GE2025 Upande wa Jamhuri walalamikia taarifa za Upotoshaji kuhusu Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu

GE2025 Upande wa Jamhuri walalamikia taarifa za Upotoshaji kuhusu Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Upande wa Jamhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, umeiomba Mahakama Kuu kupima maneno na taarifa zinazoripotiwa na vyombo vya habari, wakidai baadhi yake ni za upotoshaji na zinavunja hadhi ya Mahakama.

1758530523182.png

Soma > Mahakama Kuu yatupilia mbali pingamizi la Tundu Lissu dhidi ya Hati ya Mashtaka

Hata hivyo, Jaji anayesikiliza shauri hilo ameelekeza kuwa iwapo kuna taarifa za upotoshaji zinazohusu maamuzi ya Mahakama, upande huo unapaswa kutumia masharti ya sheria za habari na kuwasilisha maombi rasmi kwa mujibu wa taratibu za kisheria.

Licha ya malalamiko yao kuhusu upotoshaji, upande wa Jamhuri umepinga maombi ya kuruhusu kesi hiyo kuoneshwa moja kwa moja (LIVE) kupitia vyombo vya habari, jambo ambalo wadau wa haki na wafuasi wa Lissu wamelitafsiri kama kitendo cha kutaka mwenendo wa kesi uendelee kufanyika kwa usiri.

Screenshot 2025-09-22 114100.png
 
Wapumbavu wakubwa hao, kama kuna upotoshaji kwanini hawataki kesi iruke moja kwa moja YouTube kila mtu aone na kuchuja na kuona kama kuna upotoshaji?
 
..wapotoshaji watafungwa mikono ikiwa kesi itarushwa LIVE.
 
Back
Top Bottom