Uongo na Ukweli Kuhusu TANESCO Kuzuiwa Kufanya Maintenance

Hizo hoja ni mfu if it ain’t broken why you tryna fix it?

Hizi mishe zote ni sababu ya Marope tu kuingizwa katika nafasi ya uwaziri wa nishati inaeleweka kabisa kuwa amewekwa pale si kwamba ni mmbora sana ila yupo kimkakati ili kukamilisha mipango ovu ya watu flani tu ambao atakula nao.

Siku zote mtu akiwa na jambo lake hakosi sababu hata mwanamke akitaka kukuacha lazma akupe mtihani ambao anajua lazma utaushindwa tu ili iwe kama sababu ya kukuacha.

Kusingizia maintanance ni utoto sababu hata kama ni hivyo unaweza fanya maintanance ya mitambo kwa phase bila kuathiri uzalishaji.
 
Wao wanapika data na kuja kuzikomalia wakati hali halisi haiakisi hizo data zao uchwara. Toka siku naskia Magufuli amefariki nilijua tu we are Doomed! Hata kifo chake siamini kwamba kilikuwa natural death ila postmortem imepikwa tu na safu ya wapigaji!

Yani nchi hii matatizo mengi yalikuwepo kwa ajili ya manufaa ya kundi la wachache. Watu wanasaini mikataba mibovu kwa siri ili kujiwekea ulinzi wa 10% katika mabilioni yanayonyonywa na mabeberu kila mwaka. Jamaa mmemua ila hamjaua impact yake kwa raia sababu mengi aliofanya yalileta matokeo chanya kwa public welfare.

Kudhihirisha hilo ni kurejea kwa matatizo ambayo yalishaanza kusahaulika it proves that barely JPM alikuwa kidume kweli.
 
Hahahhaha yani jamaa alikaa akaona bora apike data kuwa machine running hours zilikuwa nyingi kuliko ambazo zimewekwa kama standard before maintanance?

Ina maana kwa kipindi chote hicho cha Magufuli hakukuwahi kuwa na drought?
 
Hujajua tatizo lilipo.
Issue ni kuwa huko inapochimbwa sio yetu na hatuna hata hisa..
Hiki ndio kilimvuruga jiwe sikuzote.
Watu wanahisi Magufuli alikatalia hio gesi bila sababu ya msingi! Gesi hio inamilikiwa na mabeberu japo iko kwenye ardhi yetu ila mabeberu ndio wanahodhi kimkataba.
 
Hahahhaha yani jamaa alikaa akaona bora apike data kuwa machine running hours zilikuwa nyingi kuliko ambazo zimewekwa kama standard before maintanance?

Ina maana kwa kipindi chote hicho cha Magufuli hakukuwahi kuwa na drought?
Halafu anazungumzia kampuni moja tu Songas ambayo aipo kwenye control ya TANESCO.

Nyingine zote zinazozalisha umeme chini ya TANESCO mbona hakuna mahala wamezuiwa kufanya schedule maintance.

Si ajabu Songas ataki kupoteza hela anasubiri low season ya vyanzo vya maji ndio aombe maintance akijua atakataliwa, na mara ngapi kwa mwaka aliomba kufanya hizo maintance akanyimwa, sitoshangaa kama ni collusion tu.

Watu inabidi wawe makini na hawa mafisadi na hizi report za CAG sio kumeza nzima lazima tuulize pia to what extent pia walitaka ufafanuzi kutoka kwa mkonge wa taifa na time frame kabla ya kupewa majibu.

Sijaona sehemu ambayo taasisi ya TANESCO imezuiwa kufanya schedule maintance katika hadithi yake iliyotukuka.
 
Binafsi naona mradi wa bwawa la nyerere ni muhimu sana kwa maana tukiwa na mvua za kutosha tutazalisha umeme kwa bei rahisi hata hivyo mitambo ya umeme wa gesi nayo ni muhimu kwa kuwa ndiyo umeme wa uhakika kama kuna gesi ya kutosha na mitambo ya uhakika. Mambo ya kutegemea mvua kwa asilimia Mia moja nayo ni hatari pia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Tanesco waende na vitu hivyo kwa pamoja kwa ku balance ili mradi kuwe na umeme wa uhakika na wa bei nafuu, kwote kuna faida na hasara.
 
Maelezo yanajitosheleza, tatizo wachambuaji, na hali halisi.
Kwanza hali ya ukame uenda ni tatizo kubwa tofauti na miaka ya karibuni!
Pili migao uenda haikuwepo ingawa kukatika kwa umeme hakujawahi kukoma Nchi hii.
Tatu changanya kutofanyika matengenezo na upungufu wa maji, kumeshusha uzalishaji wa umeme kipindi hichi.
Nne kila mtu ana mtu wake humu jf, ambae alikuwa au yupo, na kwa upendo walionao hawataki kubebeshwa sehemu ya lawama kwa namna yeyote ile.
Tano lawama lazima wabebe ingawa ni sehemu, kwani ukame pia sehemu ya lawama lakini kwa hawamu zote ukianzia ya Mwinyi.
Mwisho serikali inakata miti sana kwa kutoa leseni na vibali kusafirisha magogo nje ya Nchi. Wananchi wanaambiwa tunzeni mazingira, msikate miti, wao wanasafirisha magogo kwa hatari, na hawana mpango wa kukoma, ukali wote wa Magu nilidhani biashara hii itakufa kumbe ndio ilishika kasi, ukame unasababishwa na serikali!
 
View attachment 2016058Hiyo ni Nov 20 2017

Kabla mungu wa wasukuma magu hajafa umeme wadau walikuwa wanaulalamikia sawa na sasa tu.
Acha ujinga mkuu, Mungu ni mumoja wivu wa kipumbavu huo. Ulitaka awe nani Rais au kabila gani. Haya ndo matokeo yake tunaburuzwa tu kwa kushindwa kutoa mawazo ya pamoja ya kujenga tunaleta ukabila.
Niwaambie tu hivi kwa mawazo haya ccm watatuwala mpaka basi. Watakuwa wanabadirishana tu.
 
Yaani saa 10356 ni sawa na siku 431.5 ambayo ni sawa na mwaka 1 na miezi miwili mtambo ufanya kazi bila matengene.Inaumiza sana aisee.

Na wewe unaamini hizo porojo mkuu…

Gari yako usipofanyia service unaliendesha tuu…unapiga ruti Arusha, Mwanza, Kigoma, Mbeya weee unaendesha tu bila kusimama itatokea nini?!…halafu sasa isitokee kwenye mitambo ya Tanesco ilikuwa inamuogopa JPM?!….

Nasema hakuna kitu km hicho…kuna aina nyingi za maintanance ya hio mitambo…achana na watu wanaotafuta kila means kupata wanachotaka…they will do anything to materialize their every wish…anyway basi since hakuna jinsi ya kuwafanya tumwachie Mungu aingilie kati watachomana tu na ukweli tutaujua…Mwenyezi Mungu fundi…ni swala la muda tu…
 
Duuuuh kazi kweli kweli [emoji23] Magu alijua kutaka sifa aiseee sasa ndo hivo mama anateseka
Kitu cha msingi ni kuwa wakati wa magu kulikuwa hakuna kitu kama hicho cha mgao na kuhusu matengenezo mbona magufuli kachukua nchi kutoka kwa kikwete hali ya umeme ilikuwa mbaya siku zote sasa kati ya kikwete na magufuli ni nani aliyekuwa dhaifu ? Pia tukisema mitambo iliburuzwa kufanya kazi bila ya matengenezo hiyo wanataka kutuaminisha kuwa jpm alikuwa anakwenda kujiujumu yeye mwenyewe kwa kuaribu sekta ya umeme tena ukizingatia alikuwa anajenga sgr ya umeme ? Hapo utagundua ni big no ,jpm ndiye aliye liwezesha shirika la umeme tz kupata mapato makubwa kwa mara ya kwanza tena pasipo kuongeza gharama ya umeme kwa miaka yote aliyekuwa ikulu ,ukitazama kwa makini utagundua magufuli alichukua uamuzi wa akili sana kujenga bwawa la umeme wa maji ambao ni nafuu kwa zaidi ya mara tatu ya umeme wa gesi kwa sababu mradi wa gesi tulisha pigwa kimikataba ndiyo maana tunauziwa gesi kwa bei kubwa mara mbili ya iliyostaili tununue
 
Umeme ulikuwa unakatika hata kama sio kama sasa, ila kosa ilikuwa ni kutangaza. Mgao wa umeme ulianza kushika sana kasi wakati wa kampeni za 2020.
Tuambie jpm alichukua nchi ali ya umeme ilikuwaje kipindi ya kikwete magufuli ndiye raisi pekee aliye fanya mambo ya kipekee kwenye sekta ya umeme kuliko maraisi wote na ulibaki mwaka mmoja tu kama asinge fariki tz ingekuwa ni export wa umeme kwa nchi jirani
 
Mjomba hata usihangaike kunijibu this long, kwangu kwanza naangalia credibility ya mtu ndio ulete habari zako za namba atleast nitakuwa na appettite ya kukusoma.

January Makamba simuamini, utaandika sana haya madude yako lakini kwa tabia zake alizorithi toka kwa JK hata kama alikuwa naibu waziri bado hakuondoi ukweli kwamba ana tabia za udokozi na mipango ya pembeni kuusaka pesa.

Na wakati wa JK walikuwa wanatengeneza migao ya uongo ili wapate fursa ya kutupiga ndio maana zikazaliwa Richmond na nyingine, huu ukweli huwezi kuuficha kwa kuandika long article with numbers, kwangu nakuona unajipotezea muda tu, you can may be move mountains but not me.
 
Hahahhaha yani jamaa alikaa akaona bora apike data kuwa machine running hours zilikuwa nyingi kuliko ambazo zimewekwa kama standard before maintanance?

Ina maana kwa kipindi chote hicho cha Magufuli hakukuwahi kuwa na drought?
Namchora tu anavyohangaika kuandika haya "magazeti" yake huku, nani mwenye akili timamu atakaemuelewa eti tu kwa sababu anatumia "namba"?

Suala la umeme halihitaji namba, ni issue simple tu; umeme unawaka au hauwaki? sababu nini mgao? hao wanaosema hivyo wana tabia gani? ni wadokozi, case closed.
 
Jamaa anaamini namba ndio kila kitu, wakati hali halisi field iko hovyo kabisa.
 
Mimi kukufuata wewe hivi hivi siwezi.Mleta uzi kaweka data toka shirikani kwa nini nisiamini?.
 
Jamaa anaamini namba ndio kila kitu, wakati hali halisi field iko hovyo kabisa.
Sio number tu ukimuuliza alete ushahidi wa week na tarehe ndani miezi 8 kama Songas imefanya maintance to justify current power cut sidhani kama anao.
 
Aliongeza MW ngapi kwenye grid ya taifa kama kweli alifanya mambo ya kipekee?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…