Uongo gani mkubwa uliwahi kuongopewa na mwenza wako ukaja kujua ukweli?

Uongo gani mkubwa uliwahi kuongopewa na mwenza wako ukaja kujua ukweli?

ERoni alinidanganya ana migodi ya dhahabu, nikajisemea nimejiokotea sonko langu. Bwana bwana, kuja kugundua yule mpare hana hata baiskeli. Wapare sio watu.
Nakuibia siri......
Katika watu ambao hutakiwi kuwaamini wakiwa Wana tongoza ni wapare.......
1002298161.jpg
 
Habari wakuuu,

Kama tunavyojua kwenye harakati au maisha ya kimapenzi tunakutana na misuko suko ya hapa na pale, misuko suko ambayo inatufanya tuyachukie mapenzi au mahusiano.

Moja ya mambo yaliyoshamiri kwenye ndoa na mahusiano ya nyakati hizi ni UONGO uliokithiri.

Mimi binafsi niliwahi kuongopewa ujauzito na binti mmoja miaka ya nyuma kwa kuwa tulikuwa tukiishi mikoa tofauti na nilikuwa namuamini sikumtilia shaka.

Pia soma: Jambo gani baya umewahi kumfanyia mpenzi wako na utajutia milele?

Nililea mimba mpaka miezi mitano ndipo dada yake alipokuja kuniambia baada ya kuwa na yeye alikuwa anakereka na jambo alilokuwa akinifanyia mdogo wake, baadae alikuja kukiri na kuniomba msamaha, Sikumsamehe.

Rafiki yangu na yeye ilimkuta kwa binti mmoja wa Kihehe mpaka mimba ikazaliwa baadae akasema mtoto amekufa.

Je, wewe ndugu uliwahi kukutana na uongo upi kwenye ulimwengu wetu wa mapenzi?
Kisa kama cha ndugu yangu mmoja hivi.

Sema yeye alilea ile Mimba mpaka Binti akaja kujifungua na alipotangaziwa kuwa nina mimba yako walianza kuishi kama Mme na Mke.

Jamaa alipata shida na ile mimba na kwa sehemu ilimcheleweshea harakati zake nyingi sana za utafutaji.

Baada ya kujifungua kuna siku anamkuta mzee mtu mzima na mkewe wako chocho, ndo binti anafunguka hii mimba nilikubambikizia tu. Dah!

Jamaa alifanya mapenzi na binti mimba ikiwa na wiki za mwanzo kwaiyo ili kutoifedheesha familia yake(Binti) na ya yule mwanamume (Mzee) akaamua ampe jamaa yangu.

Nae alikuwa na hamu ya kuoa kweli. kaoa kumbe kaoa mke wa mtu aisee.

Jamaa yangu asaivi anamke wake fresh na familia ya watoto wawili na mambo yanaenda vizuri sana.

Hata sijui yule mwanamke aliishia wapi na mume wa mtu tena mzee mtu mzima sana.
 
Back
Top Bottom