Upanga, Dar: Yaliyojiri kutoka Ukumbi wa JWTZ, Mkutano na Waandishi wa Habari

Upanga, Dar: Yaliyojiri kutoka Ukumbi wa JWTZ, Mkutano na Waandishi wa Habari

Waandishi wote wa Tanzania Pamoja na vyombo vyote vya Habari vya Tanzania tunalo jukumu kubwa la kulinda Amani ya nchi yetu, kamwe tusikubali kurubuniwa au kuchochewa tukavuruga amani ya Nchi yetu kwa kalamu zetu au vyombo vyetu vya habari.
Nchi yetu Kwanza.
 
Salaam Wakuu,

Leo Jeshi la Wananchi Tanzania, linafanya Mkutano na Waandishi wa habari. Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) kutoa Tamko Maalumu 30 Novemba, 2021

Nipo Nimefika kwenye Ukumbi huu kuwajuza kila kitakachojiri.

=====

UPDATES: 1022hrs

======
View attachment 2027879
Waandishi wameshafika eneo la tukio

1034 hrs: Gervas Ilonda
View attachment 2027914
Wengi tumekutana hapa kujua ni nini hasa tunataka kuzungumza. Siji kutoa tamko bali nimekuja kutoa ufafanuzi wa mambo ambayo jeshi limeona yanaendelea. Hatuwezi kuyafumbia macho.

Naomba nitoe ufafanuzi kwa Vijana wanaojiandikisha kujiunga na Jeshi.

Hapo nyuma Viongozi wamekuwa wakitembelea Miradi ya Kimkakati. Wakiwa kule, wamekuwa wakilizishwa na Vija wa kujenga taifa wanavyojituma na kuwa Wazalendo.

Viongozi baada ya kuona uzalendo na umahili wa hali ya Juu wamekuwa wakiwaahidi kwamba nafasi za jeshi zikitka watapata.

Hivi karibu zimetoka nafasi kwa vijana wa Makambi ya JKT sio wote. Zimetoka chache lakini si haba.

Nimelazimika kuongea na vyombo vya habari ili tufahamishe umma kwamba kwa sasa kumeanza kuibuka kwa vitendo cya baadhi ya watu kutumia hizi nafasi za hawa vijana kujinufaisha. Vitendo vya Rushwa na Udanganyifu katika nafasi hizi. Matapeli hao wamekwenda mbali zaidi kwa kusingizia viongozi kwamba wametumwa wamewe hela ili vijana waandikishwe. Wanadai Mkuu wa majeshi ndo amewatuma. Jambo hilo sio kweli. Hatiwezi kulifumbia macho kuona viongozi wetu wanasumbuliwa. Mbaya zaidi wanachukua nyumba za kulala wageni wanaingiza vijana na kuwaambia subiri tunaenda kuwatafutia kazi, matokeo yake wanaanza kuwafuata wakuu wa Majeshi kudai nafasi zao. Kupitia kwenu nawaomba muwapuuze na msidanganyike kutoa fesha kwa nafasi za kuingia jeshini.

Natoa rai kwa wanaofanya Vitendo hivyo kwamba sio vya busara wala kiungwana. Waache mara moja.

Baadhi ya Wazazi wameanza kuwafuata viongozi waliopo Jishini kwenye ngazi mbalimbali kuwaomba wawasaidie kuwaingiza vijana wao Jeshini. Jeshi la Tanzania, lina taratibu na kanuni za kuingiza Vijana Jeshini sio kwa fedha wala kuoneana huruma.

Kijana anatakiwa awe

1). Raia wa Tanzania wa kuzaliwa

2). Umri awe na miaka 18 hadi 28

3) Awe na afya njema ya mwili na akili

4). Lazima awe mwenye tabia njema na nidhamu nzuri, asiwe amepatikana na hatia ya kijinai

5) Awe na cheti halisi cha kuzaliwa, vya shule na chuo.

Kwa Upande wa Madaktari

Awe amemaliza mafunzo kwa vitendo na pamoja na kusaidiwa na bodi ya madaktari.

Hizi ndizo sifa zitatumika kuwachuja vijana Walioandikishwa kuingia Jeshi la wananchi wa Tanzania. Sio wote walioandikishwa watapita.
Duh kwahio tayari Press imeisha?
 
haya mambo si yalipaswa yasemwe na wizara ya ulinzi na si jeshi lenyewe? huko nyuma yalikuwa yanasemwa na waziri wa ulinzi au ye yote kwa niaba yake, huyu mabeyo ameamua kufanya hivi kwa kuwa rais na waziri wa ulinzi ni wanawake?
 
Waandishi wote wa Tanzania Pamoja na vyombo vyote vya Habari vya Tanzania tunalo jukumu kubwa la kulinda Amani ya nchi yetu, kamwe tusikubali kurubuniwa au kuchochewa tukavuruga amani ya Nchi yetu kwa kalamu zetu au vyombo vyetu vya habari.
Nchi yetu Kwanza.
Wewe ndio hutaki kuwa "Mwaipaya" hahahaha Divide and rule!
 
haya mambo si yalipaswa yasemwe na wizara ya ulinzi na is jeshi lenyewe? huko nyuma yalikuwa yanasemwa na waziri wa ulinzi au ye yote kwa niaba yake, huyu mabeyo ameamua kufanya hivi kwa kuwa rais na waziri wa ulinzi ni wanawake?
Mwanamke hasipowezeshwa HAWEZI

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Kwahiyo umeanza kuhukumu kabla ya kusikia kitakachoongelewa??
Tabia huzaa mazoea.Tabia ya serikali hii ya CCM inajulikana.Hata wewe ukiibiwa ndani kwako cha kwanza utaanza kumuhisi kibaka ambae anaishi karibu na nyumba yako.
 
What......!!!!!!!

Politicization of non political entities
 
Back
Top Bottom