1. Wachaga - Kama kawaida yao sio watu wa kujisifia iwe ni biashara, maendeleo ya vijini kwao, n.k. Kiufupi hawa suala la elimu wapo Mbali tangu enzi za ukoloni, Mkoa wa Kilimanjaro ni mdogo ila ndio unaongoza kwa shule nyingi hasa maeneo ya uchagani, Kitu cha ziada ambacho wengi hawakijui ni kwamba wana mwamko wa shule za kimataifa na hata miji wanayoishi ya Moshi na Arusha kuna shule hizi nyingi kama St Constatine, Braeburn, INternational school of Moshi, Kennedy house, n.k. Kwenye shule hizi watoto utaowakuta kutoka Tz ni wachache ila majority huwa ni wachaga kwasababu ya mwamko, sio suala la mzazi kuwa na pesa tu, na hata zile nafasi za udhamini wanazijaza wao, Shule hizi ni tofauti kabisa na hizi za Necta, huku ukisoma kuna guarantee kubwa kusoma vyuo bora duniani, Walimu bora wa kimataifa, connections nzito, n.k.
2. Wahaya - Yes, Ni nani asiewajua watu hawa waliowekewa kizuizi na Nyerere kwa alama za kufaulu darasa la saba ? Hawa watu wanaipenda shule jamani, Shida ni kwamba kuna changamoto za kiuchumi mkoani Kagera, wapo wengi wanaotamanigi kuendelea na shule na uwezo upo ila inawalazimu waendelee na maisha mengine,
3. Wanyakyusa - Ughonile, Nimeishi nao so nawajua vizuri hawa kina Mwakyusa, Mwakatobe, Mwakyembe, Bukuku, n.k., wazazi wa kinyakyusa hasa wamama wanaasa sana watoto wasome, wapo tayari kujinyima kwa lolote mtoto asome shule nzuri, Nakumbuka nikiwa Mbeya mtu anaweza kuresit form 4 hata mara 3 kutafuta credit, hawana jambo dogo kwenye elimu !! kuhusu uwezo darasani wanao wa kawaida ila wapo wachache nishawai kutana nao ni ma genius, Kwa sasa Mbeya ndio mkoa inaoongoza kwa vyuo ukiitoa Dsm, Kuba shule za kiingereza 4 za serikali za msingi, Shule za Sekondari zipo nyingi
4. Wasukuma - Wingi wao kuwa 16% katika population ya nchi ndio unawabeba zaidi waweze kuonekana ila kwa asilimia ya wasomi ndani yao bado ni wachache sana walioelimika, Tatizo la kuwa chini kielimu ni kwamba huko mikoa yao walipojazana kama Simiyu, Geita, Shinyanga, n.k shule ni hazipewi kipaumbele, wasomi wengi hutokaa Mwanza,
5. Wakerewe / Wajita - (Hapa nitaomba mnisahishe hivi wakerewe na wajita ni kabila moja ? ) Anyway nachojua Wakerewe wapo visiwa vya ukerewe, Wajita wapo ukerewe na mkoa wa Mara, Ukerewe ndio wilaya inayoongoza kwa phd, Jimbo kama musoma vijijini huko ni kawaida wagombea wote kuwakuta wana phd, hawapo namba moja kwasababu wanaosoma wanafika mbali sana kielimu ila wanaopata access ya elimu bado wachache.
Bonus....
Wapare, Wakurya, wamasai wa Meru, Wamatengo wa Ruvuma, n.k. huku changamoto ni access ya elimu ila angalau nao si haba.