Mama Mwana
JF-Expert Member
- Jun 6, 2023
- 2,435
- 7,784
Kupanga uzazi ni kitendo cha mtu kuamua kuwa na idadi maalum ya watoto kwa ustawi wa familia yake. Wapo wanaotumia njia hizi wakiwa pia hawajabahatika kua na watoto.
Kuna aina kuu mbili za njia mbali mbali za kupanga uzazi ambazo ni njia za asili na zisizo za asili.
Njia za asili ni njia ambazo hazitoi aina yoyote ya kichocheo kwa mtumiaji husika kwa maana kwamba mhusika akitumia njia hio anakua hapati maudhi yoyote yale yatokanayo na njia hio. Njia hii n pamoja na:-
KUTUMIA CONDOM
Njia hii inaweza kutumika na jinsia zote mbili kwamba ziko condom jinsia ya kike na ya kiume, njia hii ni salama kwani mbegu zote huishia katika mfuko maalum ambao hauruhusu mbegu hizo kupitiliza na kuingie kwenye uke, ukiacha na kuzuia mimba njia hii huzuia maambukizi ya magonjwa kama vile HIV/AIDS na mengineyo yatokanayo na ngono isiyo salama.
KUMWAGA NJE
Njia hii mwanaume atatakiwa kujizuia kutoruhusu mbegu kumwagikia kwenye uke badala yake atatakiwa kuchomoa uume wake na kumwagia popote anakoona ni salama na sio kwenye uke, njia hii ikitumika ipasavyo huzuia mimba lakini ni ngumu mno kwan mtu anatakiwa kua makini kuchomoa kabla na wataalam wa afya husema pia yale maji maji yanayotoka mwanzo ikiwa wahusika hawajaingiliana hua na kiwango cha mbegu ambacho ni rahisi mimba ikatungwa
KUTUMIA KALENDA
hii ni njia ambayo wahusika watatakiwa kujua ni lini yai litakua karibu kurutubishwa kuzijua siku hatari za kushika mimba kwa kuhesabu mzunguko husika wa mwanamke,
kufunga mirija inayotumika kupitisha aidha yai kwa mwanamke au mbegu kwa mwanaume njia hii ni hutumika baada ya kuona mtu amepata idadi ya watoto awatakao na hana mpango wa kutumia njia zingine
Njia zisizo za asili ni njia ambazo hutoa kichocheo maalum ili kuzuia utungwaji wa mimba kufanyika, njia hii hua na maudhi madogo madogo kwa watumiaji japo sio wote huona au kupata maudhi hayo na njii hizi ni kama zifutazo:-
KIPANDIKIZI (KIJITI)
Hii ni aina flani ya kijiti cha plastic saizi ya njiti ya kiberiti ambacho huwekwa kwa mwanamke sana sana mkono wake wa kushoto. Kipo kipandikizi au kijiti cha miaka mitano au mitatu hutegemea na mtu anayechagua njia hii atajikinga kwa muda gan kabla ya kuamua kuongeza familia.
Njia hii inatoa kichocheo ambacho kinampelekea mtumiaj kua na maudhi madogo madogo kama kuongezeka hamu ya kula, kutokua na hamu ya kufanya tendo la ndoa, kupata hedhi zisizo na mpangilio maudhi haya sio kila mwanamke anakutana nayo unaweza ukatumia vizur mwanzo ukakitoa ukaja kukitumia baadae ukayapata na unaweza udione chochote katika maudhi haya ukaingia hedhi kwa mpangilio wako mpaka kitakapokwisha muda wake.
KITANZI
Njia hii huwekwa katika mji wa mimba kwa mwanamke, hii pia ina madini yanayosaidia kuzuia mimba kutungwa, nayo pia hua na muda maalum kuanzia miaka mitano had kumi (niko tayaro kurekebishwa) asilimia kubwa ya watumiaji wanjia hii husema hupata sana fangasi kitu ambacho wataalam wa afya husisitiza unapoamua kutumia njia hii usiwe ni mwingi wa kubadili wanaume
SINDANO
Njia hii mwanamke huchomwa sindano ambayo atatakiwa aichome kila baada ya miezi mitatu na hua na vichocheo ambavyo wataalamu wa afya hushauri kama hauna mtoto kabisa ni vyema ukachagua njia zingine sababu ina mtindo wa kuchelewesha sana kutungisha mimba ikiwa mtu atataka kubeba tena baada ya muda wake kuisha
Maendeleo huanzia kwenye ngazi ya familia hadi nchi, kwamba mtu unapokuwa na idadi stahiki ya watoto au mtu akiamua kutobeba ujauzito kwanza mpaka akamilishe jambo flani inakusaidia kuweza kumudu gharama za malezi au zamtu binafsi kwa sababu:-
1. Utaweza kuhudumia familia au maisha yako binafsi pasipo kujitwisha mzigo ambao n mzito kwako. Ninamaanisha kwamba kwa sasa hivi gaharama za maisha zimepanda, unapokua na idadi kubwa ya watoto au kuamua kuingia kwenye malezi bila kutarajia utashindwa kutimiza malengo husika, sana sana ukibahatika ni chakula bado kunakusomesha, kuumwa na mahitaji mengine ya msingi. Na kama nchi itaweza kuleta maendeleo kuanzia kitaifa na wananchi wake kiujumla ni sawa na kusema kuwa tutakua kama nchi tunaenda sawa sio wengine wana hali nzuri wengine bado wanajikongoja kufikia maendeleo.
2. Ili kuifikia Tanzania tuitakayo ni lazima kama nchi serikali itoe elimu kwa wananchi katika vituo vya afya. Itoe elimu bila kuficha madhara na faida na itoe hizi huduma zote ziwe zinaptikana kias hata mtu wa hali ya chini aweze kuipata, hapa ninamaanisha kwa sasa hivi vituo vyetu vya afya utaambiwa kinachopatikana ni kijiti tu zingine nenda duka la dawa mtumishi wa afya amemaliza. Serikali iweke mkazo huko na iwezeshe hizi njia zote zipatikane huko tena bure sio kwa njia ya magendo
3. Somo la kupanga uzazi liwe ni somo maalumu kuanzia msingi, kwani asilimia kubwa ya wanaoathirika ni watoto wetu walio balehe bila kupatiwa elimu hii, hii ni kutokana na unakuta mtoto anatokea familia duni, anaishia kurubuniwa ajikwamue na dhiki mwishoe anarudi na mimba au Ukimwi. Ikiwezekana somo hili lifundishwe kwa wanafunzi wa jindia zote bila kubagua hii itasiadia hata huko mbele mtu atajua anajipangaje kwa kua tayar elimu husika anayo.
4. Wazazi wawe karibu na watoto wao hasa baada ya kuona mabadiliko ya kimienendo ya watoto wao. Mzazi asiweke ukali mbele kwani watoto hutumia mbinu mbadala wakiona hawapti kile wanachokitaman kukijaribu mwisho wasiku mtoto anafunguwa ndani na bado analeta mimba zisitarajiwa kumbe mzazi angekua karibu na mwanae angeweza kuepuka kikombe hicho.
5.Kupanga uzazi kusiwe ni kwa mwanamke pekee bali hata wanaume wawe bega kwa bega na wandani wao, mwanaume aone anafanya hivi kwa sababu ananipunguzia majukum kama nguzo ya familia niweze kupmbama kwa idadi hii tuliyokua nayo na sio kumuacha au kumtelekeza kwa sababu hio,
Serikali yetu inapambana usiku na mchana kutafuta maendeleo kwetu, ili tuweze kwenda mbio hizi pamoja bila kua na nafasi baina yetu tupange uzazi kwa ajili yamaendeleo yetu wenyewe kwani unapoamua kupanga uzazi kwanza utaweza kulea bila kujiumiza,utaweza kujiwekeza kwa nafasi,

Upvote
0