Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

kumetokea hali ya sinto fahamu huko tarime baada ya kukamatwa kwa kura zaidi ya elfu 20000 zilizo onyesha jina la nyangwine, ni matumaini yangu kua ccm inaelekea kudondoka katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu kutoka na kutojiamini na wanachama wao. Ni jambo lakushangaza katika jamii kwa watia nia wa ccm kwa ngazi mbali mbali kukamatwa na rushwa. Hii ni dalili tosha la anguko la ccm mwaka huu.
 
Uchaguzi umeharishwa hadi kesho baada ya kukamatwa kwa karatasi zenye majina ya Nyambari na Gaudensia zilizotikiwa kwa majimbo ya Tarime mjini na Vijijini. Ni elfu ishirini 20,000 Invisible

Chanzo:ITV
 
Last edited by a moderator:
Hehehehe kawaida iyo ndani ya chichiem
 

Unataka kusemaje.........mbona umeongea VIRAI.....elezea kidogo walau iwe KISHAZI ila kisiwe tegemezi. Soma vizuri majina ya wagombea wa KYERWA kisha useme kuhusu huyo chacha. Pia zungumzia neutral names ambazo umeshindwa kuzi attach.... na utumbo wako utueleze unawafahamu vipi.
 

ahaaaaa loh huyu mtoto norbeth kobwino aliwa lini? Kafufukia wap? Loh kumbe na mm siku moja ntakuwa mbunge loh, norbeth wewe katafte uzoefu yo too young to this loh.

Mkuu ukipata pic ya norbeth kobwino mtoto wa mwl kobwino niwekee nione kama alikua loh. Shule moja alimaliza la 7 nikiwa std 3 and since then sijawai mwona loh
 

😱😱
 
Hivi huyu Mwinyi siyo tamaa ya MADARAKA, yaani wao wakiona Unguja kimenuka wanakuja kufanya FUJO bara, huu ni upuuzi unatakiwa kuwa defined kwenye katiba

Wanadhani majina yatawabeba, wamuche Dr bana teh teh teh
 
Wandugu vipi Habari ya Zungu na kijana mbishi Mrisho Gambo???? Mwenye update Jaman pande hizo!
 
Updates za uchaguzi jimbo la Kongwa kwa mheshimiwa Ndugai, matokeo katika baadhi ya vituo mheshimiwa ambaye alituhumiwa kumpga mgombea mwenzake ameshnda kwa kura nyngi sana dhidi ya wagombea wenzake
 
MWAKYEMBE AWABWAGA MWAKALINGA, LOWASSA NA KYELA FM KWA KISHINDO
Na Malikira S.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Kyela aliyemaliza muda wake, Dk. Harrison Mwakyembe, amewabwaga kwa kishindo kikubwa wahasimu wake wa kisiasa kwenye kura za maoni zilizofanyika wilayani Kyela leo.

Muda wa saa kumi jioni ulipotimu wa kukamilisha upigaji kura, Mwakyembe alikuwa tayari anaongoza kwenye vituo karibu vyote kwa zaidi ya asilimia 75, akiwaacha kwa mbali wagombea ubunge wenzake 9 akiwemo George Mwakalinga anayeishi Uingereza na kuitumia redio yake, Kyela FM, kinyume na taratibu kwa kujitangaza kwa wiki mbili mfululizo kuwa chaguo bora na kumkandia Dk. Mwakyembe kuwa hafai.

Mwakalinga, mhandisi aliyekosa kabisa haiba ya uanasiasa kutokana na uongeaji wake wa taratibu usio na mvuto na hasira kali za papo kwa papo, anadaiwa kuwa karibu na Edward Lowassa, mwanasiasa mkongwe nchini aliyehamia CHADEMA kutoka CCM hivi majuzi, kutokana na kaka yake Mwakalinga kuoa Monduli.

Pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kumtahadharisha asiitumie kisiasa redio yake aliyoisajili kama redio ya jamii kwa kukejeli, kutukana na kudhalilisha wengine, Mwakalinga kwa kushirikiana na wanasiasa wenzake wanane walioungana naye kumkabili Mwakyembe, ameendelea kuitumia Kyela FM kumshambulia Dk. Mwakyembe na kuwasihi wananchi wasimpe kura.

Mwakalinga kwa kushirikiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kyela, Gabriel Kipija, mwanasiasa mchanga anayefundisha Chuo cha Uhasibu Mbeya, John Mwaipopo na mkandarasi anayetuhumiwa kuchelewesha miradi mitatu ya barabara wilayani Kyela, Vincent Mwamakimbula, wamekuwa wakiwalipa fedha wafuasi wa CHADEMA kumfanyia fujo Dk. Mwakyembe kwenye mikutano ya kujinadi kwa nia ya kumvunja moyo.

Dk. Mwakyembe kama ilivyo kwa wanasiasa wazoefu, hakuteteleka na aliendelea kuelezea utekelezaji wa Ilani za Uchaguzi za CCM za 2005 na 2010 na kuwathibitishia wananchi Kyela kuwa wilaya yao imepiga hatua kubwa ya maendeleo.

Idadi kubwa ya wananchi Kyela hawajafurahishwa na udhaifu wa TCRA wa kushindwa kusimamia sheria zake, hivyo kuiacha Kyela FM ikivuruga mchakato wa kidemokrasia ndani ya CCM kwa zaidi ya wiki mbili.

Taarifa tulizopokea toka kwa mawakala wa vituo karibu vyote wilayani Kyela zinaonyesha Mwakyembe akiwa mbele ya wagombea wengine na huenda akapata zaidi ya asimilia 75 ya kura zote.
 
Uchaguzi wa kura za maoni kupitia CCM katika jimbo la Tarime Mjini na Vijijini umeahirishwa hadi kesho baada ya kukamatwa kura feki Zimekamatwa Kura feki zaidi ya elfu 20 zikiwa zimewekewa alama ya NDIO kwa majina ya wagombea Nyambare Nyangwine na Gaudencia Kabaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…