JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI, WILAYA YA MUSOMA-MKOA WA MARA
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Mhe Prof. Sospeter Mwijarubi Muhongo ameibuka mshindi katika kura za maoni ndani ya CCM kwa kukupata ushindi mkubwa sana katika kata zote 21 za Jimbo la Musoma vijijini ambapo matokeo kamili na kama ifuatavyo;
Jumla ya waliopiga kura: 38,342
Idadi ya Kura
- Prof. Sospeter Mwijarubu Muhongo- 30,431 (79.4%)
- DC Anthony Mtaka- 3,457 (9.0%)
- Everest Maganga- 2,556 (6.7%)
- Prof. E Mujungu -988
- Stephen Mafuru- 421
- Wilberforce Witss- 393
- Nelson Semba- 186
Hongereni sana wana musoma vijijini kwa kuamua kuanza kujenga uchumi imara na kuutokomeza umasikini bila shaka mtaanza kuyaona maendeleo ya dhati.
JIMBO LA KIBAKWE, WILAYA YA MPWAWA- MKOA WA DODOMA
Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene amekuwa kati ya Mawaziri wa Serikali ya awamu ya nne ya Mhe Prof. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kushinda kwa kishindo katika kinyang'anyiro cha kura za maoni ndani ya CCM ambapo ameshinda kwa kishindo katika jimbo lake na kuwaacha mbali wapinzani wake.
- Simbachawene - 18,151
- Mwanyinge- 6,901
- Myang'ali- 3562
- Sabas- 430
- Ngiliule- 214
- Bendera- 410
- Shahel- 279
Hongereni wana Kibakwe kwa uamuzi sahihi.
Asanteni.