Upendo Peneza (CHADEMA) amlipua Rais Magufuli, amtaka alipe kodi kutoka kwenye mshahara wake

Kuhubiri ni rahisi kuliko kutenda. Hata alipokula pale mgahawani mwanza hakuomba risiti
Kwani uliona wakati anatoa hiyo pesa? Kwa taarifa yako kile chakula kiliwekwa order na watu wa usalama wa taifa na ndo waliokilipia na risiti walipewa usiwe unakupukia mambo
 
Huu ndio ujasiri. Kwa hakika huyo dada kaonyesha uelewa, na vile vile kaongea point...

Namuona huyu dada angali ni kijana ila atafika mbali sana kisiasa. She is another Hillary Clinton in Bongo
Kwa kuhoji? Maneno yenyewe ameyaokota jamii forum. Wajenga hoja wapo akina Mnyika
 
....

.....Mkuu kwenye "ngawira" hata Yuda juwa hiyo kitu
 
Anataka yeye tu ndio aishi kama malaika nchi hii,, wengine tumeambiwa tunaishi kama mashetani, na wakurugenzi wanapunguziwa mshahara waishi kama sie mashetani,,
 
Mjumbe wa mkutano mkuu wa CHADEMA kupitia BAWACHA Bi UPENDO PENEZA akihojiwa katika kipindi cha STAR TV cha vijana na siasa tarehe 17/11/2014 kasema kuwa TAJIRI SABODO alitoa mamilioni ya hela kwa Ajili ya ujenzi wa Chuo cha siasa cha CHADEMA.
Swali langu ni je CHADEMA ujenzi wa hicho chuo hicho umefikia wapi? Na kiko eneo lipi? Wilaya gani na mkoa gani? Walau kiwanja mmeshanunua au mmekula hela za mzee wa watu? Nitashukuru sana nikipata majibu.

Nitashukuru sana endapo nitapewa hilo jibu
Wenu mtiifu EAST AFRICAN EAGLE
 
Mzee ukipewa wilaya ya Tandahimba utaenda? Komaa tu jitoe ufahamu upate ukuu wa wilaya uachane na kula kulala ya Houston
Tatizo lenu mnataka wengine ambao wana fikra kinzani na ninyi wasiongee au kuchangia ila ninyi ndiyo muongee au kuchangia. Haya ni mawazo ya kidikteta na upofu wa fikra.

Wewe ambaye hukomai na hujitoi ufahamu unafanya hivyo ili upewe wilaya gani?

Hizi ni fikra mufilisi au ukosefu wa nguvu za hoja.
 
Kwani uliona wakati anatoa hiyo pesa? Kwa taarifa yako kile chakula kiliwekwa order na watu wa usalama wa taifa na ndo waliokilipia na risiti walipewa usiwe unakupukia mambo
Ilitakiwa waonekane wakilipa na kuchukua risiti, kwani kama ni usalama wa taifa ndio hawapewi risiti? Kutoa oda ni jambo lingine na kukamilisha malipo ni jambo lingine, wewe ndio unakurupuka, ukisikia usalama wa Taifa unafikiri ni watu kutoka sayari nyingine?!
 
Kwani wenzangu nyie hili mmelipatia wapi,si nasikia sasa hivi huruhusiwi kusikiliza kitu chochote kinachofanyika bungeni hadi kichaguliwe na serikali ya viwanda?
 
RAIS yupo exempted kulipa kodi ,kwa mujibu wa income tax act 2004 ambayo wabunge wenyewe walipitisha, labda kipindi hicho binti upendo peneza alikuwa bado primary school.
angesema waibadili hiyo sheria sio kulipa kodi ......................
Lakini hiyo Act sio msaafu wala biblia,vyaweza kubadilishwa hivyo vifungu ili Rais na wabunge wote walipe kodi.Ni kwanini Rais asilipe kodi labda tungeanzia hapo
 
RAIS yupo exempted kulipa kodi ,kwa mujibu wa income tax act 2004 ambayo wabunge wenyewe walipitisha, labda kipindi hicho binti upendo peneza alikuwa bado primary school.
angesema waibadili hiyo sheria sio kulipa kodi ......................

Na pia anapaswa kujua ALL PEOPLE ARE EQUAL BUT SOME ARE MORE EQUAL THAN OTHERS
 

NADHANI MAGUFURI KUSIMAMIA SHERIA KUNAMGARIMU LAKINI LAZIMA ASIMAMIE. KILA SIKU MH RAIS ANASEMA WATU WALIPE KODI KWA MJIBU WA SHERIA KWA AJILI YA MAENDELO YETU. KAMA SHERIA INATOA UNAFUU KWA RAIS BASI BUNGE LIBADILI SHERIA HATA LIKISEMA WAFANYA BIASHARA WOTE WASILIPE KODI NI SAWA. LAKINI SI HAKI KUSEMA MH RAIS HALIPI KODI WAKATI SHERIA INASEMA LABDA ASILIPE?KAMA NDIVYO LAZIMA PIA BUNGE LILETE SHERIA INAYOTAKA ALOWANCES ZOTE KUANZIA PERDIEMS ZILIPWE KODI.
 
Hoja za CHADEMA bana kama majuha vile maanaa kwasasa hoja kwao eti ni mshahara wa Rais kweli ndiyo kilichowapeleka bungeni hawa wabunge.
 
Tunampongeza kwa kuonyesha uzalendo wa hali ya juu
 
kwa kuwa Rais wetu mpendwa anapenda kuishi kama mtanzania wa kawaida hadi kufikia kutangaza mshahara wake wa 9,500,000.00Tshs ni busara hiyo hiyo aitumie kulipa kodi kama anao waongoza na itakuwa vizuri sana maana atakuwa anaishi ndani ya kauri zake kwa mifano halisi. nina imani na pale Mwanza airport alipotununulia soda alikuwa mstari wa mbele kudai risiti. KIONGOZI LIPA KODI TUJENGE TANZANIA YA VIWANDA!!!!!!!!!!!!

Vile vile anaweza kutumia uwezo ule ule wa kutumbua majipu bila kuyahoji kulipa kodi nje ya katiba kwa ajili ya usitawi taifa lake!!!!!!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…