Uongozi mbovu ndo unasababisha bidhaa kupanda bei na Kukosa maji na Nishati

Uongozi mbovu ndo unasababisha bidhaa kupanda bei na Kukosa maji na Nishati

MkamaP

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2007
Posts
8,146
Reaction score
3,235
Tatizo la uongozi liliopo(vaccum of power) ndo linasababu bei ya vitu kupanda na nishati pamoja na maji kukosa. Tusingizie eti sijui awamu ya tano sijui blah blah. Tatizo liliopo sahivi na ndo chazo ya yote haya ni uongozi legelege usiosimamia kinachopaswa kusimamiwa.
 
... suluhisho la uongozi mbovu au legelege ni nini Boss? Wanasiasa hususan watawala wamegundua madhaifu mengi yaliyopo kwenye instruments za kusimamia uendeshaji wa nchi hivyo wanayatumia madhaifu hayo vilivyo na hawapendi kabisa kusikia yanaboreshwa! Tafasiri yake ni kwamba viongozi wapo pale kwa faida zao na makundi yao na sio kulisaidia taifa.
 
Toa ushauri nini kifanyike basi mzee

Wasimamie ipasavyo ama serikali iondoshwe iingie nyingine. Watu hawawezi teseka kisa watu wachache wanapendwa sana ama pretext sijui awamu ya tano. Ndiyo maana akawepo hapo ili atatue hayo matatizo, kama matatizo ya awamu iliyopita huwezi tatua, sasa upo hapo kama kiongozi kufanya nini sasa, pisha waaingie wengine wayatatue bila kulalamika.
 
Madaraka yalivyokuwa mazuri ataacha nani kwa hiari?

Aliweza baba wa taifa tu
 
Madaraka yalivyokuwa mazuri ataacha nani kwa hiari?

Aliweza baba wa taifa tu

"Madaraka matamu" ndo kosa la msingi linalosababisha uongozi legelege . Mtu akishindwa kusimamia ipasavyo na akagoma kuachia kuna namna nyingi za kidemokrasia za kumuondosha na kuweka wataosimamia.
 
Kwasisi Wahenga,Utawala mbovu ulianzia kipindi cha Nyerere.
 
Kwasisi Wahenga,utawala mbovu ulianzia kipindi cha Nyerere.
Kilichopita hatuwezi rekebisha kilishapita, tunachoweza kufanya ni ku deal nahiki kilichopo sahivi ili kibadili maisha ya sasa na yajayo.
Vitu haviwezi rocket ndani ya miezi 8 hii mara dufu halafu tukazania kulaumu waliopita. Tatizo liliopo ni sahivi uongozi legelege ndiyo maana vitu vinapanda sahivi na umeme kukosa sahivi na maji kukosa sahivi.
 
"Madaraka matamu" ndo kosa la msingi linalosababisha uongozi legelege . Mtu akishindwa kusimamia ipasavyo na akagoma kuachia kuna namna nyingi za kidemokrasia za kumuondosha na kuweka wataosimamia.
Hiyo demokrasia labda unaiongelea taifa la Ghana siyo bongo
 
Mfumuko wa bei ni mkubwa sana mbaya zaidi bidhaa hazishuki Kuna tatizo kubwa sehemu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukame, tusubiri mvua labda! (Jokes)
====
Nilishaeleza eleza humu kuwa morali ya kudai risiti na kutoa risiti imeshuka sana!! Juzi ndiyo niliiona hata kumbe hata ukidai risiti haina maana tena...! Jamaa alidai risiti baada ya kukataliwa kupunguziwa bei, mwenye duka akasema sawa, hata kama unataka risiti ya bei ya juu zaidi ya ela uliyolipa utapewa, jamaa akasema nipe hiyo. Aisee mwenye duka amkampa kweli risiti iliyokuwa inakaribia marambili ya bei ya bidhaa aliyolipia jamaa!!! Jamaa alipoondoka, muuza duka akawa anajisemea kuwa, huyu pimbi kweli yeye anadhani kudai risiti ni kunikomoa hajui zama zimebadilika siku hizi. Kibiashara sikuelewa kabisa muuzaji alifanyaje hiyo kitu!.
 
ni bora zingepanda kwa awamu, yaani bidhaa zote zinapanda ghafla wala humsikii kiongozi akitoa neno, nadhani hii ndo serikali yenye dharau zaidh kuliko zote zilizopita.
Sasa unataka nini? Utafanya nini, mwenzako kafulila unamwona anavyonenepa? Mashati ya upinzani yote hayamtoshi! Inabidi uwe mpinzani mkubwa kupata kibarua serikalini!
 
Back
Top Bottom