Uoga : Eneo lililotajwa kutumika na Lissu kwa Mkutano wa Kampeni Jimbo la Serengeti labadilishwa matumizi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426


Viongozi wa Chadema wa Jimbo la Serengeti wameongea na Waandishi wa habari ili kutoa ratiba kamili ya Mgombea wao wa Urais Mh Tundu Lissu ndani ya jimbo hilo , ikiwa ni pamoja na kueleza eneo utakapofanyika mkutano huo.

Lakini cha kushangaza muda mfupi baadaye eneo hilo likasimikwa bango la kuzuia matumizi ya kisiasa ya eneo hilo .

Kuna haja ya Tume ya Uchaguzi kutoa mwongozo wa jambo hili ili kuepusha vurugu
 
Changamoto itakuwa Arusha maana vile viwanja vyote upinzani wanapokusanyikaga Gambo kavijenga..
 

Nguvu kubwa, za wazi na za makusudi zitatumika kuonyesha eneo lote la Sukumaland ni marufuku shughuli za upinzani kufanyika. Tutegemee matukio mengi eneo hilo.
 
Yaani ni kama Arusha 2015 maeneo yote ya wazi yalibadilishiwa matumizi. Hivi sasa Arusha jiji hakuna eneo la wazi. Kisa Chadema.
 
Kawaida kiwanja chochote kabla kutumia unatakiwa kuomba kibali Cha mwenye kiwanja Sasa mfano mimi Nina kiwanja changu chamazi Cha AZam ukiambiwa ujaze utakapofanyia mkutano wako utajazaje jina la kiwanja changu Wakati hujawasiliana nami?

Na kwa kuwa Ni changu Nina Uhuru wa kubadili matumizi Wakati wowote
 
Mwenye mali ana uhuru wa kuamua eneo lake litumike kwa shughuli za kisiasa au lah, msiwapangie wananchi, huo ndio uhuru wenyewe.
 
Ndio mjue kuwa watu hawawapendi na mmechokwa. Watu hawali ndege au madaraja.
 
Hilo ango ni la kihuni kwanini lisimikwe Usiku
Ng'oeni bango watu watafute uhuru wao kutoka katika huu utawala wa mkoloni mweusi
Sheria ya ardhi inahusika huwezi ingia eneo la mtu bila ridhaa yake ndio maana viwanja huombwa vibali kwa wenye navyo kuvitumia hujiingilii tu

Huo ndio utawala wa sheria Lisu abaoupigia kelele . Kiwanja changu Nina hati nacho wewe unajiingiza kimabavu haikubaliki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…