Mahakama itachambua mbivu ma mbichi, lakini isingewezekana kuifumbia macho kauli ya Tundu
..Mahakama imeoza haina uwezo wa kutenda haki.
Mahakama itachambua mbivu ma mbichi, lakini isingewezekana kuifumbia macho kauli ya Tundu
Mwenye kufanya uasi hatangazi mipango yake hadharani (akina eugene na wenzie hawakutangaza), tuna viongoz wa ccm wakitangaza kwa maneno ya kutisha hivyo hivyo, halaf wakaachwa.Kuna njia nyingi za kutibua mipango ya uhaini na kila njia inategemea mazingira yake. Aliyepigwa risasi ni Captain Tamimu.
Huwezi kulazimisha approach zifanane kati ya Uasi wa Tundu na tuko la akina Lugangira.
Mtu anakuambia atafanya uasi kuzuia uchaguzi wa Oktoba, na wewe unasubiri ifike Oktoba ndiyo uchukue hatua. Hiyo itakuwa ni Jamhuri ya ndizi (Banana Republic )
Hajajibu vizuri.Umemjibu vizuri sana. 👍
Tatizo anaongea actual facts, shida moja tu watawala hawapendi kusikia ukweliSipendi kinachoendelea hasa kwa mtu anayetembea na vipande vya risasi mwilini.
Shida yake ni moja, anaongea sana.
Sipendi kinachoendelea hasa kwa mtu anayetembea na vipande vya risasi mwilini.
Shida yake ni moja, anaongea sana.
Mtu anayetembea na risasi mwilini haogopi kitu kwa vile tayari alikwisha chungulia kaburi. Kwa hiyo anataka na wengine tuchungulie kaburiSipendi kinachoendelea hasa kwa mtu anayetembea na vipande vya risasi mwilini.
Shida yake ni moja, anaongea sana.
Huo ni mtazamo wako.Hajajibu vizuri.
Wanasheria naomba mtusaidie hapa:.Sasa Lissu kuongea kwenye majukwaa haina tofauti na mtu kunena kwenye baa za kimpumu kule matombo, so mifano haina mfanano hata chembe!
Kama mtu aliyejaa risasi mwilini bado anapaza sauti, hiyo si "anaongea sana" bali ni manifesto ya uzalendo hai. Ukatili aliofanyiwa unampa haki ya kupaza sauti zaidi, si kufungwa midomo. Ukiukwaji wa haki, madeni ya kizembe, ukandamizaji – kama haya hayasemiwe, basi tunastahili giza la kimfumo.Sipendi kinachoendelea hasa kwa mtu anayetembea na vipande vya risasi mwilini.
Shida yake ni moja, anaongea sana.
Si ndio maana kesi ipo mahakamani ili kujua mbivu na mbichi?Wana JF heshima mbele!
Kwa anayefuatilia kesi ya Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu kwa umakini na kwa kutumia misingi sahihi ya taaluma ya sheria, bila ushabiki wa kisiasa, ataona wazi kuwa hii si kesi ya jinai, bali ni maigizo ya kisheria yaliyopangwa na watu wasiolitakia mema taifa hili. Sheria iliyotumika kumfungulia Lissu mashtaka ya uhaini ni Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania (Penal Code Cap. 16, R.E. 2022), hususan Kifungu cha 39(a) na 40 ambavyo vinahusu kosa la "treason" (uhaini) na “treasonable offences”.
Lakini ndugu zangu, ukichambua kwa kina matamshi, misimamo, na kauli alizowahi kuzitoa Tundu Lissu katika majukwaa ya siasa, utaona wazi kuwa hakuna hata moja inayofikia threshold ya kosa la uhaini kisheria. Kifungu cha 39 kinazungumzia mtu anayetenda tendo kwa madhumuni ya kumwondoa au kumdhuru Rais wa Jamhuri, au kubadilisha serikali kwa nguvu au njia zisizo halali. Hakuna ushahidi wowote—kwa mujibu wa rekodi zilizowekwa mahakamani—unaodhihirisha kuwa Lissu alihamasisha mapinduzi au kushiriki mpango wa kijeshi au wa uasi dhidi ya mamlaka halali ya kiserikali. Hili ni kosa la kuzua, kulazimisha na kubambikiza, huku nia ikiwa si ya haki bali ya kumkomesha kisiasa.
Kosa la upande wa Jamhuri ni dhahiri. Kwa mujibu wa sheria hiyo hiyo, Kifungu cha 39(3) kinatoa tafsiri pana kuhusu vitendo vinavyoweza kuchukuliwa kama uhaini, lakini pia kinabainisha wazi kuwa lazima pawepo na ushahidi wa intentional and actual act ya kuhatarisha usalama wa taifa. Lissu hakuwahi kuwa na access ya kijeshi, wala hakutoa agizo la kuandaa silaha wala kuongoza uasi. Msimamo wa kisiasa si uasi. Kukosoa serikali si uhaini. Hii ni abuse of the criminal justice system kwa kiwango cha aibu na cha kihuni, ambapo prosecution inageuzwa chombo cha kutisha wapinzani, siyo kutenda haki.
Kutokana na uelewa huo huo wa sheria, tunaweza kusema kwa nguvu zote kwamba kesi hii inapaswa kutupiliwa mbali kwa msingi wa utetezi wa kikatiba, hususan Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inayotoa haki ya kutoa maoni na uhuru wa kujieleza. Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Tafsiri ya Sheria (Interpretation of Laws Act, Cap 1), sheria yoyote inapaswa kutafsiriwa kwa mtazamo wa haki, mantiki, na maslahi ya umma. Hii kesi ya Lissu ni politically motivated indictment ambayo inalenga kuzima sauti ya uzalendo wa kweli.
Kwa mantiki hiyo, ikiwa mahakama itakubaliana na hoja za kisheria na kutupilia mbali kesi hii ya uhaini, basi ni wazi kuwa upande wa Jamhuri utakuwa umetenda kosa la jinai na kiutawala. Tunaweza kutumia Kifungu cha 96 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA – Criminal Procedure Act, Cap. 20 R.E. 2022) ambacho kinazuia matumizi mabaya ya taratibu za mahakama (abuse of process) na pia tukafungua shauri dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa kutumia mamlaka vibaya kinyume cha Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba, inayolinda haki ya kusikilizwa kwa haki na bila upendeleo.
Hili ni jambo la kitaifa. Hatuwezi kuendelea kuwa taifa linalotumia sheria kuendesha visasi vya kisiasa. Wakili wa Serikali aliyesoma sheria na kuapa kuitumikia haki, hawezi kwa dhamira safi kuandaa mashtaka ya uhaini dhidi ya mtu kwa msingi wa kisiasa, halafu ajidai kuwa anatetea taifa. Taifa gani linalohitaji kulindwa dhidi ya mdomo wa mtu anayesema ukweli? Ni lini kusema “serikali imepotoka” kuligeuka kosa la jinai? This is not law – this is political thuggery in legal disguise!
Kwa kuhitimisha, kama taifa hatutakuwa na ujasiri wa kupinga maovu haya kwa kutumia sheria hizo hizo wanazozitumia kutubana, basi tusitarajie kupata taifa la haki. Sisi Watanzania si majuha. Tunaelewa sheria, tunaelewa haki, na tunajua tofauti kati ya utawala wa sheria (rule of law) na utawala wa mabavu kwa kivuli cha sheria. Na kama sisi hatutazungumza, basi ukimya wetu utatafsiriwa kama ridhaa.
TUNAKATAA!
Sikiliza hapa tena, halafu jifanye wewe ni TISS DG, au IGP au CDF, je ungecheka na nyani?Kama hoja yako ni "kuzuia uchaguzi" ni uhaini, basi kila mwito wa maandamano au civil disobedience utahesabiwa uasi? Huo si utawala wa sheria, ni authoritarian paranoia. Lissu alizungumza, hakupanga mapinduzi. Kumpa kesi ya uhaini bila mens rea wala actus reus ni kuigeuza Tanzania kuwa Banana Republic halisi. Acha kutetea ujinga kwa kutumia akili za kipuuzi
Hoja zako zina uzito wa kitaaluma na zinagusa kiini cha tatizo—criminal liability chain. Lakini kwa mujibu wa Article 59B(4) ya Katiba na National Prosecutions Act, DPP ana constitutional discretion ya kuchuja jalada kabla ya kuendesha mashtaka. Hivyo, uzembe wa kipelelezi haumuondolei DPP dhamana ya kikatiba ya kuhakikisha haki haitumiki vibaya. Akishindwa kufanya due diligence, naye anabeba dhima ya kimaadili na kisheria.Tatizo ni tafsiri za kisheria pamoja na mienendo ya kisheria haitafsiriwi kisiasa, lakini pia kuna sehemu kubwa umejitahidi kuelezea sakata zima kisheria nakubaliana na wewe.
Ila sasa, kuna mahali umeshindwa kupata tafsiri na nini hasa hutokea kwenye makosa yote ya jinai.
Ipo hivi kwenye nazingira kama haya hauwezi kutupa lawama zako kwa DPP na ofisi nzima ya NPS wala hauwezi ilaumi Mahakama. Katika mazingira kama haya uliyoelezea wakulaumiwa ni Ofisi ya upelelezi na mpelelezi/wapelelezi wa jalada pamoja na askari wakamataji
Hawa ndio mtu unaweza kusema hata aada ya shauri kuonekana halikai kwenye kosa ndio unaweza kusema uwashtaki na sababu ni kuwa wao wanajua misingi ya makosa ya jinai na walifahamu kuwa aina ya tukio haliangukii kwenye kosa la jinai. Hivyo walifanya uzembe wa kitaaluma kwahiyo unawashtaki wao kama wao binafsi. Ukienda hivyo unaweza fanikiwa, lakini ukishtaki kwa madai ya kushtakiwa kwa hila hautaweza kutoboa.
Tukiacha haya niliyoyasema ngoja na mimi niongezee nyama kidogo kwanini inaonekana kosa aliloshtakiwa nalo Mh. Lisu halina ushahidi au muunganiko wa kuwa kosa la jinai.
Zipo sababu nyingi sana lakini zote zinaanguka kwenye misingi tano yakutokea kosa la jinai
1. Tukio liwe kosa la jinai kisheria: sasa hapa swali ni je tukio lililofanywa na Mh. Lisu ni kosa la jinai kisheria?, hapa kuna tafsiri pana sana hasa ikizingatiwa ilikuwa ni misimamo binafsi na maoni yake, hapa kuna 60% ya tukio kutokuwa jinai kisheria.
2. Kitendo kufanyika: sasa hapa tunajiuliza ni kitendo kipi kimefanyika?, ukiangalia vizuri utagundua kilichofanyika ni maoni binafsi ya mtu sasa je maoni binafsi yanaweza kuwa jinai au uchochezi wa ghadia? Hapa ni 50% kwa aina ya maoni aliyoyatoa.
3. Wazo ovu: Sasa hapa napo kina walakini sana kama kweli Mh. Lisu alikuwa na wazo ovu ambalo kwa kosa aliloshitakiwa nalo linaweza kuonekana. Hii ni kwasababu aina ya mawazi yake ni mtazamo wa yajayo hasa wakati wa kumtafuta kiongozi wa nchi ambapo hatakuwa aliyepo wakati huo. (Hapa ni pagumu) tuwape 30%
4. Muunganiko wa wazo ovu na kitendo kilichofanyika: Hapa ndipo mizani inazidi kuwaacha Jamhuri na upande mzima wa mashtaka. Hakijafanyika kitendo chochote kuelekea wazo ovu kama lipo. Hapa ni pagumu sana landa tuweke 10%
5. Madhara yaliyotokea: Huu ni mlima mrefu sana kwa upande wa mashtaka. Ni yapi madhara yaliyosababishwa na yote hayo?, ukiangalia hakina taharuki na kuithibitisha taharuki ni jambo gumu hasa kwenye mazingira ya kisiasa tuwape 5%
Ni mjadala mpana sana lakini bado Jamhuri wana faida ya kwenda kujaribu kuyaonesha makosa yaliyotendwa na hapa ndipo tunapoona ombwe kwenye mnyororo mzima wa haki jinai ambao pia uliongelewa sana na ile Tume ya haki jinai.
Lakini labda tusubiri huwenda hii kesi ikabadili falsafa ya haki jinai nchini.
Ndiyo maana kesi iko Mahakamani, kushindwa kwa Serikali kuthibitisha basi ndiyo kuachiwa huru kwa Tundu.Mwenye kufanya uasi hatangazi mipango yake hadharani (akina eugene na wenzie hawakutangaza), tuna viongoz wa ccm wakitangaza kwa maneno ya kutisha hivyo hivyo, halaf wakaachwa.
Tukiita double standard mtu utakataa?
Kesi ni politicaly motivated sababu serikal inashindwa hata ku prove , kesi ina sua sua sababu shahidi mwenyewe hajui cha ku represent
Ni upotevu wa muda na rasilimal
Wanasheria naomba mtusaidie hapa:.
Hivi mtu akiwa bar akasema tumuue rais, haitakuwa kosa kwa kuwa kashika chupa ya bia mkononi?
Vipi kama mahakama ikitafsiri kuwa Lisu alitamka jukwaani kuhusu uasi lkn huwenda alitumika kama msemaji wa kundi kubwa la waasi lilio nyuma yake?
Kisheria, kosa la jinai linahitaji actus reus (kitendo) na mens rea (nia ovu), lakini pia lazima pawe na capacity to execute the threat. Kauli ya mtu akiwa bar au jukwaani, bila imminent threat au organized capacity, hubaki kuwa political rhetoric au idle talk.Wanasheria naomba mtusaidie hapa:.
Hivi mtu akiwa bar akasema tumuue rais, haitakuwa kosa kwa kuwa kashika chupa ya bia mkononi?
Vipi kama mahakama ikitafsiri kuwa Lisu alitamka jukwaani kuhusu uasi lkn huwenda alitumika kama msemaji wa kundi kubwa la waasi lilio nyuma yake?
Huo si utawala wa sheria, bali ni burden-shifting fallacy. Utawala wa sheria (rule of law) hauanzi mahakamani, unaanza kwenye maamuzi ya kupeleka mtu kizimbani. Kama kesi haina msingi, hatua ya kumshtaki tayari ni ukiukaji wa haki (malicious prosecution). Mahakama si chombo cha kuchuja uzembe wa DPP ni ya kutoa haki, si kusafisha hila.Ndiyo maana kesi iko Mahakamani, kushindwa kwa Serikali kuthibitisha basi ndiyo kuachiwa huru kwa Tundu.
Na huo ndiyo utawala wa sheria