UPDATE: Watumishi waliomwagiana Maji ya Dripu wakisherehekea 'Birthday' wasimamishwa Kazi

Kuna mambo mengi sana ya msingi serikali ya kuyatolea ufafanuzi na si hiyo birthday.

-Umeme kila siku unakatika
-Barabara mbovu/hazipitika ,wanafunzi wanavuka kwa kuogelea kwenda shule
-Hospital rushwa kibao
-Matumizi ya anasa serikalini.
-Upigaji /20% kibao.
-Treni ya Mwendo kasi 160km/hr sawa na speed ya Hitcher wakati Mwendo kasi Dalali Kitenge katuonyesha ni 318km/hr.
Eh walitumia maelfu ya drip kujimwagia kwani
Mkuu drip moja bei gani kwani

Ova
 
View attachment 2832151
=============

View attachment 2832152
Serikali iemanza kufanya uchunguzi kuhusu video inayosambaa mtandoni ikiwaonyesha watoa huduma za afya wakisherehekea siku ya kuzaliwa kwa kumwagiana majitiba maarufu ‘dripu’.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili, Desemba 3, 2023 Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu amesema bado video hizo hazina uhalisia na eneo linalotajwa, hivyo wanashirikiana na waganga wakuu wa maeneo husika kujiridhisha.

“Nimeiona asubuhi hii tunafuatilia, inaonekana kama hicho kituo kilichoandikwa pengine si chenyewe, lakini hatujapata uhakika vizuri,” amesema.'

Profesa Nagu amesema wanafuatilia kupitia Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Geita, lakini bado hawana uhahika kama ni kituo cha Serikali au cha binafsi.

“Tumeona picha za watu, lakini tunafuatilia kuona ni kituo gani, inawezekana pia si jina la kituo kilichoandikwa, tukishafuatilia tutatoa majibu mpaka tupate ukweli wa tukio lenyewe,” amesema Profesa Nagu.

Katika video hiyo iliyokuwa na maelezo kuwa ni watumishi wa afya katika kituo cha afya Nyankumbu, walionekana wanatumia maji ya kutibia wagonjwa (dripu) kwa sherehe yao ya kuzaliwa.

Hata hivyo, maoni ya watu mbalimbali katika mtandao wa kijamii wa Instagram yalijikita kwa Wizara ya Afya kutolea ufafanuzi jambo hilo, wakitaka ichukue hatua na kama kuna uvunjifu wa maadili ya utumishi wa afya, uwajibikaji uwepo.

“Watanzania wanakosa dawa na vifaa tiba huko kwenye vituo vya afya vijijini, lakini wengine wanafanyia birthday?” amehoji Amos James.

“Unatumia mali ya Serikali iliyogharimu mabilioni ambayo kule Tanga mama mjamzito alipoteza uhai kwa kukosa tu pesa ya huduma ya upasuaji, huduma ambayo huenda angeipata bila kulipa chochote,” amesema Abdul Salaam.

Fahamu kuhusu dripu

Mfamasia na Mkufunzi wa Shule ya Famasia wa Chuo Kikuu Muhimbili (Muhas), David Myemba amesema majitiba yanayotumika kumwekea mgonjwa kupitia mishipa ya damu kawaida nusu lita huuzwa Sh2,000 japokuwa inategemea na ujazo husika kama ni lita moja ni zaidi ya hapo.

Alipoulizwa iwapo kuna madhara yoyote ambayo mtu anaweza kuyapata akitumia ndivyo sivyo, Mnyemba amesema hakuna madhara, isipokuwa kama mtu atakunywa mengi anaweza kuharisha.

“Ukinywa mengi unaweza kuharisha, lakini kuna mengine hayana madhara yoyote, ukinywa yenye sukari nyingi inapandisha sukari ghafla na kuna mengine yana madini mengi akitumia anaweza kupata madhara.

“Kwa kunywa hayana madhara, lakini hayatakuwa na faida ya moja kwa moja. Majitiba yanatakiwa kutumika kwa kuingiza moja kwa moja kweye mishipa ya damu, kwani hata ukinywa hayakati kiu kirahisi kama maji ya kawaida,” amesema Mnyemba.

MWANANCHI
Inawezekana walijaza maji kwenye chupa zilizokwisha tumika kwa sababu zinabonyezeka hivyo kurusha maji.
 
mbona mabro mnafika mbali sana[emoji23][emoji23]

tupate umri wa hao wahudumu kwanza.

Sent from my Redmi Note 8 using JamiiForums mobile app
Sisi tuliozaliwa miaka ya 70's na 80's hatukuwa na birthday utotoni mwetu haya maisha ya kusherehekea birthday tumeanza kuyaona miaka ya 90's....

Kipindi hicho MASHOGA walikuwa wachache tofauti na miaka hii ya kwenu
 
Nimeambiwa walichukua chupa tupu za drip zilizotumika wakajaza maji ya kawaida ili wazitumie kurusha maji.
Hakuna kesi.
 
Sisi tuliozaliwa miaka ya 70's na 80's hatukuwa na birthday utotoni mwetu haya maisha ya kusherehekea birthday tumeanza kuyaona miaka ya 90's....

Kipindi hicho MASHOGA walikuwa wachache tofauti na miaka hii ya kwenu
hawa ni vijana wa 2000,ndio hata hutuomba tuwapost kwenye status zetu.

Sent from my Redmi Note 8 using JamiiForums mobile app
 
GEITA: Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Sakamu amewasimamisha kazi Watumishi wa Afya walioonekana kwenye Video iliyosambaa Mtandaoni wakimwagiana Maji ya Dripu kwa lengo la Kusherehekea Siku ya Kuzaliwa ya Mmoja wao

Pamoja na Mkurugenzi kuomba radhi kwa kitendo hicho, amesema Hospitali imechukua hatua hizo ili kupisha uchunguzi kwaajili ya kuchukua hatua zaidi za Kiutumishi kwa kuzingatia Kanuni na Taratibu kulingana na Mabaraza ya Kitaaluma

Soma UPDATE: Watumishi waliomwagiana Maji ya Dripu wakisherehekea 'Birthday' wasimamishwa Kazi

#JamiiForums #Governance #JFUwajibikaji23 #Accountability #Afya
FB_IMG_1701621578049.jpg
 
Serikali yetu bhn, ujinga ujinga mwingi sana. Mara sjui mkuu wa shule kasimamishwa kisa honey ya zuchu mara sjui usenge gani, hamna kazi za kufanya..??
 
Dah .
Pole yao.
Mwezi huu unawekwa pembeni!? Unaweza chukiwa na ukoo mzima. Mwezi wa ada!?😭😭
 
Back
Top Bottom