1. Wachaga - Kama kawaida yao sio watu wa kujisifia iwe ni biashara, maendeleo ya vijini kwao, n.k. Kiufupi hawa suala la elimu wapo Mbali tangu enzi za ukoloni, Mkoa wa Kilimanjaro ni mdogo ila ndio unaongoza kwa shule nyingi hasa maeneo ya uchagani, Kitu cha ziada ambacho wengi hawakijui ni kwamba wana mwamko wa shule za kimataifa na hata miji wanayoishi ya Moshi na Arusha kuna shule hizi nyingi kama St Constatine, Braeburn, INternational school of Moshi, Kennedy house, n.k. Kwenye shule hizi watoto utaowakuta kutoka Tz ni wachache ila majority huwa ni wachaga, sio suala la mzazi kuwa na pesa pekee bali na mwamko wa kuwapa watoto elimu ya kimataifa, na hata zile nafasi za udhamini watanzania kusoma bure huwa ni watoto wa kichaga. Ikumbukwe shule hizi ni tofauti kabisa na hizi za Necta, huku ukisoma kuna guarantee kubwa kusoma vyuo bora duniani, Luhgha za wazungu walimu ni wazungu, connections nzito za watoto wa wazito, n.k.
2. Wahaya - Yes, Ni nani asiewajua watu hawa waliowekewa kizuizi na Nyerere kwa alama za kufaulu darasa la saba ? Hawa watu wanaipenda shule jamani, Shida ni kwamba kuna changamoto za kiuchumi mkoani Kagera, wapo wengi wanaotamanigi kuendelea na shule na uwezo upo ila inawalazimu waendelee na maisha mengine,
3. Wanyakyusa - Ughonile, Nimeishi nao so nawajua vizuri hawa kina Mwakyusa, Mwakatobe, Mwakyembe, Bukuku, n.k., wazazi wa kinyakyusa hasa wamama wanaasa sana watoto wasome, wapo tayari kujinyima kwa lolote mtoto asome shule nzuri, Nakumbuka nikiwa Mbeya mtu anaweza kuresit form 4 hata mara 3 kutafuta credit, hawana jambo dogo kwenye elimu !! kuhusu uwezo darasani wanao wa kawaida ila wapo wachache nishawai kutana nao ni ma genius, Kwa sasa Mbeya ndio mkoa inaoongoza kwa vyuo ukiitoa Dsm, Kuba shule za kiingereza 4 za serikali za msingi, Shule za Sekondari zipo nyingi
4. Wasukuma - wasukuma wapo wengi sana hii nchi ila tatizo maeneo yao mengi hawaipi elimu kipaumbele, mikoa waliyojazana wasukuma kama Simiyu, Geita, Shinyanga, n.k elimu haipewi uzito na shule ni chache, Mwanza ndio inawabeba.... Laiti wasukuma wangejiongeza kielimu lingekuwa ni tishio kubwa sana hapa nchini maana katika kila watanzania sita kuna msukuma moja, Huenda mkoloni hakupeleka elimu usukumani alishaona watadominate sana.
5. Wakerewe / Wajita - (Hapa nitaomba mnisahishe hivi wakerewe na wajita ni kabila moja ? ) Anyway nachojua Wakerewe wapo visiwa vya ukerewe, Wajita wapo ukerewe na mkoa wa Mara, Ukerewe ipo mkoa wa Mwanza lakini kijiografia ipo mkoa wa Mara, Ukerewe inaongoza kwa utitiri wa phd Tanzania nzima, upande wa mkoa wa Mara Jimbo kama musoma vijijini huko ni kawaida wagombea wote kuwakuta wana phd, Kundi hili sijaliweka namba moja kwasababu wakazi wa huko wengi hawana access nzuri ya elimu ila wachache wanaoipata ndio wanafikia mpaka phd ila ukihessabu walioweza kufika hata degree bado wachache,
Bonus....
Wapare, Wakurya, wamasai wa Meru, Wamatengo wa Ruvuma, n.k. huku changamoto ni access ya elimu ila angalau nao si haba.