Uonevu dhidi ya Lissu: Watanzania hatuwezi kuendelea kuitwa taifa lenye akili halafu tukanyamazie ujinga wa mamlaka

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
533
Reaction score
1,499
Wana JF heshima mbele!

Kwa anayefuatilia kesi ya Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu kwa umakini na kwa kutumia misingi sahihi ya taaluma ya sheria, bila ushabiki wa kisiasa, ataona wazi kuwa hii si kesi ya jinai, bali ni maigizo ya kisheria yaliyopangwa na watu wasiolitakia mema taifa hili. Sheria iliyotumika kumfungulia Lissu mashtaka ya uhaini ni Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania (Penal Code Cap. 16, R.E. 2022), hususan Kifungu cha 39(a) na 40 ambavyo vinahusu kosa la "treason" (uhaini) na “treasonable offences”.

Lakini ndugu zangu, ukichambua kwa kina matamshi, misimamo, na kauli alizowahi kuzitoa Tundu Lissu katika majukwaa ya siasa, utaona wazi kuwa hakuna hata moja inayofikia threshold ya kosa la uhaini kisheria. Kifungu cha 39 kinazungumzia mtu anayetenda tendo kwa madhumuni ya kumwondoa au kumdhuru Rais wa Jamhuri, au kubadilisha serikali kwa nguvu au njia zisizo halali. Hakuna ushahidi wowote—kwa mujibu wa rekodi zilizowekwa mahakamani—unaodhihirisha kuwa Lissu alihamasisha mapinduzi au kushiriki mpango wa kijeshi au wa uasi dhidi ya mamlaka halali ya kiserikali. Hili ni kosa la kuzua, kulazimisha na kubambikiza, huku nia ikiwa si ya haki bali ya kumkomesha kisiasa.

Kosa la upande wa Jamhuri ni dhahiri. Kwa mujibu wa sheria hiyo hiyo, Kifungu cha 39(3) kinatoa tafsiri pana kuhusu vitendo vinavyoweza kuchukuliwa kama uhaini, lakini pia kinabainisha wazi kuwa lazima pawepo na ushahidi wa intentional and actual act ya kuhatarisha usalama wa taifa. Lissu hakuwahi kuwa na access ya kijeshi, wala hakutoa agizo la kuandaa silaha wala kuongoza uasi. Msimamo wa kisiasa si uasi. Kukosoa serikali si uhaini. Hii ni abuse of the criminal justice system kwa kiwango cha aibu na cha kihuni, ambapo prosecution inageuzwa chombo cha kutisha wapinzani, siyo kutenda haki.

Kutokana na uelewa huo huo wa sheria, tunaweza kusema kwa nguvu zote kwamba kesi hii inapaswa kutupiliwa mbali kwa msingi wa utetezi wa kikatiba, hususan Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayotoa haki ya kutoa maoni na uhuru wa kujieleza. Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Tafsiri ya Sheria (Interpretation of Laws Act, Cap 1), sheria yoyote inapaswa kutafsiriwa kwa mtazamo wa haki, mantiki, na maslahi ya umma. Hii kesi ya Lissu ni politically motivated indictment ambayo inalenga kuzima sauti ya uzalendo wa kweli.

Kwa mantiki hiyo, ikiwa mahakama itakubaliana na hoja za kisheria na kutupilia mbali kesi hii ya uhaini, basi ni wazi kuwa upande wa Jamhuri utakuwa umetenda kosa la jinai na kiutawala. Tunaweza kutumia Kifungu cha 96 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA – Criminal Procedure Act, Cap. 20 R.E. 2022) ambacho kinazuia matumizi mabaya ya taratibu za mahakama (abuse of process) na pia tukafungua shauri dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kutumia mamlaka vibaya kinyume cha Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba, inayolinda haki ya kusikilizwa kwa haki na bila upendeleo.

Hili ni jambo la kitaifa. Hatuwezi kuendelea kuwa taifa linalotumia sheria kuendesha visasi vya kisiasa. Wakili wa Serikali aliyesoma sheria na kuapa kuitumikia haki, hawezi kwa dhamira safi kuandaa mashtaka ya uhaini dhidi ya mtu kwa msingi wa kisiasa, halafu ajidai kuwa anatetea taifa. Taifa gani linalohitaji kulindwa dhidi ya mdomo wa mtu anayesema ukweli? Ni lini kusema “serikali imepotoka” kuligeuka kosa la jinai? This is not law – this is political thuggery in legal disguise!

Kwa kuhitimisha, kama taifa hatutakuwa na ujasiri wa kupinga maovu haya kwa kutumia sheria hizo hizo wanazozitumia kutubana, basi tusitarajie kupata taifa la haki. Sisi Watanzania si majuha. Tunaelewa sheria, tunaelewa haki, na tunajua tofauti kati ya utawala wa sheria (rule of law) na utawala wa mabavu kwa kivuli cha sheria. Na kama sisi hatutazungumza, basi ukimya wetu utatafsiriwa kama ridhaa.

TUNAKATAA!
 
Kesi inayohusu Chadema judge anatupilia mbali na kuamua papo kwa papo
Kesi ambayo CCM ina maslahi judge anapiga huku na huku, kama ndumila kuwili, anajidai anamsikiliza Lissu lakini baadaye anakuja na Lakini ati tuwape muda Jamhuri. Hapo ndiyo tulipofikia.

Kwa sasa hivi kurudisha Imani kwa Polisi, Mahakama na hata Majeshi yote kazi ngumu sana. Ni kama nchi haina dereva. Kama nisemavyo kila siku, hakuna " Rule of Law", bali kuna "Rule by Law"
 
Wana JF heshima mbele!

Kwa anayefuatilia kesi ya Mheshimiwa Tundu A

Kwa kuhitimisha, kama taifa hatutakuwa na ujasiri wa kupinga maovu haya kwa kutumia sheria hizo hizo wanazozitumia kutubana, basi tusitarajie kupata taifa la haki. Sisi Watanzania si majuha. Tunaelewa sheria, tunaelewa haki, na tunajua tofauti kati ya utawala wa sheria (rule of law) na utawala wa mabavu kwa kivuli cha sheria. Na kama sisi hatutazungumza, basi ukimya wetu utatafsiriwa kama ridhaa.

TUNAKATAA!
Unless umezaliwa baada ya 1980s, ila kwa sisi tuliokuwapo tuna kumbukumbu ya kesi ya Lugangira aka Uncle Tom na MacGhee na wenzao akina Hanspope, Eugene Maganga, Mbogoro, Banyikwa etc waliotaka kumpindua Rais Nyerere mwaka 1982/3.

Serikali haikusubiri wapindue ndiyo iwashitaki. Kwa sasa iachie Mahakama ifanye kazi yake
 
Hao uliowataja huoni miongoni mwao kuna waliowahi kuwa wanajeshi?

Askari ana access na silaha tofauti na raia asiye na umiliki hata wa kisu halafu unasema anataka kupindua nchi?
 
Wewe ndiyo Muongo. Akina Lugangira, Yule Kanali aliyepigwa Risasi Kinondoni, akina Hanspope wote walikamatwa tu baada ya kukamilisha mbinu zao, TISS ya wakati ule walikuwa nao ndani kujifanya nao wamo hadi ma TAXI drivers,

Sasa kwa nini yule Kanali alipigwa risasi, si baada ya kutaka kushikwa akatoa bunduki, msitetee uongo, wale Shaidi X wa zama za Mahiga siyo kama huyu doria wa mtandao anayetumia sijui version gani, hata hajui ku-jail break.
 
Wana JF heshima mbele!

Kwa anayefuatilia kesi ya Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu kwa umakini na kwa kutumia misingi sahihi ya taaluma ya sheria, bila ushabiki wa kisiasa, ataona wazi kuwa hii si kesi ya jinai, bali ni maigizo ya kisheria yaliyopangwa na watu wasiolitakia mema taifa hili. Sheria iliyotumika kumfungulia Lissu mashtaka ya uhaini ni Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania (Penal Code Cap. 16, R.E. 2022), hususan Kifungu cha 39(a) na 40 ambavyo vinahusu kosa la "treason" (uhaini) na “treasonable offences”.

Lakini ndugu zangu, ukichambua kwa kina matamshi, misimamo, na kauli alizowahi kuzitoa Tundu Lissu katika majukwaa ya siasa, utaona wazi kuwa hakuna hata moja inayofikia threshold ya kosa la uhaini kisheria. Kifungu cha 39 kinazungumzia mtu anayetenda tendo kwa madhumuni ya kumwondoa au kumdhuru Rais wa Jamhuri, au kubadilisha serikali kwa nguvu au njia zisizo halali. Hakuna ushahidi wowote—kwa mujibu wa rekodi zilizowekwa mahakamani—unaodhihirisha kuwa Lissu alihamasisha mapinduzi au kushiriki mpango wa kijeshi au wa uasi dhidi ya mamlaka halali ya kiserikali. Hili ni kosa la kuzua, kulazimisha na kubambikiza, huku nia ikiwa si ya haki bali ya kumkomesha kisiasa.

Kosa la upande wa Jamhuri ni dhahiri. Kwa mujibu wa sheria hiyo hiyo, Kifungu cha 39(3) kinatoa tafsiri pana kuhusu vitendo vinavyoweza kuchukuliwa kama uhaini, lakini pia kinabainisha wazi kuwa lazima pawepo na ushahidi wa intentional and actual act ya kuhatarisha usalama wa taifa. Lissu hakuwahi kuwa na access ya kijeshi, wala hakutoa agizo la kuandaa silaha wala kuongoza uasi. Msimamo wa kisiasa si uasi. Kukosoa serikali si uhaini. Hii ni abuse of the criminal justice system kwa kiwango cha aibu na cha kihuni, ambapo prosecution inageuzwa chombo cha kutisha wapinzani, siyo kutenda haki.

Kutokana na uelewa huo huo wa sheria, tunaweza kusema kwa nguvu zote kwamba kesi hii inapaswa kutupiliwa mbali kwa msingi wa utetezi wa kikatiba, hususan Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayotoa haki ya kutoa maoni na uhuru wa kujieleza. Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Tafsiri ya Sheria (Interpretation of Laws Act, Cap 1), sheria yoyote inapaswa kutafsiriwa kwa mtazamo wa haki, mantiki, na maslahi ya umma. Hii kesi ya Lissu ni politically motivated indictment ambayo inalenga kuzima sauti ya uzalendo wa kweli.

Kwa mantiki hiyo, ikiwa mahakama itakubaliana na hoja za kisheria na kutupilia mbali kesi hii ya uhaini, basi ni wazi kuwa upande wa Jamhuri utakuwa umetenda kosa la jinai na kiutawala. Tunaweza kutumia Kifungu cha 96 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA – Criminal Procedure Act, Cap. 20 R.E. 2022) ambacho kinazuia matumizi mabaya ya taratibu za mahakama (abuse of process) na pia tukafungua shauri dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kutumia mamlaka vibaya kinyume cha Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba, inayolinda haki ya kusikilizwa kwa haki na bila upendeleo.

Hili ni jambo la kitaifa. Hatuwezi kuendelea kuwa taifa linalotumia sheria kuendesha visasi vya kisiasa. Wakili wa Serikali aliyesoma sheria na kuapa kuitumikia haki, hawezi kwa dhamira safi kuandaa mashtaka ya uhaini dhidi ya mtu kwa msingi wa kisiasa, halafu ajidai kuwa anatetea taifa. Taifa gani linalohitaji kulindwa dhidi ya mdomo wa mtu anayesema ukweli? Ni lini kusema “serikali imepotoka” kuligeuka kosa la jinai? This is not law – this is political thuggery in legal disguise!

Kwa kuhitimisha, kama taifa hatutakuwa na ujasiri wa kupinga maovu haya kwa kutumia sheria hizo hizo wanazozitumia kutubana, basi tusitarajie kupata taifa la haki. Sisi Watanzania si majuha. Tunaelewa sheria, tunaelewa haki, na tunajua tofauti kati ya utawala wa sheria (rule of law) na utawala wa mabavu kwa kivuli cha sheria. Na kama sisi hatutazungumza, basi ukimya wetu utatafsiriwa kama ridhaa.

TUNAKATAA!
Kwa kuhitimisha, kama taifa hatutakuwa na ujasiri wa kupinga maovu haya kwa kutumia sheria hizo hizo wanazozitumia kutubana, basi tusitarajie kupata taifa la haki. Sisi Watanzania si majuha. Tunaelewa sheria, tunaelewa haki, na tunajua tofauti kati ya utawala wa sheria (rule of law) na utawala wa mabavu kwa kivuli cha sheria. Na kama sisi hatutazungumza, basi ukimya wetu utatafsiriwa kama ridhaa.📌📌📌📌❗🔨🔨🔨🔨
 
Serikali ya CCM ni kuogopa ushindani wa uchaguzi.
IMG_1793.jpeg
 
Unless umezaliwa baada ya 1980s, ila kwa sisi tuliokuwapo tuna kumbukumbu ya kesi ya Lugangira aka Uncle Tom na MacGhee na wenzao akina Hanspope, Eugene Maganga, Mbogoro, Banyikwa etc waliotaka kumpindua Rais Nyerere mwaka 1982/3.

Serikali haikusubiri wapindue ndiyo iwashitaki. Kwa sasa iachie Mahakama ifanye kazi yake
Hata katika kesi ya Uncle Tom, kulikuwapo ushahidi wa vitendo vya kijeshi na njama halisi. Lissu hajatenda lolote linalofikia threshold ya actus reus ya uhaini. Kutumia historia ya njama halisi kuhalalisha tuhuma hewa ni intellectual dishonesty na ni hatari kwa utawala wa sheria.
 
Unless umezaliwa baada ya 1980s, ila kwa sisi tuliokuwapo tuna kumbukumbu ya kesi ya Lugangira aka Uncle Tom na MacGhee na wenzao akina Hanspope, Eugene Maganga, Mbogoro, Banyikwa etc waliotaka kumpindua Rais Nyerere mwaka 1982/3.

Serikali haikusubiri wapindue ndiyo iwashitaki. Kwa sasa iachie Mahakama ifanye kazi yake

Hawa walifanya conspiracy/njama na walikuwa na mpango kamili/execution plan! Na walikua na qualification (maafisa wa jeshi) na walikua na access ya vifaa vya kupindulia. Sasa Lissu kuongea kwenye majukwaa haina tofauti na mtu kunena kwenye baa za kimpumu kule matombo, so mifano haina mfanano hata chembe!

Atapindulia youtube? Basi hakuna serikali kama inaweza kupinduliwa kwa kunena kwa lugha, shandakararara kairobo nakishabababababo! Mama huyo nduki anaacha ikulu

Halafu mtoa mada nani alisema tuna akili? Sina kumbukumbu nifahamishage kenge mwenzio
 
Kunasisiku hata hilo neno sheria haitokuwa na nguvu...ni pale watoto,vijana na wazee tutakaposimama na kusema serikali ivunjwe na ianzishwe mpa....nitajitolea ucaptain na nitaongoza vyema msururu wangu wa wapiganaji.....
Unasema Wazee gani? Wazee wa Dar? JK kila akitaka kuhalalisha uovu anaofanya alikua anaita wazee wa Dar, hao ndiyo sample representative ya wazee wa Tanzania, alikuwa anawahutubia kulishwa sumu wanaishia kuimba CCM CCM, na hapo ujue wameambiwa Pesa ya ITPL ya Escrow ni yenu (ya UMMA) au si ya UMMA, wanakubali siyo ya umma na kukubali siyo fedha yao. Angalia hao wazee wana chembe ya IQ? Hayo yote, Pamoja na yote inatakiwa reforms za hali ya juu. Factor ya Mtu kama Lissu, ndiyo inaingia hapo. REFORMS of the mindset
 
Hao uliowataja huoni miongoni mwao kuna waliowahi kuwa wanajeshi?

Askari ana access na silaha tofauti na raia asiye na umiliki hata wa kisu halafu unasema anataka kupindua nchi?
Kwani kuna njia moja tu ya kupindua nchi?

Kwani hao niliowataja walikutwa na bunduki?
 
Unless umezaliwa baada ya 1980s, ila kwa sisi tuliokuwapo tuna kumbukumbu ya kesi ya Lugangira aka Uncle Tom na MacGhee na wenzao akina Hanspope, Eugene Maganga, Mbogoro, Banyikwa etc waliotaka kumpindua Rais Nyerere mwaka 1982/3.

Serikali haikusubiri wapindue ndiyo iwashitaki. Kwa sasa iachie Mahakama ifanye kazi yake

..kama ulifuatilia kesi ya uhaini ya MacGhee, na wenzake, basi hutasita ku-conclude kwamba Tundu Lissu sio mhaini, na watawala wamelenga kumtesa tu.
 
Wewe ndiyo Muongo. Akina Lugangira, Yule Kanali aliyepigwa Risasi Kinondoni, akina Hanspope wote walikamatwa tu baada ya kukamilisha mbinu zao, TISS ya wakati ule walikuwa nao ndani kujifanya nao wamo hadi ma TAXI drivers,

Sasa kwa nini yule Kanali alipigwa risasi, si baada ya kutaka kushikwa akatoa bunduki, msitetee uongo, wale Shaidi X wa zama za Mahiga siyo kama huyu doria wa mtandao anayetumia sijui version gani, hata hajui ku-jail break.
Kuna njia nyingi za kutibua mipango ya uhaini na kila njia inategemea mazingira yake. Aliyepigwa risasi ni Captain Tamimu.

Huwezi kulazimisha approach zifanane kati ya Uasi wa Tundu na tuko la akina Lugangira.

Mtu anakuambia atafanya uasi kuzuia uchaguzi wa Oktoba, na wewe unasubiri ifike Oktoba ndiyo uchukue hatua. Hiyo itakuwa ni Jamhuri ya ndizi (Banana Republic )
 
Wale walikua ni wanajeshi huyu kaweka ni vifungu vilivyokiukwa Wewe unaleta Ushabiki mandazi kwenye mambo ya Kitaifa ngoja nikujulisha serikali ni kikundi cha watu wa chache Leo kipo kesho kutwa hakipo tuwe wazalendo kwa nchi sio serikali
 
Wana JF heshima mbele!

Kwa anayefuatilia kesi ya Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu kwa umakini na kwa kutumia misingi sahihi ya taaluma ya sheria, bila ushabiki wa kisiasa, ataona wazi kuwa hii si kesi ya jinai, bali ni maigizo ya kisheria yaliyopangwa na watu wasiolitakia mema taifa hili. Sheria iliyotumika kumfungulia Lissu mashtaka ya uhaini ni Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania (Penal Code Cap. 16, R.E. 2022), hususan Kifungu cha 39(a) na 40 ambavyo vinahusu kosa la "treason" (uhaini) na “treasonable offences”.

Lakini ndugu zangu, ukichambua kwa kina matamshi, misimamo, na kauli alizowahi kuzitoa Tundu Lissu katika majukwaa ya siasa, utaona wazi kuwa hakuna hata moja inayofikia threshold ya kosa la uhaini kisheria. Kifungu cha 39 kinazungumzia mtu anayetenda tendo kwa madhumuni ya kumwondoa au kumdhuru Rais wa Jamhuri, au kubadilisha serikali kwa nguvu au njia zisizo halali. Hakuna ushahidi wowote—kwa mujibu wa rekodi zilizowekwa mahakamani—unaodhihirisha kuwa Lissu alihamasisha mapinduzi au kushiriki mpango wa kijeshi au wa uasi dhidi ya mamlaka halali ya kiserikali. Hili ni kosa la kuzua, kulazimisha na kubambikiza, huku nia ikiwa si ya haki bali ya kumkomesha kisiasa.

Kosa la upande wa Jamhuri ni dhahiri. Kwa mujibu wa sheria hiyo hiyo, Kifungu cha 39(3) kinatoa tafsiri pana kuhusu vitendo vinavyoweza kuchukuliwa kama uhaini, lakini pia kinabainisha wazi kuwa lazima pawepo na ushahidi wa intentional and actual act ya kuhatarisha usalama wa taifa. Lissu hakuwahi kuwa na access ya kijeshi, wala hakutoa agizo la kuandaa silaha wala kuongoza uasi. Msimamo wa kisiasa si uasi. Kukosoa serikali si uhaini. Hii ni abuse of the criminal justice system kwa kiwango cha aibu na cha kihuni, ambapo prosecution inageuzwa chombo cha kutisha wapinzani, siyo kutenda haki.

Kutokana na uelewa huo huo wa sheria, tunaweza kusema kwa nguvu zote kwamba kesi hii inapaswa kutupiliwa mbali kwa msingi wa utetezi wa kikatiba, hususan Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayotoa haki ya kutoa maoni na uhuru wa kujieleza. Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Tafsiri ya Sheria (Interpretation of Laws Act, Cap 1), sheria yoyote inapaswa kutafsiriwa kwa mtazamo wa haki, mantiki, na maslahi ya umma. Hii kesi ya Lissu ni politically motivated indictment ambayo inalenga kuzima sauti ya uzalendo wa kweli.

Kwa mantiki hiyo, ikiwa mahakama itakubaliana na hoja za kisheria na kutupilia mbali kesi hii ya uhaini, basi ni wazi kuwa upande wa Jamhuri utakuwa umetenda kosa la jinai na kiutawala. Tunaweza kutumia Kifungu cha 96 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA – Criminal Procedure Act, Cap. 20 R.E. 2022) ambacho kinazuia matumizi mabaya ya taratibu za mahakama (abuse of process) na pia tukafungua shauri dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kutumia mamlaka vibaya kinyume cha Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba, inayolinda haki ya kusikilizwa kwa haki na bila upendeleo.

Hili ni jambo la kitaifa. Hatuwezi kuendelea kuwa taifa linalotumia sheria kuendesha visasi vya kisiasa. Wakili wa Serikali aliyesoma sheria na kuapa kuitumikia haki, hawezi kwa dhamira safi kuandaa mashtaka ya uhaini dhidi ya mtu kwa msingi wa kisiasa, halafu ajidai kuwa anatetea taifa. Taifa gani linalohitaji kulindwa dhidi ya mdomo wa mtu anayesema ukweli? Ni lini kusema “serikali imepotoka” kuligeuka kosa la jinai? This is not law – this is political thuggery in legal disguise!

Kwa kuhitimisha, kama taifa hatutakuwa na ujasiri wa kupinga maovu haya kwa kutumia sheria hizo hizo wanazozitumia kutubana, basi tusitarajie kupata taifa la haki. Sisi Watanzania si majuha. Tunaelewa sheria, tunaelewa haki, na tunajua tofauti kati ya utawala wa sheria (rule of law) na utawala wa mabavu kwa kivuli cha sheria. Na kama sisi hatutazungumza, basi ukimya wetu utatafsiriwa kama ridhaa.

TUNAKATAA!
Hili ni tatizo kubwa saana nchi, ambalo linaua system zima ya nchi , maana tatizo hili linaambukiza toka juu kwenda chini, na toka wizara moja kwenda nyingine, matokeo yake tuna kuwa Taifa la majuha kama ulivyosema na hata wanaofurahi huo utovu wa maadili NK IPO siku watoto au ndugu, zao watapata adha kutoka kwa watu waliotendea vibaya na wewe
 
Wewe ndiyo Muongo. Akina Lugangira, Yule Kanali aliyepigwa Risasi Kinondoni, akina Hanspope wote walikamatwa tu baada ya kukamilisha mbinu zao, TISS ya wakati ule walikuwa nao ndani kujifanya nao wamo hadi ma TAXI drivers,

Sasa kwa nini yule Kanali alipigwa risasi, si baada ya kutaka kushikwa akatoa bunduki, msitetee uongo, wale Shaidi X wa zama za Mahiga siyo kama huyu doria wa mtandao anayetumia sijui version gani, hata hajui ku-jail break.
Umemjibu vizuri sana. 👍
 
Wale walikua ni wanajeshi huyu kaweka ni vifungu vilivyokiukwa Wewe unaleta Ushabiki mandazi kwenye mambo ya Kitaifa ngoja nikujulisha serikali ni kikundi cha watu wa chache Leo kipo kesho kutwa hakipo tuwe wazalendo kwa nchi sio serikali
Mahakama itachambua mbivu ma mbichi, lakini isingewezekana kuifumbia macho kauli ya Tundu
 
Kuna njia nyingi za kutibua mipango ya uhaini na kila njia inategemea mazingira yake. Aliyepigwa risasi ni Captain Tamimu.

Huwezi kulazimisha approach zifanane kati ya Uasi wa Tundu na tuko la akina Lugangira.

Mtu anakuambia atafanya uasi kuzuia uchaguzi wa Oktoba, na wewe unasubiri ifike Oktoba ndiyo uchukue hatua. Hiyo itakuwa ni Jamhuri ya ndizi (Banana Republic )
Kama hoja yako ni "kuzuia uchaguzi" ni uhaini, basi kila mwito wa maandamano au civil disobedience utahesabiwa uasi? Huo si utawala wa sheria, ni authoritarian paranoia. Lissu alizungumza, hakupanga mapinduzi. Kumpa kesi ya uhaini bila mens rea wala actus reus ni kuigeuza Tanzania kuwa Banana Republic halisi. Acha kutetea ujinga kwa kutumia akili za kipuuzi
 
Back
Top Bottom