UPDATES: Madhara ya mvua iliyonyesha jijini Dar - Desemba 17, 2019

Mbezi-Kimara na viunga vyake mvua ni kubwa mno, mno kiasi kwamba kama umejenga/unaishi bondeni Kwa kweli ujipange. Nilipita jangwani kama 0800hrs bado magari yalikuwa yanapita ilà kwa hali hii sidhani.
 
Sasa hivi bado wamelala ila wakiamka tu utasikia wanatoa tahadhari kua mvua inatoka kusini mashariki kuelekea kaskazini magharibi kwa kasi ya kilo tatu na nusu kwa saa, pia bahari ikakua na mawimbi madogo madogo pamoja na ngurumo za radi kwa ukanda wa kilwa kivinje.
 
Tungependa kufahamu huu mradi wa DMDP. Mbona Tunaona maeneo mengine hatujengewi barabara kiwango cha lami, mitaro na mngekuwa na mipango ya muda mrefu mngejenga Centralised sewarage system Dar nzima maana biashara ya vyoo kujaa ni kadhia na inaleta magonjwa sana hapa mjini.

Ombi Mods: Anzisheni thread ya mradi wa maendeleo jiji la dsm DMDP na wahusika waje watujibu au wasome madukuduku yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za asubuhi wadau, maeneo ya Mbagala kuna mvua kubwa sana yenye radi inanyesha tangu majira ya saa 12 asubuhi hadi muda huu, radi ni za nguvu hadi ardhi inatetema, tuombe Mungu isilete madhara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wiki mbili zilizopita ilinysha mvua kubwa sana, huko Kivule radi iliua watu watatu na ng'ombe kadhaa. Wengine wengi vifaa vyao vya electronic viliunguzwa.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…