Naomba kuuliza, ni sababu gani ambazo zimesababisha kupanda kwa bei ya vitu mbalimbali hapa Tanzania? (Mfano, vifaa vya ujenzi, mafuta ya kupikia nk)
Pia, naomba kufahamu, kupanda huku kwa bei ya vitu na maisha kuwa magumu ni hapa Tanzania tu au hata nchi nyingine za Kiafrika?
Kwa wale wenye exposure ya kutembelea nchi za Kiafrika hali ikoje huko? (Usitolee mifano ya nchi za Ulaya)
Nahitaji kujua kama huu ugumu wa maisha ni kawaida kwa nchi nyingine za Kiafrika au kuna sehemu Tanzania tumeishakosea, tujiandae kisaikolojia!