Sawa ulimwengu haujaumbwa na umetokeza wenyewe tu. Lakini nani ana hakika kama ulimwengu umejitokeza tu hauna Mwanzo Wala mwisho??
Sijasema kwamba
"ulimwengu uli jitokeza wenyewe"
Kauli yako hii tayari ina zua maswali mengine kwamba ulijitokeza kutoka wapi? Na huko uliko jitokeza kulitoka wapi?
Nilisema na Nasema hivi, Ulimwengu upo tu, Hauna mwanzo wala mwisho.
Ukianza kuweka ulazima wa chanzo cha kitu fulani, basi hata hicho chanzo cha hicho kitu, kitahitaji chanzo.
Na hapa kutakuwa na Vyanzo vingi visivyokuwa na mwisho
(Endless sources) to infinity hukooooo....
Mantiki ni kujibu swali na si kushambulia wanaoamini kwamba Kuna Mungu.
Ndio najibu maswali hapa, sishambulii mtu.
Iko hivi 👇
Binadamu wote Hatuwezi kujua, Tusicho kujua ( ndio principle hii)
Ukisema unajua kitu fulani, lazima ueleze kitu hicho umekijuaje, na utoe uthibitisho wa jinsi ulivyo kijua na si mawazo yako ya kufikirika tu.
Lazima ueleze kitu hicho ulicho kijua, kipo kwa namna gani. Kwamba
je kina onekana, kinashikika, kinasikika au kinahisika?
USISEME kwamba ulikijua kitu hicho kwa mawazo yako tu ya kufikirika pasipo kuonyesha namna gani ulikijua na utoe uthibitisho angalau wa kuonekana, kushikika, kusikika, au wa kuhisika.
ili kitu hicho kisiwe mawazo yako ya kufikirika tu.
Jee unaweza kusema ni kwa nini wewe ni binadamu na si Ng'ombe??
Mimi ni Binadamu na si ng'ombe kwa vile, 👇
Kitu lazima kiwe kwa namna moja tu.
Kitu kimoja Hakiwezi kuwa kwa namna mbili kwa wakati mmoja.
Kama ni ng'ombe ni ng'ombe tu, ila sio Ng'ombe binadamu.
Na kama ni binadamu ni binadamu tu, ila sio Binadamu ng'ombe.
Ningeweza kuwa ng'ombe pia, Ila nisingeweza kuwa Binadamu.
Ila mimi ni Binadamu, Na siwezi na Haiwezekani niwe ng'ombe.
Logic imekamilika....📌🔨