Siyo siri tena kuwa tangia kurejea nchini kwa mwanasiasa TAL, hali ya kisiasa nchini imebadilika kabisa.
Haipo shaka kuwa huyu ndiye mwanasiasa anayefuatiliwa zaidi kwa sasa hapa nchini na makundi yote. Humo wamo wafuasi wa chama chake na hata wafuasi wa vyama hasimu, chawa na viongozi wao bila kuwasahau watanzania wengine.
Tathmini ya kawaida mitaani na kwenye mitandao inaonyesha hivyo. Kwa hakika haihitajiki TWAWEZA kuthibitisha hilo.
Wapo ambao kwenye kujitoa kimasomaso wametaka kumkejeli na hata kutaka kukejeli kushambuliwa kwake Dodoma. Wapo ambao wana wivu kama ule wa Six, wenye hata kutamani wao wangekuwa huyu mwamba. Wapo wenye kuchukizwa na popularity yake. Wapo wenye kujidhania kuwa ni bora zaidi kwanini iwe huyu, nk nk.
Zaidi sana wapo waliomfyatulia risasi na hata wale wenye lao jambo, walioliratibu shambulizi zima kule Dodoma.
"Yapo pia mataifa hasimu yanayotuzunguka ambayo yanaweza kupenda kuukaanga mbuyu."
Kwa hakika itakuwa kujidanganya sana kudhani kuwa eti hali ni shwari bin sawia.
"TAL na CHADEMA chonde chonde, uinzi unasibu uhalisia."