Uonevu dhidi ya Lissu: Watanzania hatuwezi kuendelea kuitwa taifa lenye akili halafu tukanyamazie ujinga wa mamlaka

Uonevu dhidi ya Lissu: Watanzania hatuwezi kuendelea kuitwa taifa lenye akili halafu tukanyamazie ujinga wa mamlaka

Mtafanayaje?? Hamna cha kufanya.
 
Leta risiti ya kuuzia nchi tuione hapa. Mabwege mmekalia kalalamika tu, fursa zinapita kazi yenu kuchonga mdomo. Mkipewa kazi kwenye mashirika ya umma mnaiba na mashirika yanakufa. Kuyakodisha kwa wawekezaji siyo kuyauza. Angalia TBL, TCC, Twiga Cement, NMB. Kama Mkapa angewasikia pimbi kama nyinyi miaka 1995-2005 leo hii tusingekuwa na mashirika haya hata moja.

Samia amekabidhi usimamizi wa TPA kwa DP WORLD na Mwendokasi nao anatoa kwa kampuni ya ESG kutoka UAE. Watapiga kazi mpaka mshangae
1000211033.jpg

Nchi inaenda kubaya itauzwa
 
Ndiyo. Yule kanali aliyeuawa maeneo ya kinondoni alikuwa anajibizana risasi kwa risasi na alipoishiwa Alidandia gari la breweries akaawa anawarushia wakamataji chupa za bia. Upo mkongwe?
Kweli, nilifika hadi eneo la tukio kwenye saa 1.00 jioni hivi. Sekeseke lilianzia nyumbani kwa George Banyikwa pale maeneo ya Drive Inn, ndipo akina Mabere Marando na timu yao walipowavamia akina Lugangira. Waliweza kuwakamata wote kasoro captain Tamimu ambaye alitumia mbinu za kikomando ku-escape.

Ndipo akikimbia akakutana na lori la TBL, akarukia na kuanza kuwashiana risasi kama sinema
 
View attachment 3376781
Nchi inaenda kubaya itauzwa
Angalia deliveries linganisha na mkopo!! Kila leo mnafurahi kupanda SGR kwenda Dodoma na Moro mnadhani imejengwa kwa mikojo ya mama zenu?

Angalia Bwawa la Nyerere, daraja la Wami, daraja la Busisi, mashule na hospitali kwenye wilaya mbalimbali. Mnaongelea deni lakini hakuna mtu ana match na deliverables za Samia
20250610_072519.jpg
 
Leta risiti ya kuuzia nchi tuione hapa. Mabwege mmekalia kalalamika tu, fursa zinapita kazi yenu kuchonga mdomo. Mkipewa kazi kwenye mashirika ya umma mnaiba na mashirika yanakufa. Kuyakodisha kwa wawekezaji siyo kuyauza. Angalia TBL, TCC, Twiga Cement, NMB. Kama Mkapa angewasikia pimbi kama nyinyi miaka 1995-2005 leo hii tusingekuwa na mashirika haya hata moja.

Samia amekabidhi usimamizi wa TPA kwa DP WORLD na Mwendokasi nao anatoa kwa kampuni ya ESG kutoka UAE. Watapiga kazi mpaka mshangae
WEwe ni mwehu haki ya Mungu. Kumbe na bishana na mpumbavu. Walio ua miradi yoote ni hao hao unao watetea maCCM mkuu upo sawa kweli toka uhuru kuna chama nje ya CCM kilikamataga dollar hiii. ? Kuna mtu wa upinzan amehusika na kuanzisha miradi inayofeli..? Kuna kiongozi au chama cha upinzani kimeua shirika lolote..?
Sasa kwa akili zako za kipumbavu nikuulize tena. Majizi yoote ya CCM anzia awamu ya mwinyi mkapa kikwete jpm na mama yenu umesikia mwizi yeyote alikamatwa kwa ubadhirifu ili hali ripoti za CAG unazisikia kila mwaka..? Mikataba yoote ya kiwendawazimu umesikia kuwa upinzan wametia saini ..?
Wewe ni mtu ambae tukikuwahi unabadilika
 
Angalia deliveries linganisha na mkopo!! Kila leo mnafurahi kupanda SGR kwenda Dodoma na Moro mnadhani imejengwa kwa mikojo ya mama zenu?

Angalia Bwawa la Nyerere, daraja la Wami, daraja la Busisi, mashule na hospitali kwenye wilaya mbalimbali. Mnaongelea deni lakini hakuna mtu ana match na deliverables za Samia
View attachment 3376784
Vitu vya kufanyika karne ya 20 ndivyo mnajigamba karne ya 21 upo sawa kweli. Jiulize kwann mataifa yaliyo pata uhuru karibia na sisi leo yapo mbali saana kila idara
 
Hivi wewe kuwaita watu wajinga hapa, nani mjinga?
Fikiria Lissu angekuwa na hayo majeshi nchi ingekuwa wapi?
Ukichanganya CCM yote (ile cream), ni chini ya Tundu Lissu mmoja.
Mlichofanya ni kumfunyia ukatili baada ya kumchapa risasi 38
Sasa mmemuweka gerezani na wafungwa waliohukumiwa kunyongwa
Barbaric & Sadists
Angefanya haya haya ambayo mnadhani ccm inakosea.

Kwa hiyo mnaposhulikiwa na CCM komaeni maana siku mkishinda na wao mtawashighulikia.

Sasa unataka nani akuonee huruma?
 
Sikiliza hapa tena, halafu jifanye wewe ni TISS DG, au IGP au CDF, je ungecheka na nyani?
View attachment 3376488
Lazima tutunze amani yetu kwa wivu wa hali ya juu. Mbwa ukimdekeza atakufuata hadi msikitini
Mkuu, ref. hiyo clip yako. Inaonyesha mhusika anazungumza na watu wengine, namna ya utekelezaji wa hicho unachodai ni "UHAINI", sasa kwa nini hao wengine ambao kwa mtazamo wako walikuwa wanapanga mpango huo, HAWA KUKAMATWA PAMOJA NAYE kwenye huo mpango wa uhaini?
 
Tu
Tuliza tako vyombo vyetu viko makini sana
Sasa tusi la nini wakati comment yangu haina hata chembe ya kumdhihaki mtu?

Au nikuripoti kwa wahusika kisha waone ulicho comment kama ni sawa ama lah?

Kama huna cha kuchangia ni vema kukaa kimya mkuu sio lazima ujibu.
 
More......
Wakati huo wanapanga kumuua Nyerere kupindua nchi walikuwa wanajeshi.
Sasa Lissu mmoja anabwabwaja jukwaani no reforms no election anafanyaje uhaini?
Ndicho nilichohoji hata mimi mkuu.
 
Sikiliza hapa tena, halafu jifanye wewe ni TISS DG, au IGP au CDF, je ungecheka na nyani?
View attachment 3376488
Lazima tutunze amani yetu kwa wivu wa hali ya juu. Mbwa ukimdekeza atakufuata hadi msikitini
Njama huwa inapangwa na mtu mmoja?

Kama kweli pangekuwa na elements za kupanga njama za kinachoitwa uasi/uhaini basi wahusika wote wa njama hizo wangekamatwa.

Kama huna uelewa na masuala ya kisheria basi kwa kusikiliza clip hiyo unaweza kudhani kuna offense yoyote lakini kiuhalisia ni maneno ya kisiasa kama yalivyo maneno mengine.
 
Wana JF heshima mbele!

Kwa anayefuatilia kesi ya Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu kwa umakini na kwa kutumia misingi sahihi ya taaluma ya sheria, bila ushabiki wa kisiasa, ataona wazi kuwa hii si kesi ya jinai, bali ni maigizo ya kisheria yaliyopangwa na watu wasiolitakia mema taifa hili. Sheria iliyotumika kumfungulia Lissu mashtaka ya uhaini ni Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania (Penal Code Cap. 16, R.E. 2022), hususan Kifungu cha 39(a) na 40 ambavyo vinahusu kosa la "treason" (uhaini) na “treasonable offences”.

Lakini ndugu zangu, ukichambua kwa kina matamshi, misimamo, na kauli alizowahi kuzitoa Tundu Lissu katika majukwaa ya siasa, utaona wazi kuwa hakuna hata moja inayofikia threshold ya kosa la uhaini kisheria. Kifungu cha 39 kinazungumzia mtu anayetenda tendo kwa madhumuni ya kumwondoa au kumdhuru Rais wa Jamhuri, au kubadilisha serikali kwa nguvu au njia zisizo halali. Hakuna ushahidi wowote—kwa mujibu wa rekodi zilizowekwa mahakamani—unaodhihirisha kuwa Lissu alihamasisha mapinduzi au kushiriki mpango wa kijeshi au wa uasi dhidi ya mamlaka halali ya kiserikali. Hili ni kosa la kuzua, kulazimisha na kubambikiza, huku nia ikiwa si ya haki bali ya kumkomesha kisiasa.

Kosa la upande wa Jamhuri ni dhahiri. Kwa mujibu wa sheria hiyo hiyo, Kifungu cha 39(3) kinatoa tafsiri pana kuhusu vitendo vinavyoweza kuchukuliwa kama uhaini, lakini pia kinabainisha wazi kuwa lazima pawepo na ushahidi wa intentional and actual act ya kuhatarisha usalama wa taifa. Lissu hakuwahi kuwa na access ya kijeshi, wala hakutoa agizo la kuandaa silaha wala kuongoza uasi. Msimamo wa kisiasa si uasi. Kukosoa serikali si uhaini. Hii ni abuse of the criminal justice system kwa kiwango cha aibu na cha kihuni, ambapo prosecution inageuzwa chombo cha kutisha wapinzani, siyo kutenda haki.

Kutokana na uelewa huo huo wa sheria, tunaweza kusema kwa nguvu zote kwamba kesi hii inapaswa kutupiliwa mbali kwa msingi wa utetezi wa kikatiba, hususan Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayotoa haki ya kutoa maoni na uhuru wa kujieleza. Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Tafsiri ya Sheria (Interpretation of Laws Act, Cap 1), sheria yoyote inapaswa kutafsiriwa kwa mtazamo wa haki, mantiki, na maslahi ya umma. Hii kesi ya Lissu ni politically motivated indictment ambayo inalenga kuzima sauti ya uzalendo wa kweli.

Kwa mantiki hiyo, ikiwa mahakama itakubaliana na hoja za kisheria na kutupilia mbali kesi hii ya uhaini, basi ni wazi kuwa upande wa Jamhuri utakuwa umetenda kosa la jinai na kiutawala. Tunaweza kutumia Kifungu cha 96 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA – Criminal Procedure Act, Cap. 20 R.E. 2022) ambacho kinazuia matumizi mabaya ya taratibu za mahakama (abuse of process) na pia tukafungua shauri dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kutumia mamlaka vibaya kinyume cha Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba, inayolinda haki ya kusikilizwa kwa haki na bila upendeleo.

Hili ni jambo la kitaifa. Hatuwezi kuendelea kuwa taifa linalotumia sheria kuendesha visasi vya kisiasa. Wakili wa Serikali aliyesoma sheria na kuapa kuitumikia haki, hawezi kwa dhamira safi kuandaa mashtaka ya uhaini dhidi ya mtu kwa msingi wa kisiasa, halafu ajidai kuwa anatetea taifa. Taifa gani linalohitaji kulindwa dhidi ya mdomo wa mtu anayesema ukweli? Ni lini kusema “serikali imepotoka” kuligeuka kosa la jinai? This is not law – this is political thuggery in legal disguise!

Kwa kuhitimisha, kama taifa hatutakuwa na ujasiri wa kupinga maovu haya kwa kutumia sheria hizo hizo wanazozitumia kutubana, basi tusitarajie kupata taifa la haki. Sisi Watanzania si majuha. Tunaelewa sheria, tunaelewa haki, na tunajua tofauti kati ya utawala wa sheria (rule of law) na utawala wa mabavu kwa kivuli cha sheria. Na kama sisi hatutazungumza, basi ukimya wetu utatafsiriwa kama ridhaa.

TUNAKATAA!
Hichi uliachoandika, wewe ndio umekuwa kielelezo cha ujinga na unyumbu.
 
Mkuu, ref. hiyo clip yako. Inaonyesha mhusika anazungumza na watu wengine, namna ya utekelezaji wa hicho unachodai ni "UHAINI", sasa kwa nini hao wengine ambao kwa mtazamo wako walikuwa wanapanga mpango huo, HAWA KUKAMATWA PAMOJA NAYE kwenye huo mpango wa uhaini?
Wenyewe wapelelezi wanajuwa kwa nini wanemdaka kiranja kwanza. Usikute hao watakuja kama mashahidi baadaye, au wakaunganishwa ikibidi
 
Njama huwa inapangwa na mtu mmoja?

Kama kweli pangekuwa na elements za kupanga njama za kinachoitwa uasi/uhaini basi wahusika wote wa njama hizo wangekamatwa.

Kama huna uelewa na masuala ya kisheria basi kwa kusikiliza clip hiyo unaweza kudhani kuna offense yoyote lakini kiuhalisia ni maneno ya kisiasa kama yalivyo maneno mengine.
Hata mbuyu ulianza kama mchicha. Genocide ya 1994 Rwanda ilipaishwa na kauli za Radio inaitwa Mille Collines na Kabendera Shinani (RIP) alikuwa mtangazaji huko.

Usipo deal na symptoms itakuwa vigumu kutatua tatizo likikomaa. Mzarau mwiba huota tende.

Mtu anakuambia tutakinukisha ili kuvuruga uchaguzi, kweli umuache tu bila ya kumhoji??

Tuwe serious, Tundu alileta dharau kwa mamlaka, mwache ajifunze kwa mwalimu ulimwengu
 
Ukizungumzia kwa muktadha wa mtazamo wako upo sahihi,ila tukizungumzia kwa muktadha Sheria hakuna ingredients za kutengeneza njama za uasi/uhaini.
 
Back
Top Bottom