Uonevu dhidi ya Lissu: Watanzania hatuwezi kuendelea kuitwa taifa lenye akili halafu tukanyamazie ujinga wa mamlaka

OKTOBA TUNATIKI
 
Tu
Hao uliowataja huoni miongoni mwao kuna waliowahi kuwa wanajeshi?

Askari ana access na silaha tofauti na raia asiye na umiliki hata wa kisu halafu unasema anataka kupindua nchi?
Tuliza tako vyombo vyetu viko makini sana
 
Uy
Kunasisiku hata hilo neno sheria haitokuwa na nguvu...ni pale watoto,vijana na wazee tutakaposimama na kusema serikali ivunjwe na ianzishwe mpa....nitajitolea ucaptain na nitaongoza vyema msururu wangu wa wapiganaji.....
We bwege utasimama na watoto wako
 
Wanasheria naomba mtusaidie hapa:.

Hivi mtu akiwa bar akasema tumuue rais, haitakuwa kosa kwa kuwa kashika chupa ya bia mkononi?
Kwa hawa "wapiga doria mtandaoni" unprofessional wa Bi Chura Kiziwi, huu unaweza kuwa ni uhaini of the highest level😄. Ataburutwa mahakamani wallahi🤔
Vipi kama mahakama ikitafsiri kuwa Lisu alitamka jukwaani kuhusu uasi lkn huwenda alitumika kama msemaji wa kundi kubwa la waasi lilio nyuma yake?
Kulitafsiri Neno "uasi" hakuanzii na kuishia kwenye akili na vichwa vya watu wa Samia a.k.a Chura Kiziwi pekee. Tunapaswa kutoka kwenye tafsiri za vichwa vyao, twende kwenye tafsiri pana na huru zaidi..

Kauli ya Tundu Lissu siku ile ilikuwa very clear kusadifu na kufafanusha mantiki inayobebwa na hoja na kaulimbiu ya NO REFORMS NO ELECTION..

He clearly said; ".....Yes, tutafanya uasi dhidi ya mifumo mibaya, isiyo haki ya chaguzi zetu..."

Kukataa kukubaliana na kupinga (kuasi) sheria na taratibu mbaya za kisiasa, za dhuluma na zisizo haki za uchaguzi ili kupata viongozi tangu lini inahesabiwa kuwa ni uhaini...?

On the other hand yes, ana kundi kubwa lililo nyuma ya Tundu Lissu (kina sisi wananchi) litakalofanya uasi wa mifumo mibovu, isiyo haki na dhuluma ya chaguzi zetu kwa kutokwenda kupiga kura ikiwa ni ujumbe kuwa, reforms kwanza ili tupate mifumo ya kisheria na taratibu za haki na usawa ili tuwe na chaguzi huru, za haki, wazi na za kuaminika kwa wote ndipo tuingie kwenye sanduku la kura. Kama huu ni uhaini, basi tubadlishe sheria zetu Ili kutambua uhaini huu!!
 
Be blessed dear lawyer for sharing with me this very useful knowledge
 
Aisee! Asante, maana Kuna "wanasheria" wa vijiweni (bush lawyers) wasema yao huku mitaani.
 
Tatizo anaongea actual facts, shida moja tu watawala hawapendi kusikia ukweli
Mtawala aliepita baada ya kukosolewa alitamani kumuangamiza. Mungu akamuokoa. Mtawala wa pili nae kamsingizia uhaini. Najiuliza hawa watawala wanahofia nini kwa tundu lisu?
 
Kama nyie wajinga ndio mlimtuma acholoze nyuki nenda kamtoe unataka kumshirikisha nani kwenye upuuzi wenu?
 
Huenda huna ufahamu wa kutosha juu ya kesi Ile ya kina uncle Tom na wenzake. Hawa wote walikuwa wanajeshi Tena baadhi yao wakiwa na vyeo na viapo vya utii wa katiba na walikuwa pia viongozi ndani ya jeshi kwa maana waliweza kumobilize wengine kujiunga nao ili watimize adhima yao pia walikuwa na access ya zana za kivita yaani silaha.
Lissu hana kiapo chochote Cha kikatiba Wala silaha, hivyo anakosa sifa za kuwa mhaini au muasi. Nilikuwepo mahakamani na kimsingi nilikijifunza mengi kwa kuifuatilia Ile kesi. Maua yao mawakili wa utetesi kina Lamwai na yule mhindi nimemsahau jina.
 
Kwani kuna njia moja tu ya kupindua nchi?

Kwani hao niliowataja walikutwa na bunduki?
Ndiyo. Yule kanali aliyeuawa maeneo ya kinondoni alikuwa anajibizana risasi kwa risasi na alipoishiwa Alidandia gari la breweries akaawa anawarushia wakamataji chupa za bia. Upo mkongwe?
 
Kama nyie wajinga ndio mlimtuma acholoze nyuki nenda kamtoe unataka kumshirikisha nani kwenye upuuzi wenu?
Hivi wewe kuwaita watu wajinga hapa, nani mjinga?
Fikiria Lissu angekuwa na hayo majeshi nchi ingekuwa wapi?
Ukichanganya CCM yote (ile cream), ni chini ya Tundu Lissu mmoja.
Mlichofanya ni kumfunyia ukatili baada ya kumchapa risasi 38
Sasa mmemuweka gerezani na wafungwa waliohukumiwa kunyongwa
Barbaric & Sadists
 
Acha Mahakama ifanye kazi yake tuuone huo Ujinga kwenye Hukumu maana Serikali ina kazi ya kuhalalisha huo Uasi na Kukinukisha ili kumnyonga Lissu..
Siyo kila mtuhumiwa tayari ni mfungwa..
 
Hao uliowataja huoni miongoni mwao kuna waliowahi kuwa wanajeshi?

Askari ana access na silaha tofauti na raia asiye na umiliki hata wa kisu halafu unasema anataka kupindua nchi?
More......
Wakati huo wanapanga kumuua Nyerere kupindua nchi walikuwa wanajeshi.
Sasa Lissu mmoja anabwabwaja jukwaani no reforms no election anafanyaje uhaini?
 
We mbwa koko huu uchafu wako tafuta jukwaa la kuupeleka, this is rubbish! Subiri maamuzi ya mahakama, ni mwehu tu atasoma haya matope. We u nani kuzungumzia na kuitolea maamuzi shauri lililoko mahakamani?
Una shida Gani kwenye ubongo wako? Huwezi kusoma bandiko la mwenzako na ukapita tu bila kucomment Kama limekukwaza? Ona lugha uliyoitumiq hapa, ikirejeshwa kwako Kama ulivyolandika utajisikiaje? Kuwa na kifua Cha kustaamili yake unayoona siyo sawa kwako na siyo kupachika waleta hoja majina yenye kukaraisha! Sijapenda!
 
Thomas Lugangira, Zera Banyikwa, George Banyikwa walikuwa wanajeshi wa jeshi gani?

Acheni kuweka simulizi za kuambiwa. Nilikuwa naishi Kinondoni Manyanya, na Tamimu kauliwa Mkwajuni akiwa kweye gari ya Bia
 
Nchi inalindwa kwa kuuzwa..? Wewe n mwehu abduli anaishi dubai ww upo bonyokwa unalipwa 7000 ya bando kutetea majizi
Leta risiti ya kuuzia nchi tuione hapa. Mabwege mmekalia kalalamika tu, fursa zinapita kazi yenu kuchonga mdomo. Mkipewa kazi kwenye mashirika ya umma mnaiba na mashirika yanakufa. Kuyakodisha kwa wawekezaji siyo kuyauza. Angalia TBL, TCC, Twiga Cement, NMB. Kama Mkapa angewasikia pimbi kama nyinyi miaka 1995-2005 leo hii tusingekuwa na mashirika haya hata moja.

Samia amekabidhi usimamizi wa TPA kwa DP WORLD na Mwendokasi nao anatoa kwa kampuni ya ESG kutoka UAE. Watapiga kazi mpaka mshangae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…