Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Kwa kipindi hiki ambacho wagonbea wa CCM wako kwenye mchakato wa kura za maoni kuwapata wagombea wao kumezuka malalamiko wao kwa wao kuchezeana rafu nyingi kwenye Uchaguzi.
Malalamiko wanayolalamikia ni pamoja na wizi wa kura,kutoa rushwa kila kona ya nchi.Tumesikia aliyekua mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu nchemba alikamatwa na TAKUKURU na kuhojiwa masaa matatu, Katibu wa itikadi na uenezi Taifa wa CCM alikamatwa na TAKUKURU na kuhojiwa masaa matano kwa kutoa rushwa huko jimbo la mtama mkoani Lindi,Wagombea wengi wanalalamika kukamatwa kwa kura zilizopigwa tayari ili hali Uchaguzi bado hujaanza.

My take;

Kwa hali hii ambapo tunaenda kupiga kura kushindanisha vyama mbali mbali 25 October hali itakuaje? Rafu hizi upinzani/UKAWA mmejiandaaje?
Mjue kabisa ushindi ni mgumu na rahisi kama mnavyofikiria, wanoeni mawakala wenu ipasavyo. Mjiulize ni kwanini CCM wanalalamikiana wao kwa wao? Mjue ikifika October ntalalamika ninyi.Ni tahadhari tu!
 
Matokeo Jimbo Tabora Kaskazini 1.ALMAS A. MAIGE 9000+,2.SHAFF SUMA 6000+,3.JOSEPH KIDAHA 5000+ jumla ya wagombea ilikuwa 10

Ila huu upumbavu wa wanyamwezi nashangaa sana. Wamemng'ang'ania mhindi Suma utafikiri ni mtu wa maana sana. Utajashangaa huyo Maige wakamkata kisha wakamrudisha Suma!
 
Kama kuna kitu ambacho kilikuwa kikinishangaza wakati wagombea wakizunguka kujinadi kabla ya kura za maoni ilikuwa ni habari kuwa waziri wa maliasili na utalii ambaye ni mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu kwamba hakubaliki na alikuwa anazomewa kila alipokuwa akienda. Ilifikia hatua hadi zikaanza kutembezwa message kwa sisi wakazi wa Singida kuwa kuna maagizo jamaa ahakikishe hapiti na juzi ikaenezwa propaganda kuwa anashikiliwa na takukuru kama ilivyokuwa kwa mheshimiwa Mwigulu.

Matokeo rasmi yametoka na mheshimiwa Nyalandu kawaacha mbali sana wapinzani wake kwa kuibuka na ushindi wa kishindo kwa kupata kura 13496 huku anaemfuatia akiwa na kura 5822. Nadhani hili ni fundisho kwa sisi watu wa Singida ambao kwa siku za karibuni tumeanza siasa za majitaka kuchafuana kupitia mitandao, tunasahau asilimia kubwa ya wapiga kura wako vijijini. Hiyo nguvu tungeielekeza kwenye shughuli za maendeleo tungefika mbali sana na mkoa wetu ungepiga hatua. Hongera kwa Nyalandu na hongera Nchemba, wananchi wameongea na sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Tukutane Oktoba.
 
Kwa kipindi hiki ambacho wagonbea wa CCM wako kwenye mchakato wa kura za maoni kuwapata wagombea wao kumezuka malalamiko wao kwa wao kuchezeana rafu nyingi kwenye Uchaguzi.
Malalamiko wanayolalamikia ni pamoja na wizi wa kura,kutoa rushwa kila kona ya nchi.Tumesikia aliyekua mbunge wa Iramba Magharibi Mwigulu nchemba alikamatwa na TAKUKURU na kuhojiwa masaa matatu, Katibu wa itikadi na uenezi Taifa wa CCM alikamatwa na TAKUKURU na kuhojiwa masaa matano kwa kutoa rushwa huko jimbo la mtama mkoani Lindi,Wagombea wengi wanalalamika kukamatwa kwa kura zilizopigwa tayari ili hali Uchaguzi bado hujaanza.

My take;

Kwa hali hii ambapo tunaenda kupiga kura kushindanisha vyama mbali mbali 25 October hali itakuaje? Rafu hizi upinzani/UKAWA mmejiandaaje?
Mjue kabisa ushindi ni mgumu na rahisi kama mnavyofikiria, wanoeni mawakala wenu ipasavyo. Mjiulize ni kwanini CCM wanalalamikiana wao kwa wao? Mjue ikifika October ntalalamika ninyi.Ni tahadhari tu!

Wote ambao hawTatendewa haki ndani ya ccm wataitafuta njee ya ccm na wananchi watazungumza kwenye box la kura
 
Omari Mhando ( OG Walawala) mmoja wa wagombea ubunge jimbo la Muheza Ameshindwa vibaya katika uchaguzi wa kura Za maoni ndani ya CCM uliofanyika jana.
Balozi Adadi Rajabu Ameshinda rasmi kura za maoni kwa kura nyingi na kuwaacha mbali wagombea wengine.
Kwa habari ambazo hazijathibitishwa inasemekana kwamba ndg Omari Mhando (OG) anategemea kukihama rasmi chama chake CCM na kwenda chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA)
 
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Bunda, Stephen Wasira ametangazwa kushinda kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya ulinzi mkali polisi.

Matokeo hayo ambayo yametangazwa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe na msimamizi wa uchaguzi wa CCM, Margret Mtatiro alisema Wasira ameshinda kwa zaidi ya kura 223 baada ya kupata jumla ya kura 6,429 akifuatiwa na Robert Maboto (6206), Christopher Sanya (1140), Exavari Lugina (846), Simon Odunga (547), Magesa Mugeta (446), Peres Magiri (385) na Brian Bita (263).

Matokeo hayo yalitangazwa jana majira ya saa 4 alasiri baada ya mvutano mkali tangu juzi usiku, ambapo ilidaiwa kuwa baada ya kujumlisha kura zote mpinzani wake Robert Maboto alionekana kumzidi Wasira kwa kura 67.

Hata hivyo kutokana na Wasira kutoridhika, uhakiki ulirudiwa tena ambapo majira ya saa 4 asbuhi jana Jeshi la polisi lilifika katika ofisi za CCM na kuweka ulinzi dhidi ya wapambe wa Maboto ambao walionesha wasiwasi wa Maboto kuporwa kura zake.

Kabla ya Polisi kufika katika eneo hilo, mkuu wa wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe alionekana katika ofisi hizo akifanyakazi kubwa ya kutuliza wafuasi wa Maboto ambao walikuwa wakiimba, ‘Maboto ni mbunge', Maboto ni Mbunge".

Hadi Matokeo yanatangazwa Mkuu huyo wa Wilaya alionekana akiingia na kutoka mara kwa mara ndani ya ofisi hizo ambazo shughuli za uhesabuji kura zilikuwa zikifanyika jambo ambalo halikuwaridhisha wapenzi wa wagombea wengine.

Pamoja na hayo Wakala wa Maboto aliyejitambulisha kwa jina moja la Chang'ang'a alikiri kuwepo mizengwe katika kurudia mahesabu ya kura hivyo yeye na Maboto wamesaini kutoridhwa na matokeo hayo.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi huku wanachama wengine wakipiga kelele kwa kutoridhishwa na matokeo hayo , Wasira alisema bado jimbo la Bunda mjini halijapata mgombea mpaka majina matatu ya washindi yatakapojadilliwa na halmashauri kuu ya CCM taifa(NEC).

"Sasa CCM ni mamoja, hapa sasa hakuna kikundi cha Wasira wala Maboto, tumepata mgombea mmoja atakayepambana na UKAWA, lakini mpaka majina yote yakajadiliwe katika halmashauri kuu ya CCM," alisema Wasira.

Baada ya matokeo hayo mamia ya wanachama ambao hawakuonesha kuridhwa na mchakato wa utangazwaji wa matokeo hayo walichana kadi za CCM na kuimba Ukawa huku wakidai CCM imekuwa ikiwaletea wananchi wagombea wasiowakubali hivyo watajiunga na UKAWA.
 
wana ccm kuweni watulivu,zoezi la uvuaji magamba linatekelezeka kimkakati,wataondoka mmoja mmoja kwenda kwenye kichaka cha ufisadi na mafisadi lilikojificha gamba kuu.Tumeanza na makongoro mahanga,now huyu na wengine watafuata,waondoke watuachie chama chetu wakulima na wafanyakazi tuanze upya.
 
Nimeona taarifa ya habari yani wanakulana wao kwa wao ka samaki, kila kona wizi , wao wenyewe ndo wanazidi kuchafuana, hawa jamaa ni noma
 
sam_4512.jpg


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Monaban ya jijini Arusha, Philemon Mollel ambaye pia ni Mgombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM akimwaga sera zake.​

Huyu mzee, ni mwepesi kama nini.......

Kazi tulishaimaliza Arusha
 
Hivi huyo Makongoro Mahanga si ndiye yeye kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alimfunga Fred Mpendazoe wa Chadema 'goli' la mkono kwa kukimbia na masanduku ya kura baada ya kugundua amieshindwa uchaguzi huo?

Itabidi Chadema sasa wawe makini sana na watu wa design kama ya Makongoro ambao wanataka kuja Chadema baada ya kupigwa chini kwenye kura ya maoni kwenye chama chao cha magamba.

Watu wa design hiyo kama kweli watakuwa na mapenzi ya kweli na Chadema basi wakubali kupokelewa lakini siyo kwa wao kutoa masharti ya kuingia CDM kwa kupewa fursa ya kugombea Ubunge, bali waanze kwanza kuwa wanachama wa kawaida.
Ebu fikiria tu wawe na akina 'Shibuda' kumi katika bunge! Nini hasa kitatokea? CHADEMA wanapaswa kulitafakari hili. Nilishauliza watawamanage au kuwadhibiti vipi hawa?
 
Back
Top Bottom