Huu ni mtizamo wako tu na si Sheria ya ulimwengu. Usipowaelewa wengine na wewe usishangae wao kutokukuelewa wewe.
Kwanza nani aliye sema kwamba tuna elewana?
Binadamu hawawezi na hatuwezi kuelewana kwa sababu tuna mitazamo tofauti na
pasipo ku kubaliana binadamu hawawezi kuelewana.
Sheria zipo kwa sababu, Binadamu Hatu elewani. Lakini kupitia sheria wote tunalazimika kuelewana kupitia sheria inavyosema.
Hii Sheria ya kwamba Kila chenye chanzo ni Lazima kiwe na chanzo kingine unaziona kama ni kanuni timilifu?
Ndio ni kanuni timilifu ili pasiwepo "Maulizo" yeyote yale kuhusu chanzo cha kitu kingine. Maana na chenyewe lazima kiwe na chanzo chake.
Ili muundo ule ule ufuatwe, pasiwepo kitu kilicho jitokeza tu chenyewe bila chanzo chake maana kitavuruga muundo mzima, kitazua utata na maswali ya "Maulizo" kwamba kimewezaje kuwepo bila chanzo chake?
Kama kanuni hii si timilifu, Basi hata Dunia Haihitaji kuwa na chanzo.
Na si lazima dunia iwe imeumbwa.
Ila kama dunia lazima iwe imeumbwa na lazima dunia iwe na chanzo chake, Basi hata huyo Mungu lazima awe ame umbwa.
Ili muundo wa Kanuni hii ufuatwe, pasiwepo Maulizo ya nani kamuumba mwenzake.
Ni hivi👇
Kama Mungu Hana chanzo, Basi hata dunia si lazima iwe na chanzo.
Kama Dunia lazima iwe na chanzo, Basi hata Mungu lazima awe na chanzo.
Tuseme chanzo cha kokoto ni Mwamba. Jee chanzo cha mwamba ni nini?
Chanzo cha mwamba, ni mwamba wenyewe, Si lazima mwamba huo uwe na chanzo.
Ukianza kuweka ulazima wa mwamba huo uwe na chanzo, Tunarudi kule kule kwenye ile kanuni yetu ya kwamba 👇
Nani, ni chanzo wa chanzo cha mwamba?
Na Maulizo haya yata endelea to infinity (Endless)