Updates za Kimbunga Hidaya: Ulipo hali ikoje?

Updates za Kimbunga Hidaya: Ulipo hali ikoje?

Hivi kubashiri hali ya hewa ni dhambi?

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Siyo dhambi kwa sababu hawamaanishi kubashiri au kutabiri kule tunakokujua sisi bali wanapima kwa vipimo vya kitaalamu. Kama ilivyo vitu vya mwanadamu haviko perfect na ndiyo maana hata wakati mwingine wanasema hivi kisha inatokea vingine au tofauti kidogo, muda mwingine wanasema itakuwa hivi kisha baada ya muda kabla haijawa wanasema tena itakuwa vingine nk.

Kwahiyo ni uchache tu wa msamiati katika kiswahili ndio sababu tunasema utabiri wa hali ya hewa lakini haimaanishi TMA wamekaa tu kumtegemea mzee fulani mwenye nyota au jaha au kipawa au nguvu fulani ya kiroho atabiri ndipo watangaze, laa! Bali wanapima hali ya hewa kwa vipimo mbalimbali ndipo wanacalculate mpaka kupata kuona hali ya hewa itakavyokuwa mbele. Kwahiyo UTABIRI WA HALI YA HEWA= MATOKEO YA UPIMAJI WA HALI YA HEWA

Kutabiri ambako ni dhambi ni ile ya kuletewa habari na mashetani kisha mtu akasema natabiri mwakani kiongozi mkubwa sana atafariki kwa njia ya...! Lakini kama watu wamesuka njama ya kumuua kiongozi huyo kisha mmoja kati yao akasema hadharani kuwa mwakani siku fulani naona kuna kiongozi mkubwa atafariki kwa njia ya...! Huyu hatusemi ametabiri hata tukio likija kutokea kwa namna ileile aliyosema!

Mfano mwingine mwizi akiiba kwenye majiji yetu hususan Dar wakimkamata wanamtia kiberiti aghalabu. Mzee mwenye kijana mwizi mwandamizi mkoani atakapokuwa amepata habari mwanaye huyo amehamia kuishi Dar akasema "mwanangu hatamaliza mwaka anakufa kifo kibaya sana cha kuchomwa moto". Ikitokea kweli ndani ya muda mfupi kijana kapigwa vitofa kafa huko Dar hatuwezi kusema "Baba alitabiri" bali itakuwa "Baba alisema!"

Kuna jambo lingine hapa tuliweke sawa nalo ni juu ya kubashiri au kubet na lugha nyingine za mfano huo. Hii kitu kuna wanaowianisha na ishu ya hali ya hewa kwa kusema mbona TMA wakibashiri mnasema halali ila sisi tukibashiri mnasema haramu? Kwanza mtu anayesema kauli kama hizo inabidi awahiwe haraka sana kabla ubongo haujaathirika zaidi!

Kinachokatazwa pale ni ile biashara inayotokeza pale na wala si vinginevyo! Haya sasa na watuambie hawa watu wa kubet je TMA wakishasema kesho kimbunga na mvua watu wachukue tahadhari je kuna muamala gani umefanyika hapo?

Ninachomaanisha ni kwamba kama mtu ataonelea katika nafsi yake au atasema hadharani kuwa timu fulani itashinda kisha mwingine akabisha basi hapana ubaya wowote kwani huenda kuna viashiria wote wawili wameviona kila mmoja kwa namna yake mfano mazoezi ya kutosha, usajili, hali ya uwanja, historia ya timu, nk.

Lakini kama watu hao wanafikia kuweka kitu katika hayo wanayoyaamini yatajitokeza kisha atakayekosea anakuwa ameliwa tayari hapo kumeingia muamala wa biashara ambapo kunakosekana sharti fulani fulani za biashara halali na ndiyo maana waislamu wanaambiwa KUBET HARAMU

Kubashiri pia tukienda kiundani tunakuta ilikuwa ni kazi ya mitume ambapo maana yake ni kuwapa habari njema wale wanaowaamini wao na kutekeleza wanayoambiwa. Habari njema yenyewe ni juu ya malipo mema na neema watakazopata mbinguni.
 
Kubashiri hali ya Hewa××
Kutabiri hali ya Hewa✓✓
Nafikiri hapo maana ni moja mkuu
Kiswahili ni chetu na hatujakikariri unaweza kutumia neno moja wapo kati ya hayo na ukaeleweka kwa maana moja

Kitabu cha dini kinasema kubashiri ni dhambi hii imekaaje

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Tuambieni basi nini kinaendelea huko mjini kabla vi betri vyetu vya simu huku vijijini havijaituishia...
 
Update Iko hivi. Huyo Hidaya mnaemtaja Kila saa Sasa hivi yupo guest na bwanake. Over
 
GMtiGDnXkAAvTs9.jpeg
 
Back
Top Bottom