Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Hii ni kwa hisani ya blog ya habari247


Matokeo ya awali ya kura za maoni kwa wagombea udiwani na ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi uliofanywa jana katika baadhi ya kata yameanza kutangazwa huku baadhi ya vigogo wakiangushwa vibaya.

Baadhi ya majimbo ya Mkoa wa Dar es Salaam, yamekuwa na upinzani mkali, ambapo aliyekuwa Mbunge wa Segerea, Dk. Makongoro Mahanga na Jimbo la Ukonga na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa, wameanguka vibaya.

Katika matokeo hayo Jimbo la UKONGA: Anayeongoza ni Ramesh Patel kwa kupata kura 5139 dhidi ya Jerry Slaa aliyepata kura 1034.

SEGEREA: Bona Kalua anaongoza katika kura za awali na kumuangusha aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga.

ILALA: Mbunge aliyekuwa anaongoza jimbo hilo Mussa Azzan Zungu anaongoza katika kura za awali
KINONDONI: Idd Azzan anaongoza katika matokeo ya awali
UBUNGO: Dk. Didas Masaburi

Mwanahabari mkongwe Saed Kubenea anayegombea ubunge jimbo la Ubungo, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),ameibuka kidedea katika kura za maoni kwa kujizolea kura 61 akifuatiwa na Goodluck Mollel kura 20 na Gudat Lehad akiambulia kura nne.

CHALINZE: Ridhiwan Kikwete ameongoza kata kumi kati ya 15.
KIBAHA VIJIJINI: Hamoud Jumaa ameongoza kata nane kati ya 11.

BAGAMOYO: Dk. Shukuru Kawambwa ameongoza kata sita kati ya tisa.
KIBAHA MJINI: Silvestry Koka anaongoza kata tisa kati ya 14.

TANGA: Salum Kisauji (4240), Omary Nundu (3684), Kassimu Mbughuni (1218), Kassimu Makube (1082), Athuma Baruani (948). Matokeo hayo ni ya kata 16 bado kata 11.

KOROGWE: Kata ya Majengo ni Mary Chatanda anaongoza kwa kura 238, akifuatiwa na Francis Bago (83), Yussuph Nassir 21 na Mustapha Berko 12.

KOROGWE VIJIJINI: Kata ya Mnyuzi Stephen Ngonyani 30, Dk Edmund Mndolwa, 30, Ernest Kimaya 10, Cecilia Korassa 4, Allly Hozza 4.

PANGANI: Kata ya Pangani Magharibi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM, Jumaa Awesso anaongoza kwa kura 479, Abdulrahaman Magati 300, Salehe Pamba 270.

BUMBULI: January Makamba amepata kura,13,366, Kaniki kura 1,781, Mshihiri kura 171, Shekwevi kura 46 huku kura zote zilizopigwa zikiwa ni 15,364.

MOROGORO: Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(Utumishi) Celina Kombani,ambaye ni Mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo la Ulanga Mashariki ameshinda katika mchujo wa kura za maoni.

Kombani aliwashinda wapinzani wake Agustino Matefu na Daud Kitolelo kwa kuongoza kwa kura nyingi katika vituo vyote 123.

MOROGORO MJINI: Mbunge Mtetezi wa Jimbo la Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood ameelekea kushinda tena baada ya wanachama kumpigia kwa nyingi katika Kata 29 za manispaa hiyo.

Katika uchaguzi huo anachuana na wagombea wawili akiwemo Simon Barege , na Peter Ongara ambaye imeelezwa tayari alishajiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho.

DODOMA: Tawi la Chinyoya ndani ya Kata ya Kilimani: Anthony Mavunde alipata kura 91 akifuatiwa na Dk.David Malole, aliyepata kura 13.

Wagombea wengine na kura zao kwenye mabano, Haidary Guramali (34), Mloki Alexander Mloki (0), Robert Mchami (1), Anthony Kanyamakura (3), Emmanuel Kamara kura (2), Mohamed Ngori (0), Musa Luhamo (0) na Steven Masangia (15).

Matokeo ya awali ya kura za maoni za kusaka ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapindzuzi (CCM) katika majimbo yaliyopo baadhi ya mikoa ya kanda ya ziwa.

NYAMAGANA: Stanslaus Mabula
MUSOMA MJINI: Vedastus Mathayo
MUSOMA VIJIJINI: Sospeter Muhongo
BUTIAMA: Nimrod Mkono
RORYA: Lameck Airo
MWIBARA: Kangi Lugola

KAHAMA: Katibu wa CCM wa wilaya Alexandrina Katabi, alisema matokeo yote ya watia nia ya ubunge katika majimbo yote yaliyopo wilayani humo, yatatangazwa asubuhi leo.

Hata hivyo, katika hatua nyinngine wanachama zaidi ya 70 wa CCM wilayani humo, waliandamana na kuchana kadi zao na wengine kuzirudisha kwa madai ya kutoridhishwa na mchakato mzima wa upigaji kura.

BUKOMBE: Dotto Mpira alikuwa akiongoza kura za awali
GEITA VIJIJINI: Joseph Kasheku Msukuma alikuwa akiongoza
BUCHOSA: Charles Tizeba alikuwa akiongoza

NYANG’WALE: Hussein Nassor Amar
MBOGWE: Augustine Masele
SENGEREMA: William Ngeleja alikuwa anachuana na Lawrance Masha
GEITA MJINI: Costantine Kanyasu alikuwa anaoongoza
JIMBO LA MTAMA:Nape Mnauye karibu kata zote amejinyakulia kura nyingi dhidi ya wapinzani wenzake watano.

LUDEWA: Deo Filikunjombe katika matawi 13 ameongoza na kuwaacha wagombea wenzake mbali baada ya kupata kura 2933
KISARAWE: Seleman Jafo ameongoza kata 14 kati ya 16.

KALENGA: Mgimwa
MULEBA KUSINI😛rofesa Anna Tibaijuka
MOSHI VIJIJINI: Dk. Cyril Chami (5563), anayemfuatia ni Ansi Mmas (3176)

MWANGA: Profesa Jumanne Maghembe anaongoza kwenye kura za awali.

SENGEREMA: Ngeleja amepeta na kumshinda Lawrence Masha
MUFINDI: Cosatho Chumi ameongoza na kumuangusha Naibu waziri wa maliasili na Utalii Mahamoud Mgimwa

Source www.habari247.co.tz
 
Ni sawa tu..
.uongozi ni karama ya asili siyo lazima iibuliwe shuleni. Acha awaongoze maana hata wasomi wengi wao ni matapeli tu.
 
hata kama kusoma hujui hata picha tu huoni kuwa msigwa ubunge tayari anao na hana mpinzani hizo zako ni ndoto za bunuwasi.
 
Una akili sawa sawa wewe..Matiko yuko CCM? Au umezinduka toka kilabuni
Na hapo ndipo uwezo wako ulipofikia...
nimeshaelewa huna jibu,kwahiyo umeangalia weakness ya swali...but ulikuwa una uwanja wa kujibu General kama nilivyouliza...Salute "KIGOGO"
 
Uongozi wa kweli na kiongozi anaefahaa sio lazima ajue kusoma na kuandika kwani wengi wenye madigiliii wezi na waroho wenye uchu wa kusaka tonge wanufaishe matumbo yao...
 
Kama hamujui siasa ni bora musi changie chochote . Maana nitabishana na watu amabo hata mwetekiti wao wa mtaa hawamjui so its better to wait untill october alafu muone msigwa akirudi kuhubiria kanisani
 
Komoni ya kwa Mwagongo ni kali nahisi kama heroin hadi uwezo wa kuona picha ni mdogo....full blurr...😀😀:thumbdown::thumbdown:
 
Wassira naona ana staili ya 'tukose wote' yaani akishindwa yy basi na mwenzake akose ili liende Ukawa.

Mkuu wa wilaya tangu lini asimamie kura za maoni ndani ya vyama?
Mkuu wa wilaya ni mkuu wa usalaama ndani ya wilaya
 
Dah

Kweli CCM chama kubwa

Ukawa kama hawapo vile
 
kanikimbia kilabu cha barabara hapa kumbe ndo amekuja huku,njoo mama kisebengo anawaka
 
KURA ZA MAONI CCM
1. Mwigulu - Iramba
2. Nape - Mtama
3. Mwakasaka - Tabora Mjini
4. Mama Sitta - Urambo
5. Kadutu - Ulyankulu
6. Bashe - Nzega
7. Ngeleja - Sengerema
8. Seif - Igunga ktk jimbo jipya.
9. Masaburi - Ubungo
10. Jerry Slaa- Ukonga
11. Prof Kamala - Nkenge, Misenyi
12. Kagasheki -
13. Lukuvi - Isimani
14. January - Bumbuli
15. Muhongo - Musoma vijijini
16. Ndugai - Kongwa
17. Chumi - Mafinga
18. Kigola - Mufindi kusini
19. Mgimwa - Mufindi kaskazini
20. Filikunjombe - Ludewa
21. Mgimwa - Kalenga...
22. Lusinde - Mtera
23. Imani Moshi - Kaliua
24.Mwakasaka -Tabora mjini
25.Fenala Mkangara -Kibamba
26.Mapunda-Mbinga mjini
27.Masele -Kahama
28.Antony Mavunde-Dodoma hizi ndio data nilizopata

Alex gashaza- ngara
 
Back
Top Bottom