kuwa ni sababu mojawapo kutokana na unywaji holela, pombe Kali kuuzwa bei rahisi, pombe feki nk

2. Matunda
Wengi wetu tunaamini tupo salama Sana kula matunda, ila kiukwel ni hatar Sana
Matunda yanatokana na mbegu za maabara (GMO) sio Yale matunda ya asili tena

Mbolea za sumu ndo zinatumika kuyakuza, dawa za sumu za kuua wadudu kipindi cha ukuaji, dawa ambazo zinapigwa Hadi siku ya mavuno na tunazibugiza vyakutosha

3. Mboga za majani
Kama ilivyo kwa matunda, mkulima anapiga dawa usiku asubuhi zinavunwa zinapelekwa sokoni dawa ambayo ilibidi ipigwe siku tatu kabla ya kuvuna

4. Vinywaji baridi (carbonated drinks)na energies
Vinywaji hivi vina kiwango kikubwa cha sukari na sumu (preservatives) na vimekuwa ni sehemu ya kawaida ya milo yetu kila siku

5. Kutokufanya mazoezi
Katika Hali ya kawaida mazoezi ni muhimu kwa afya, pata picha mtu anatumia vitu vyote hapo juu ( 1 Hadi 4) halaf hafanyi mazoezi

6. Matumizi holela ya madawa
Pharmacy wanauza dawa hovyo hovyo ni wewe Tu kwenda na hela yako unapata dawa yeyote unayoitaka na kutumia unavyotaka wewe
Watu wanatumia madawa bila kupima, bila ya maelekezo ya daktari, bila ya kufuata mtiririko wa dozi, bila kumaliza dozi, kuchangia dawa,,,, dawa inanunuliwa inatumiwa na familia nzima kila mtu kwa wakati wake

YOYE HAYO UKICHANGANYA KWA PAMOJA UNATEGEMEA NINI HAPO?
 
Hapo vyote si ishu hapo
Umesahau jambo kubwa ambalo karibu 80% Kwa ambao hawana matatizo yoyote Yale ila FIGO zinafeli ghafra basi ni kutokana
Matumizi yasiyo SAHIHI ya ANTIBIOTIC

AZUMA(Azithromycin)
POWERSELF SINDANO (ceftriaxone)
DOXYCYCLINE(tetracycline)
ZINDOLIN(Ciprofloxacin)

Hizo dawa ndio zinawaondoa VIJANA wengi Kwa FIGO kuferi 7bu ya NGONO zembe DISPENSARY ucharwa za mtaani
kumeza hovyo hovyo unavyofeel dalili za U.T.I
Kuna wengine wanatembea na Ciprofloxacin(ZINDOLIN) au AZUMA mfukoni
Akimaliza kut*mba tu anabwia hiyo midawa

FIGO zitaachaje kufeli
AZUMA ni dawa za nini??

Maana kuna madam nilimsikia anaonbgea na simu anatamka dr kampa hiyo azuma azuma.
 
Back
Top Bottom