Upepo kisiasa umebadilika, Lissu aongezewe ulinzi

Siyo siri tena kuwa tangia kurejea nchini kwa mwanasiasa TAL, hali ya kisiasa nchini imebadilika kabisa.

Haipo shaka kuwa huyu ndiye mwanasiasa anayefuatiliwa zaidi kwa sasa hapa nchini na makundi yote. Humo wamo wafuasi wa chama chake na hata wafuasi wa vyama hasimu, chawa na viongozi wao bila kuwasahau watanzania wengine.

Tathmini ya kawaida mitaani na kwenye mitandao inaonyesha hivyo. Kwa hakika haihitajiki TWAWEZA kuthibitisha hilo.

Wapo ambao kwenye kujitoa kimasomaso wametaka kumkejeli na hata kutaka kukejeli kushambuliwa kwake Dodoma. Wapo ambao wana wivu kama ule wa Six, wenye hata kutamani wao wangekuwa huyu mwamba. Wapo wenye kuchukizwa na popularity yake. Wapo wenye kujidhania kuwa ni bora zaidi kwanini iwe huyu, nk nk.

Zaidi sana wapo waliomfyatulia risasi na hata wale wenye lao jambo, walioliratibu shambulizi zima kule Dodoma.

"Yapo pia mataifa hasimu yanayotuzunguka ambayo yanaweza kupenda kuukaanga mbuyu."

Kwa hakika itakuwa kujidanganya sana kudhani kuwa eti hali ni shwari bin sawia.

"TAL na CHADEMA chonde chonde, uinzi unasibu uhalisia."
Ushauri tayari ushafanyiwa kazi , angalia video akiwa Dodoma leo
 
Yeye nwenyewe anatamka waziwazi kuwa aliyetaka kumwua ni JP.

Naamini hata akifa sasa hivi atakuwa kahusika JP na si mwingine.
 
Kwa sababu hizo ndiyo maana anafuatiliwa mno labda kuliko mwingine yeyote hapa nchini?

Labda ungezipitia tena sababu zako kuona kama zinaweza kumshawishi yeyote?
Anafatiliwa na nani-yeye tu ndiye ajiweka kwenye mwanga kama changudoa wa mtaa wa Ohio
 
Hakika Tundu Lissu, ndiye Nelson Mandela wa nchi hii, hivi sasa

Kupitia mateso aliyoyapata Kwa kupigwa risasi 16, mchana kweupe, bila hata mtuhumiwa hata mmoja kukamatwa Ili ahojiwe.

Huyu ndiye ninayemtabiri kuwa the next President of our country
TAL ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya bongo for now. Ana sauti kubwa. Asaidie ipatikane katiba mpya haraka ila nadhani Bado hayuko salama.
 
Back
Top Bottom