UPDATE: Watumishi waliomwagiana Maji ya Dripu wakisherehekea 'Birthday' wasimamishwa Kazi

Nilijua tu hawa watakuwa wanawake kwani wapenda sana kufanya vijisherehe uchwara....hawataki kupitwa na sherehe yoyote. Tatizo ni hawo wanaume wsliojichomeka humo kwenye sherehe. Hawa wanaume yafaa wachukuliwe hatua maradufu zaidi.
 
Kwanza kabisa siyo kama nawatetea kwa picha iliyopo hapo juu, ila twende mbele turudi nyuma. Tuna uhakika gani kama hiyo ni drip au walitumia chupa ambayo ilishatumika kujaza maji? Tusiwe wepesi sana wa kutamka kosa bila ya kuwepo uthibitisho. Miaka ya hivi karibuni watumishi wa umma wamekuwa wakichambuliwa kuwa na makosa bila kupata ushahidi wa kutosha. Unakuta mtumishi katenda kazi yake inavyotakiwa lakini unakuja sikia ooh afukuzwe,asimamishe, ashitakiwe bila kuwepo uthibitisho wa kosa. Nimekuwa nikifatilia sana nisikiapo watumishi wa umma lakini asilimia kubwa huwa tunawaonea sana kuanza sema wafukuzwe bila kuwepo ushahidi wa kosa. Sasa kama hapa ingependeza ufanyike ushahidi ili ijulikane ni kweli wametenda kosa ndiyo hatua stahiki zichukuliwe.. Kuna mtumishi mmoja iliwahi tokea kaletewa pesa na ndugu yake akamlipie ada kama kawa kuna mtu akapiga picha na kusambaza kuwa anapokea rushwa cha ajabu pesa jamaa alipokea akawa anahesabu bila kificho. Fikiria alivyomchafua mtu yule.Hawa ni madaktari siamini sana kama kwa taaluma yao tena wakuijirekodi kuwa wametumia drip kufanya hivi tuache uchunguzi uthibitishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…