KERO Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili shughulikieni kero ya ubovu wa magari ya taasisi

KERO Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili shughulikieni kero ya ubovu wa magari ya taasisi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
197
Reaction score
233
Tunaomba uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kushughulikia kero ya ubovu wa magari ya taasisi.

Shughuli nyingi zimekwama zinazofanyika nje ya hospitali kama kusafirisha sampuli, kufuata mahitaji mbalimbali nje ya hospitali na pia kufanya huduma za ustawi wa jamii.

Kila tukifuatilia kupata usafiri kutoka kwa Afisa Usafirishaji tunaambiwa magari yote ni mabovu.

Tunaomba uongozi usimamie matengenezo ya magari mabovu ili kurahisisha huduma kwa wateja na kuboresha utendaji kazi wa wafanyakazi.

Kuna watu wengi sana wanategemea kupata huduma inayohusisha usafiri wa magari katika Hospitali ya Muhimbili, hivyo kinachoendelea sasa kinawaathiri watu wengi.
 
Back
Top Bottom