@Infropreneur na @Smotor hebu tulijadli suala hili la kuwepo ama kutokuwepo kwa MUNGU kimantiki.
Mleta mada @Mayu na nyie ni lazima tukubaliane kwamba hoja ya Mungu kwamba yupo ama hayupo ni lazima ianzie kwenye hoja ya kuumbwa kwa ulimwengu
Kama huamini kuwa kuna Mungu basi amini pia kuwa hakuna shetani. Na kama hakuna Mungu Wala shetani basi hakuna uwezo wa kupima mema ama mabaya.
Logical non sequitur
Mbona hakuna Mungu wala shetani ila bado tunaweza kupima mema na mabaya!?
Maana jambo linakuwa jema ama baya kwa kigezo gani? Mtu akizini, akiiba, akisema uongo, akiua au akisingizia mtu, haliwezi kuwa jambo jema ama baya Kwa kuwa hakuna chanzo cha kuonesha jambo husika kama ni jema ama baya
Logical non sequitur
Wewe umeathirika na mapokeo ya dini.
Unataka kusema kuwa ubaya ni lazima awepo shetani!?
Habari ya lipi jema lipi baya ni tafsiri ya ubongo tu.
Kigezo cha kujua hayo ni kupima mambo ambayo ukifanyiwa wewe utafurahi ama utachukia.
Kama huamini kuwa kuna Mungu, basi usiuchukie ushoga!!!
Logical non sequitur
Ninaweza nikawa siamini na nkauchukia ama nisiuchukie ushoga.
Issue ni tafsiri ya ubongo.!!
Wapinga Mungu husema kwamba dunia imeibuka tu toka kusikojulikana mamilioni kadhaa ya miaka iliyopita.
Unauhakika na madai haya!?
Lakini kabla hatujaenda mbali sana jee nyie akili zenu zinawatuma kwamba ulimwengu ulianzaje na ni kwa nini nyie mmetokeza kuwa binadamu na siyo Ng'ombe!!
Kwasababu ulimwengu unatanuka kila siku, inaonesha kabisa kuwa Ulimwengu ulianza katika nukta ndogo na ulikuwa na kiwango kikubwa cha nishati kilichojaa katika eneo dogo sana ndio ukaanza kutanuka.
ulimwengu wetu ulianza kutoka hali ya joto na mnururisho mwingi sana miaka bilioni kama 13.8 iliyopita.
Kisha, ghafla ulimwengu ulianza kupanuka kwa kasi kubwa.Hii ilisababisha joto na nishati kuanza kupoa na kuruhusu atomi na molekuli kuunda na kutokea. Baada ya mamilioni ya miaka, ulimwengu ulianza kuwa na muundo unaofanana na ulivyo leo, na nyota, sayari, na vitu vingine vyote vilivyopo katika ulimwengu wetu vilianza kutengenezeka
kugunduliwa kwa mnururisho wa cosmic microwave background (CMB) na uwezo wa kuona ulimwengu ukiongezeka kwa kasi kwa kutumia darubini za anga ni ushahidi wa madai haya.
Viumbe vimetokea vyenyewe,
reaction mbalimbali za kikemia zilisababisha viumbe kutokea
Vitu kama RNA, DNA vilitangulia.
Miller experiment ilikuwa jaribio la kujaribu kuelewa jinsi molekuli za kikaboni zinaweza kuundwa katika hali ya zamani ya dunia, inayofanana na ile iliyokuwepo kabla ya kuwepo kwa uhai. Experiment hii ililenga kujenga hali ya "dunia ya zamani" katika maabara na kuchunguza ikiwa hali hiyo inaweza kutoa molekuli za kikaboni, ambazo ni muhimu kwa uhai.
Miller alianzisha mfumo wa maabara uliokuwa na viungo vya kemikali muhimu katika ulimwengu wa zamani, kama vile methane (CH4), ammonia (NH3), maji (H2O), na hidrojeni (H2). Kisha alitumia umeme kuigiza umeme wa radi katika anga la zamani ya dunia.
Baada ya siku kadhaa za majaribio, Miller aligundua kuwa mfumo wake ulikuwa umetengeneza asidi amino, ambazo ni vitengo muhimu vya kujenga protini, molekuli muhimu kwa uhai. Hii ilikuwa ni moja ya ushahidi wa awali wa jinsi molekuli za kikaboni zinaweza kuundwa kutoka kwa viungo vya kikemia katika mazingira yanayofanana na yale ya zamani ya dunia.
Sisi ni binadamu na sio ng'ombe Because of Natural selection.
Unaweza kuthibitisha Mungu wako yupo?