Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Leo ni August 1,2015 Wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) nchi nzima wanakusanyika katika maeneo ya matawi yao kuchagua mgombea mmoja atakayeshindana na wagombea wengine kutoka vyama tofauti na CCM.

Mchakato wa kampeini katika mkoa huu zimetawaliwa na vituko,udhalilishaji kwa baadhi wa wagombea hivyo hata upigaji kura za maoni utakuwa hivo hivyo,hii ndiyo sababu inatufanya tufuatilie live kura hizi.

Updates...

MORE UPDATES:

vo matokeo ya kura za maoni ubunge ilemela mwanza nani kashinda?
 
Yeye katoa milion 6 wenzake wakapanda dau.
CCM ina wenyewe.
 
Friends Of Hon.Membe wapeta nafasi za ubunge.

Katika hali ya ushindani wa makundi hasimu ya kambi za urais ndani ya Ccm hadi sasa kundi la Bernard Membe limeonesha kung'ara dhidi ya kundi la Edward Lowassa.

Ushindi mkubwa unaovunja rekodi waliopata marafiki na mashabiki wa Bernard Membe kwenye kura za maoni nafasi za ubunge umezidi kuwaumiza vichwa marafiki na wapambe wa Edward Lowassa walioangukia pua.

Baadhi ya makada waliopo kwenye kambi ya Bernard Membe wameangusha "mibuyu" iliyojimilikisha majimbo na vyeo ndani ya Ccm kwa kutumia hela chafu.

Mmoja wa wanachama wa Ccm alisema,"Bernard Membe kasaidia kusafisha uozo kwenye chama.Wachafu waliomuunga mkono Edward Lowassa waanguka na kuhamia upinzani na waliobaki wamekosa dira na sasa wanasubiri huruma ya Ccm.Bernard Membe anazungukwa na waadilifu.Waliomuunga mkono ilikuwa lazima washinde kutokana na ukweli kwamba wana dhamira ya kusaidia nchi kama aliyonayo Bernard Membe mwenyewe ambaye pamoja na kukosa urais ila bado anaheshimu maamuzi na kukiheshimu Ccm".

Baadhi ya makada wanaomsapoti Bernard Membe na walioangusha "mibuyu" ya ufisadi iliyokuwa na Edward Lowassa ni Bona Kaluwa aliyemwangusha Dk.Makongoro Mahanga,Dc Masala aliyemwangusha Mathias Chikawe,Aboubakar Asenga aliyemwangusha Abdul Mteketa,Mnec Miraji aliyemwangusha Pereira Ame Silima na Nape Nnauye aliyemwangusha Suleiman Mathew.

Kwa uchache tu hapa imedhihirika Bernard Membe ana nguvu kuliko Edward Lowassa.Mzizi wa fitina umekatwa na bado matokeo mengine yapo loading.....tutazidi kuwaletea!

Lowassa yupi tena ktk CCM...??
 
Rejea Kichwa Cha Habari Na Naombeni Majibu Na Kama Mkiwa Mmetupitishia Abdallah Majura au Jerry Muro NAHAMA Rasmi Kawe, CCM Na Nahamia Nami CHADEMA. Nasubiri Majibu Yenu Ili Nijue Na Mimi Niitishe Press Conference Kama Lowassa na Mahanga au Hapana. Waandishi Wa Habari Jiandaeni Kwani Kama CCM Wakiwapitisha Mmoja Kati Ya Hao Watajwa Hapo Juu Nitawaita Katika Mkutano Nanyi Katika Nyumba Hii Niliyopanga Kwani Baba Mwenye Nyumba Wangu Kakubali Kunipa Kibaraza Chake Niweze Kuzungumza Nanyi.
 
Aden rage huyo siku wanamuhoji clouds fm michezo story3 za yule jamaa tupatupa nilishangaa rage anajisifu kula pipi za wanaukawa anajielezea kuwa kila wakigoma kazi yake kupita meza mojamoja anachukua pipi.........sasa sikuelewa hiki ndio walichomchagulia wananchi au na wangemrudisha ningebadili kabila
 
Pole classmate wangu Mtela aka Ganzi enzi za mbeya secondary. Hiyo ndo zawadi ya usaliti. Vp Mwigulu hajakupiga tafu? Au ndo alikukopa hiyo ml 6 then ukiingia mjengoni utamlipa... kwi kwi kwiiiii

Ganzi aliondoka CDM kwa mbwembwe! Sasa yamemkuta tena.
 
Mtela Mwampamba inabidi ukaendelee kuuza duka lako la nguo maana hakuna namna nyingine tena.
 
Alitema big G kwa karanga za kuonjeshwa...
 
Pole Mwampamba. Kutoka kura 32,000 ulizopewa na wana Mbozi wakati ukiwa mgombea kupitia Chadema mpaka kura tatu! Duh! Heri uache siasa au uvae sketi upewe viti maalum. Na huo mwili utapendeza kweli kweli.
 
Kama wamehonga kupita wengine lazima wapete. CCM inanuka rushwa na damu kumwagika kwenye kura za maoni.
 
Acha unyanyasaji wa kijinsia wewe kwani mwanamke hawezi? Lolote unalosema na kudhani juu ya mwanamke,jua inamrudia mama yako,dada yako na shangazi yako.

Huo ndio ukweli mchungu,makabila ya Wamasai na Wakurya kuongozwa na mwanamke ni nadra sana,CCM kama wangemsimamisha mgombea mwanamme Tarime Mjini angemsumbua sana Esther Matiko,lakini kwa kumsimamisha Gaudensia Kabaka ni kama waameshamtangaza Esther Matiko kuwa Mbunge wa Tarime Mjini
 
Yaani hawa mawaziri walikua mizigo kwa wizara, walishindwa kutetea maslahi ya maaskari bungeni tofauti na waziri wa ulinzi alivyokua akipigania maslahi ya wanajeshi, pia wameshindwa kuleta maendeleo kwenye majimbo yao, kwa hiyo WAKATWE TU.

Kama hukufuatilia bajeti ya wizara ya mambo ya ndani na ulinzi msimu huu usichangie thread yangu sababu utakua unashindana bila reference.
 
Kwa habari nilizozipata kutoka Bunda mjini ni kwamba Wasira anaenda kupita. Pia jimbo la Mtama Lindi mheshimiwa Nape Nnauye Mambo yamemunyookea...nitawaletea kura zilivyo kwa kila mgombwa soon.Kama una ukweli wa sehemu yako tuwekee..pia naambia naibu spika Mh Ndugai upepo upo vizuri kwake.

unamatokeo ya nkas magharibi na kusin kama unayonisaidie
 
Huo ndio ukweli mchungu,makabila ya Wamasai na Wakurya kuongozwa na mwanamke ni nadra sana,CCM kama wangemsimamisha mgombea mwanamme Tarime Mjini angemsumbua sana Esther Matiko,lakini kwa kumsimamisha Gaudensia Kabaka ni kama waameshamtangaza Esther Matiko kuwa Mbunge wa Tarime Mjini

Mmmh Viroba vya mchana nini!!
Esther Matiko ni Mwanaume?
 
Yaani hawa mawaziri walikua mizigo kwa wizara, walishindwa kutetea maslahi ya maaskari bungeni tofauti na waziri wa ulinzi alivyokua akipigania maslahi ya wanajeshi, pia wameshindwa kuleta maendeleo kwenye majimbo yao, kwa hiyo WAKATWE TU.

Kama hukufuatilia bajeti ya wizara ya mambo ya ndani na ulinzi msimu huu usichangie thread yangu sababu utakua unashindana bila reference.

wewe uliefuatilia weka ushahidi angalau takwimu za bajeti!
usiendeshwe na matukio. ulichelewa nini kuanzisha uzi huu
 
Yaani hawa mawaziri walikua mizigo kwa wizara, walishindwa kutetea maslahi ya maaskari bungeni tofauti na waziri wa ulinzi alivyokua akipigania maslahi ya wanajeshi, pia wameshindwa kuleta maendeleo kwenye majimbo yao, kwa hiyo WAKATWE TU.

Kama hukufuatilia bajeti ya wizara ya mambo ya ndani na ulinzi msimu huu usichangie thread yangu sababu utakua unashindana bila reference.

Waziri wa mambo ya ndani ni yule bwana Chikawe? alitishia kuzifuta taasisi za kidini (makanisa) kwa kuwa zilihamasiha watu waipigie katiba pendekezwa kura ya HAPANA. Kafutika yeye!:cheer2:
 
Back
Top Bottom