Uongozi wa klabu ya Simba SC wamegoma kufanya kikao cha kocha na waandishi wa habari kisa bango lenye nembo ya GSM

Uongozi wa klabu ya Simba SC wamegoma kufanya kikao cha kocha na waandishi wa habari kisa bango lenye nembo ya GSM

Mimi sitaki hata ku comment hapa maana unaweza kushambuliwa kuwa labda shabiki wa team fulani ila ki ukweli katika makuzi yangu nilikuwa mpenzi sana wa Simba ila siku hizi sina ushabiki wa hivyo zaidi ni Liverpool tu...
Hujawahi kuwa mshabiki wa Simba SC hata kwa nukta moja kwa kauli hiyo wewe Utopolo.

Haya ya leo unaona hayana maana, lakini kugomea nembo ya Vodacom na NBC hadi ibadilishwe rangi umeona ni sahihi.

Mikataba ya kificho baina ya TFF na GSM-Yanga bila ushirikishwaji kwa timu nyingine wewe kwako sawa.

Usiandike kwa ushabiki, andika kwa hoja.
 
Ifike kipindi tuache ushabiki na tuangalie maslahi ya timu na timu nyingine. Mimi ni mshabiki wa Simba lakini kwa hili siungi mkono. Tuangalie sheria zinasemaje kuhusu udhamini lakini pia maslahi ya timu yetu. Pia tusijiangalie sisi kwa kuwa tuna udhamini, tuangalie pia vitimu vidogo visivyo na wadhamini na uwezo wa kulipa mishahara Kama Biashara United,Namungo nk. Mabifu ya wahindi/ waarabu tusiyavae.
Watu mnajinasibu kuwa ninyi ni mashabiki wa Simba, kumbe bandia! Umewasikia viongozi walihoji nini? Hizo sheria ndizo walizohoji.
 
Ifike kipindi tuache ushabiki na tuangalie maslahi ya timu na timu nyingine. Mimi ni mshabiki wa Simba lakini kwa hili siungi mkono. Tuangalie sheria zinasemaje kuhusu udhamini lakini pia maslahi ya timu yetu. Pia tusijiangalie sisi kwa kuwa tuna udhamini, tuangalie pia vitimu vidogo visivyo na wadhamini na uwezo wa kulipa mishahara Kama Biashara United,Namungo nk. Mabifu ya wahindi/ waarabu tusiyavae.
Sheria mdhamini mkuu anakaa bega la kuria sheria haitaji mdhamini mwenza anakaa wapi maana bega jengine klabu zina haki ya kuweka wadhamini
 
Safii. Na kesho wakilazimisha kuweka mabango uwanjani, Simba msiingize timu ili Yanga ipewe point 3 za bure.

Kususa kwa zamu. Yanga waliwahi kugomea mabadiliko ya kuanza kwa mechi, Leo wengine wanamgomea mfadhili wa Yanga na TFF

Kumbukeni Simba ndio inayochangamsha hii ligi yenu. Kama vipi ihamishieni Simba kule Champion League kwa kina Tambwe muone mvuto utavyohamia kule.
Fateni utaratibu
Mdhamini ni pesa
Kama Simba wana pesa nao waweke pesa TFF yabga atavaa jezi zao
Pesa inashindana na pesa
 
Hujawahi kuwa mshabiki wa Simba SC hata kwa nukta moja kwa kauli hiyo wewe Utopolo.

Haya ya leo unaona hayana maana, lakini kugomea nembo ya Vodacom na NBC hadi ibadilishwe rangi umeona ni sahihi.

Mikataba ya kificho baina ya TFF na GSM-Yanga bila ushirikishwaji kwa timu nyingine wewe kwako sawa.

Usiandike kwa ushabiki, andika kwa hoja.
Soma comments zangu za nyuma kuhusu upumbavu wa Yanga kugomea rangi za wadhamini huo ulikuwa upumbavu mkubwa na wapumbavu ni wale waliokubali kubadilisha sheria na haya ndio matokeo yake. Nilikuwa mshabiki lakini sina mapenzi na team yoyote. Bahati nzuri sio kwamba siendi uwanjani muda mrefu hata kwenye TV siangalii huwa natizama matokeo tu kwenye simu.
 
Na kesho kabla ya mechi haijaanza tunaanza kukagua uwanja kama matangazo yapo
Yametolewa ,hahahahaaaaa hamna kisingizio tena leta timu hiyo kudadadeki kipigo kiko palepale unaleta janja janja ya kihindi kukwepa fedheha baada ya kuona barua yako ya kuomba kusogeza mchezo mbele kukataliwa na bodi ya ligi ukatafuta sababu nyingine ili ukimbie mechi sasa watu wenye akili kuliko wewe wametoa mabango kitakachotokea leo ni aibu kubwa kwa Simba na itakuwa historia katika soka la Tanzania,Yanga atacheza soka Safi lenye burudani kedekede,ball possession 98 % kwa 2% na kushinda Magoli zaidi ya 3 . Leo uwanjani ni kumshangilia mwanzo mwisho Simba akidharaulika.
 
Back
Top Bottom