UPDATE: Watumishi waliomwagiana Maji ya Dripu wakisherehekea 'Birthday' wasimamishwa Kazi

UPDATE: Watumishi waliomwagiana Maji ya Dripu wakisherehekea 'Birthday' wasimamishwa Kazi

Issue ndogo lakin8 itafanywa habari kuuuubwa....

Wakati zile habari kubwa za ukweli ukweli huwa zinapotezewa na wenye mamlaka...
 
Kwani wao Serikali inatumia gharama kiasi gani kununua V8 na kugawana?
 
Wamejaza maji kawaida kwenye hizo drip nalo ni kosa ???
Ndio maana wamesimamishwa kazi, ili kupisha uchunguzi.
Uchunguzi utatoa majibu juu ya hoja zote hizi.
Lakini Swali la msingi linabaki palepale kwamba, Je,. maadili ya kazi yao yanasemaje kuhusiana na hicho kitendo walichotenda??Hata kama chupa hizo (dripu) zilijazwa maji ya kawaida??
Is that action Ethical or Unethical according to their Professional Codes of Conduct???
 
Mimi sijaelewa, yn wamesimamishwa kazi halafu hapo hapo hawajui hilo tukio limetokea wapi.?
 
Nilijua tu hawa watakuwa wanawake kwani wapenda sana kufanya vijisherehe uchwara....hawataki kupitwa na sherehe yoyote. Tatizo ni hawo wanaume wsliojichomeka humo kwenye sherehe. Hawa wanaume yafaa wachukuliwe hatua maradufu zaidi.
Hao wanaume wapigwe nyundo ya maana

Mwanaume kamili unasherekea birthday ya Kazi gani?
 
Hao ni wajinga...wanafanyaje birthday ofisini na muda wa kazi,watanzania tunaonekana wavivu na wazembe kazini kwa mambo kama hawa...

Kuna baadhi ya nchi hawaruhusu kabsa matumizi ya simu ofisini...sembuse hili la kufanya part ofisini tena kituo cha afya..

Ningekuwa mimi mkuu wa kituo hcho ningewafukuza kazi mara tatu....shenziii hao ukute mtu na. Ka boy kake
 
Hii serikali inapenda kupoteza muda. Kuna kipi cha kuwafukuza kazi hapo ?
Kumwagiana maji ? Ukute hata chupa moja ya maji haijaisha
Kuimba ?
Kutumia muda wa serikali kuimbiana ?
Kama ni muda aa serikali wana uhakila ni muda wa kazi ? Pengine ni jioni.
Karne yaTIKTOK serikali iache mihemko,
Viongozi wa serikali fanyieni kazi tuhuma za CAG ambazo ni za kisayansi na kuachana na habari za udaku za tiktok, yaani kiongozi unafanyia kazi habari ya tiktok halafu ya CAG unaipotezea, mzima wewe!
Utafanyia ngapi ?
Umekosa wasimamizi pale kituoni.
 
Kuna mambo mengi sana ya msingi serikali ya kuyatolea ufafanuzi na si hiyo birthday.

-Umeme kila siku unakatika
-Barabara mbovu/hazipitika ,wanafunzi wanavuka kwa kuogelea kwenda shule
-Hospital rushwa kibao
-Matumizi ya anasa serikalini.
-Upigaji /20% kibao.
-Treni ya Mwendo kasi 160km/hr sawa na speed ya Hitcher wakati Mwendo kasi Dalali Kitenge katuonyesha ni 318km/hr.
Wanapenda habari kama hizi kufunika udhaifu wao. Mabos wengi ni very weak intellectually and ethically.
CAG report inadhihirisha kila mwaka.
Kwa savabu nchi yetu inawafuata upepo wasio reason out watawaunga mkono.
Upuuzi puuzi unafanywa kuwa habari za muhimu.
Kwa mtu alie iva kiuongozi sio kila jambo ni la ku react. Mengine ni ya kupotezea, hilo tukio halileti hasara yoyote kwenye hio taasisi zaidi ni kupewa onyo la kinidhamu.
 
Kinachonishangaza ukiwasikiliza wenye mamlaka wanapigia kelele hao watumishi kupiga video na kusambaza ila hawalaumiwi kwa kumwagiana maji ya drip
 
Mnaosema wametumia hizo chupa kujaza maji, mnaelewa kweli mnachosema? Kifaa tiba kikiisha matumizi yake kinatakiwa kufanywaje?

Hata mimi ambaye sio professional naelewa.
 
Hivi hawawezi kujitetea kwamba ni kweli chupa ni ile inayotumika kuwekwa drip na kwamba walichukua chupa tupu iliyokwisha tumika wakaweka maji ya kawaida ya bomba na wakati wa shamrashamra za birthday wakawa wametumia chupa hiyo yenye maji ya bomba kumwagiana? Nani anaweza kuthibitisha kuwa chupa ilikuwa na drip na siyo maji ya kawaida? Na je, kama hiyo drip ya 2,000/= walinunua kwa pesa yao wenyewe bado ni kosa kubwa la kuwafanya wafukuzishwe kazi au ilifaa wapewe barua ya onyo tu? Wanyonge wananyongwa kweli na hawana watetezi wakati kuna kundi kubwa la watu hasa viongozi wa serikali na siasa wanaokiuka maadili na kuangamiza taifa kila siku lakini wanadunda tu kazini.
 
Mimi naona hili jambo halina mashiko kuliundia tume au kumsimamisha mtu ni kupoteza nguvu kazi, nashukuru kwanza hili jambo limethibitishwa kutokea kwenye kituo binafsi cha Afya, pili hayo maji watu wanayoyatolea macho hayana thamani yeyote mpaka yakiwa yanawekwa kwa mgonjwa, drip moja kwa bei ya jumla hailingani hata na maji ya Uhai (500mls ni kati ya 250tsh mpaka 300tsh)

Tatu hakuna mwenye ushahidi kwamba yale maji yalikuwa ya drip maana Kuna uwezekano wa wao kutumia kopo lililotumika wakajaza maji na kumwagiana

Kwa hali hiyo hakuna uwezekano mkubwa wa kuwabana maana kumwagiana maji kutumia kopo la drip is not criminal offense wala sio offense ya kitaaluma zaidi ya kuwa na hisia hasi kwa jamii.

Ushauri Serikali iliache hili kwenye mikono ya wamiliki wa hospital husika wawajibishe kulingana na hasara waliopata kama itathibitika!
 
Kama itabqinika ni kweli basi nashauri watu hao wafukuzwe kazi pia wafunguliwe mashitaka kwa mujibu wa sheria.
Hakuna Sheria inayosema ukimwagiana maji ya drip ya 250tsh utafungwa au kufukuzwa kazi, nashauri Serikali ijitenge na shauri hili, maana litawapunguzia heshima, watawasimamishwa au kuwafukuzwa kazi mwishowe watafungua kesi na kushinda na watadai fidia, kwanza hakuna ushahidi wa yale maji ndani yalikuwa ya drip! Sawa na wasanii wanaoigiza wanakunywa pombe kumbe hajawahi kuonja na ndani ya chupa ameweka juice!
 
Mwenye namba ya mwenye suruali nyeupe nataka nimfanyie birthday party hadi mjinyonge
 
Back
Top Bottom