Friends Of Hon.Membe wapeta nafasi za ubunge.
Katika hali ya ushindani wa makundi hasimu ya kambi za urais ndani ya Ccm hadi sasa kundi la Bernard Membe limeonesha kung'ara dhidi ya kundi la Edward Lowassa.
Ushindi mkubwa unaovunja rekodi waliopata marafiki na mashabiki wa Bernard Membe kwenye kura za maoni nafasi za ubunge umezidi kuwaumiza vichwa marafiki na wapambe wa Edward Lowassa walioangukia pua.
Baadhi ya makada waliopo kwenye kambi ya Bernard Membe wameangusha "mibuyu" iliyojimilikisha majimbo na vyeo ndani ya Ccm kwa kutumia hela chafu.
Mmoja wa wanachama wa Ccm alisema,"Bernard Membe kasaidia kusafisha uozo kwenye chama.Wachafu waliomuunga mkono Edward Lowassa waanguka na kuhamia upinzani na waliobaki wamekosa dira na sasa wanasubiri huruma ya Ccm.Bernard Membe anazungukwa na waadilifu.Waliomuunga mkono ilikuwa lazima washinde kutokana na ukweli kwamba wana dhamira ya kusaidia nchi kama aliyonayo Bernard Membe mwenyewe ambaye pamoja na kukosa urais ila bado anaheshimu maamuzi na kukiheshimu Ccm".
Baadhi ya makada wanaomsapoti Bernard Membe na walioangusha "mibuyu" ya ufisadi iliyokuwa na Edward Lowassa ni Bona Kaluwa aliyemwangusha Dk.Makongoro Mahanga,Dc Masala aliyemwangusha Mathias Chikawe,Aboubakar Asenga aliyemwangusha Abdul Mteketa,Mnec Miraji aliyemwangusha Pereira Ame Silima na Nape Nnauye aliyemwangusha Suleiman Mathew.
Kwa uchache tu hapa imedhihirika Bernard Membe ana nguvu kuliko Edward Lowassa.Mzizi wa fitina umekatwa na bado matokeo mengine yapo loading.....tutazidi kuwaletea!