Kisa kama cha ndugu yangu mmoja hivi.
Sema yeye alilea ile Mimba mpaka Binti akaja kujifungua na alipotangaziwa kuwa nina mimba yako walianza kuishi kama Mme na Mke.
Jamaa alipata shida na ile mimba na kwa sehemu ilimcheleweshea harakati zake nyingi sana za utafutaji.
Baada ya kujifungua kuna siku anamkuta mzee mtu mzima na mkewe wako chocho, ndo binti anafunguka hii mimba nilikubambikizia tu. Dah!
Jamaa alifanya mapenzi na binti mimba ikiwa na wiki za mwanzo kwaiyo ili kutoifedheesha familia yake(Binti) na ya yule mwanamume (Mzee) akaamua ampe jamaa yangu.
Nae alikuwa na hamu ya kuoa kweli. kaoa kumbe kaoa mke wa mtu aisee.
Jamaa yangu asaivi anamke wake fresh na familia ya watoto wawili na mambo yanaenda vizuri sana.
Hata sijui yule mwanamke aliishia wapi na mume wa mtu tena mzee mtu mzima sana.