Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Noted with regret!
 

Titakuja kuelewa muda ni dawa kaka!!Ngoja tuone njia waliyoamua viongozi tuipite ili kuiondoa CCM.Yawezekana itafanya kazi,lakini viongozi wamejiandaa vizuri namna ya kumcontroll Lowassa?Kwenye majibu yake tumeona namna anavyojibu kwa kiburi cha pesa,je tutamuweza akiingia akawa na madaraka?
 
Ni kweli kabisa, maana hata hapo CHADEMA imethibitika zimetolewa 10b ili kununua ugombea. Rushwa ni kansa ya taifa.

Hili siwezi kusema maana hakuna TAA KUUKUU iliyotuambia kwamba kuna pesa zimekutwa huko...
 

Julius rugenalira siyo Wa escrow Hutu alikuwa raid Wa daruso 2003, ni kijana Fulani and strong alishirik ngomo Wa 2000 na iliyofuatia
 
Julius rugenalira siyo Wa escrow Hutu alikuwa raid Wa daruso 2003, ni kijana Fulani and strong alishirik ngomo Wa 2000 na iliyofuatia
Very good naona sasa umempatia vizuri kabisaaaaa. Ila sasa ndo keshakosa. Huyu Kamara si Balozi mbona anarudi tena? UKAWAAAAA Piga hodi.
Yahani CCM wamechoka hivi kwamba hawana wagombea??? si bora angebaki Asumpter
 
Baada ya matokeo ni walati muhafaka sasa kamati ya maadili kula vichwa.
 

Jamani mu nahitaji matokeo ya LINDI MJINI, MTWARA MJINI NA VIJIJINI.
 
JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI, WILAYA YA MUSOMA-MKOA WA MARA

Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Mhe Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo ameibuka mshindi katika kura za maoni ndani ya CCM kwa kupata ushindi wa kishindo katika kata zote 21 za Jimbo la Musoma vijijini ambapo matokeo kamili ni kama ifuatavyo;

Jumla ya waliopiga kura: 38,342

Idadi ya Kura


  1. Prof. Sospeter Mwijarubu Muhongo- 30,431 (79.4%)
  2. DC Anthony Mtaka- 3,457 (9.0%)
  3. Everest Maganga- 2,556 (6.7%)
  4. Prof. E Mujungu -988
  5. Stephen Mafuru- 421
  6. Wilberforce Witss- 393
  7. Nelson Semba- 186

Hongereni sana wana musoma vijijini kwa kuamua kuanza kujenga uchumi imara na kuutokomeza umasikini kwa kuchagua mwakilishi bora atakayesukumu gurumu la maendeleo kikamilifu pasipo shaka yoyote ile. Hongera sana Profesa Muhongo kawatendee haki wana Musoma vijijni na watanzania wote kwa ujumla.



JIMBO LA KIBAKWE, WILAYA YA MPWAWA- MKOA WA DODOMA

Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene amekuwa kati ya Mawaziri wa Serikali ya awamu ya nne ya Mhe Prof. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kushinda kwa kishindo katika kinyang'anyiro cha kura za maoni ndani ya CCM ambapo ameshinda kwa kishindo katika jimbo lake na kuwaacha mbali wapinzani wake.


  1. Simbachawene - 18,151
  2. Mwanyinge- 6,901
  3. Myang'ali- 3562
  4. Sabas- 430
  5. Ngiliule- 214
  6. Bendera- 410
  7. Shahel- 279


Hongereni wana Kibakwe kwa uamuzi sahihi.

Asanteni.
 

Ushindi wa Simbachawene ni wa goli la mkono na wala hakubaliki jimboni kwetu kulingana kauli zake za kibabe na jeuri, Kiukwel wananchi wameumizwa na matokeo hayo kwa sababu anajiona Mungu mtu.
Viongozi wa CCM mliombeba Simbachawene na kukandamiza sauti ya wengi Mungu awasamehe maana hamjui mlitendalo
 
Tumewekewa nguzo za umeme na Prof Muhongo mradi wa REA, Lakini Simbachawene mara baada ya kupewa wizara kagoma kuleta umeme kisa hakubaliki kijijini so anakomoa wananchi,
Mleta Uzi Mungu akusamehe kwa sababu hujui mateso tunayopitia kupitia huyu mtu uliemuita CHAGUO SAHIHI.
Tunamuomba Rais ajae amkumbuke Prof Muhongo ktk wizara yake ambayo Simbachawene hastahili kuiongoza
 
Kwani ndio mwisho? Badomna nafasi 25th October 2015
 
Kwa upepo wa mchakato unavyoendelea kwenye hili zoezi ndani ya CCM, ni kazi sana kuamini kama hawa jamaa hawajatumia rushwa, nnachoweza kukiona hapa ni kwamba wamefanikiwa kutumia mbinu bora zaidi za rushwa kuliko zile waliotumia wenzao wakakamatwa.
 
Mwigizaji Irene Uwoya ameashinda kura za maoni Ubunge Viti Maalum (vijana) huko Tabora kwa kupata kura 38 huku mpinzani wake akipata kura 34. Ubunge wanukia kwa Irene, heko kwake.
 
Yesu, hivyo vimini na vikuku vitazidi vya yule mkuu wa wilaya. Vipi, Kamata kapita?
 
Shinji ni kweli kabisa kumekuwepo kwa ucheleweshaji wa ukamilishaji wa miradi ya umeme vijijini (REA), mara ya mwisho kabla Prof Muhongo hajatoka wizarani alitoa maelekezo kwa wakandarasi wote wanatekeleza miradi ya umeme na makubaliano ilikuwa tarehe 30 Juni miradi yote iwe imekamilika. Bila shaka serikali ya awamu ya tano itahakikisha hilo linakamilika kwa wakati. Shabaha kubwa tunayohitaji watanzania ni wanancho wote tuishio maeneo mjini ya vijijini tunaunganishiwa umeme kwa bei nafuu na wa uhakika.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…