Upendo Peneza (CHADEMA) amlipua Rais Magufuli, amtaka alipe kodi kutoka kwenye mshahara wake

Upendo Peneza (CHADEMA) amlipua Rais Magufuli, amtaka alipe kodi kutoka kwenye mshahara wake

Mjumbe wa mkutano mkuu wa CHADEMA kupitia BAWACHA Bi UPENDO PENEZA akihojiwa katika kipindi cha STAR TV cha vijana na siasa tarehe 17/11/2014 kasema kuwa TAJIRI SABODO alitoa mamilioni ya hela kwa Ajili ya ujenzi wa Chuo cha siasa cha CHADEMA.
Swali langu ni je CHADEMA ujenzi wa hicho chuo hicho umefikia wapi? Na kiko eneo lipi? Wilaya gani na mkoa gani? Walau kiwanja mmeshanunua au mmekula hela za mzee wa watu? Nitashukuru sana nikipata majibu.

Nitashukuru sana endapo nitapewa hilo jibu
Wenu mtiifu EAST AFRICAN EAGLE
Ina uhusiano gani na kodi ya Magufuli?
 
hivi waliozipitisha hizi sheria sijui walikuwa wamelala,"eti mshahara wa Rais haujadiliwi popote pale",jamani amekuwa Mungu?ndio tabu ya zile "ndiyooooooo".Mshahara wa rais hautajadiliwa popote,wanaoafiki waseme ndiyo,mijamaa "ndiyooooo".
...

.....ndiyooooooooooooo
 
RAIS yupo exempted kulipa kodi ,kwa mujibu wa income tax act 2004 ambayo wabunge wenyewe walipitisha, labda kipindi hicho binti upendo peneza alikuwa bado primary school.
angesema waibadili hiyo sheria sio kulipa kodi ......................
Obama wa Bongo, nakubaliana nawe kweli mbunge inabidi apeleke hoja ya kubadili sheria ili raisi alipe kodi
 
Nadhani baba yako anajuta kuwa TOTO la aina yako,HASEMI Tu,.
Baba angu hawezi juta wala hata juta maana katufundisha kujali future na ndio nilivyo, hasara kwa baba ako mwenye mtoto anaetafakari yaliyopita bila kuganga yajayo.
 
Mbunge kamshauri Rais awe mzalendo ,afunge mkanda ....alipe kod...au ndo kusema ,ccm wanamuona rais ni mtakatifu haguswi.......alipe kod kulipa kod ,haijalishi ni uzalendo

Sheria ndio inahukumu mtu kuwa ni mtakatifu au la!! Sheria inasema Raisi hatakiwi kulipa kodi na halipi ni Mtakatifu huwezi kusema sio mtakatifu sababu hajavunja sheria ya kodi!! Kaitii.Inasema asilipe na yeye halipi.

Huyo mbunge angeanzisha mjadala wa kubadili sheria ya kodi ili kila mtu alipe kodi wakiwemo wabunge.Ila hiyo hoja akiianzisha na ikapita asahau kabisa ubunge viti maalumu kupitia CHADEMA hawatampa tena kwani kawapunguzia ulaji.
 
Tatizo la wabunge wetu ni kutojitambua. Hawaelewi kabisa kazi yao ni nini? Kwa sheria walizozipitisha wao wenyewe Magufuli akilipa kodi atakuwa anakwenda kinyume na sheria. Huyo mbunge badala ya kuleta mipasho bungeni angekuja na hoja binafsi. Silly season!
 
Mbunge hajui kuwa kazi za bunge ni kutunga sheria. Apeleke hoja kuwa Rais akatwe kodi kwenye mshahara wake. Sio kubwabwaja tu.
 
Safi sana ngoja za bungeni ziaje kuvuja kwa kasi, hapo ndio CCM wataelewa kuwa dunia ya sasa hakuna kitu kinaweza kufichwa.
Tena sasa zitakua zinakuja za upinzani halafu waanze kupata kazi ya kukanusha, watabanaa mwisho wataachia
 
Fanya utafiti ndg, wabunge wanakatwa kodi

Posho za vikao wanakatwa kodi?usituletee kichefu chefu hapa watu tuna hasira na hizo posho za vikao acha tu.Hawalipi kodi maeneo kibao.Magari yao tu wanayokopeshwa wanalipa kodi WAO WENYEWE TOKA MIFUKONI KWAO? jibu ni hapana.Mlalahoi akinua kigari used cha milioni tatu analipa kodi karibu nmara tatu ya hicho kigari wakati mbunge anaaachiwa tu.

Kuna mambo hawalipi kodi usiwatetee
 
mi sikusoma digirii..
lakini kama mshahara wa rais haujadiliwi..
ALITUONESHA KWA NINI ?
unawaambia watu ...jamani nimejisikia kumleta mke wangu ili tu na nyinyi mumuone ila hamruhusiwi kumjadili...
kumbe tusiosoma tuna raha..
akili zetu hazikuingizwa matope ya kikoloni.
 
Tena sasa zitakua zinakuja za upinzani halafu waanze kupata kazi ya kukanusha, watabanaa mwisho wataachia

Wapinzani wajitaiti tu kuibua hoja za nguvu, anavyozungumuza ahakikishe tu simu yake ipo on kwa kurekodi.
 
Ukisoma ibara ya 43(2) ya katiba inazungumzia mshahara wa Raisi kutuponguzwa kwa namna yoyote Raisi awapo madarakani lakini hakuna mahali katika ibara hiyo panapokatza kujadili mshahara wa Raisi.

Vile vike hata ukisoma ibara ya 43(1) ambayo nayo inaongelea mshahara wa Raisi hakuna mahali ibara hii inakataza mshahara wa Raisi kujadiliwa popote.

Swali:Mawaziri wa aina hii watatufikisha wapi?

Jamani tusikubali kupelekwapelekwa hii ni nchi yetu sote.
Safi sana mkuu
 
Mwajiriwa wa serikali ya Tanzania anayelipwa mshahara mnono zaidi Kama halipi kodi anajipotezea mamlaka ya kuwataka watanzania wenzake walipe kodi.

Kuna kiongozi wa nchi nyakatizo aligogorana na mkewe, walisuluhishwa kwa muda mrefu bila mafanikio, ikafika zamu ya padri kusuluhisha kwa maana ni kiongozi wake kiroho,
KIONGOZI:-
Padre una mke?

PADRE:-
Wewe wajua kuwa sii ruhusa kwa padre kuoa.

KIONGOZI:-
Sasa utajuaje uchungu wa mke na matatizo ya ndoa!!?

PADRE:-
Kwa kusoma BIBLIA

KIONGOZI:-
Hata na mimi biblia ninayo ndani, naisoma papoja na mke wangu na bado mgogoro umeibuka, sembuse wewe usiye na mke utajuaje migogoro ya ndoa inavyoibuka ili uwe na ladha ya kivitendo na siyo kusadikika.

HITIMISHO:-
Kiongozi akamkatalia padre kusuluhisha ndoa yake kwa kigezo hicho.

WATANZANIA SIO WATUMWA WA RAIS,
Simbachawene ajue kama mshahara wa rais haujadiliwi popote basi huo mshahara haupo, maana unapoanza kufikiri tumlipe ngapi tayari unakiuka hiyo sheria.

MAGUFULI LIPA KODI.
 
Back
Top Bottom