Upepo wa kisiasa nchini hausomeki, kuna nini?

Kiukweli kwa dunia ya sasa fedha ndio kila kitu na si matokeo
 
Huyu mama hana baraka zake Mungu kukalia kiti, ndiyo maana matukio yasiyo ya kawaida yanatokea
Kuna vyombo inaelekea haviko katika control yake.
Vinajiendesha with impunity na haviwajibiki kwa lolote au kwa mtu yeyote.
Kilio cha utekaji, mauaji ni cha muda sasa lakini serikali haijafanya lolote.
Huu ni mtaji tosha wa kumchafua kabisa mama.
 
Una 'kiona mbali' sana mkuu.
 
Hivi unafikiri Kinana kujiuzulu ghafla ilikuwa kawaida ?

Nahisi uchaguzi ndio unaleta shida ...tena kubwa sana
Mimi hii point ya uchaguzi hainiingii akilini sana kwa sababu siuoni upinzani wenye nguvu, nje ya chama na ndani ya chama.

Ama labda nipate ufafanuzi zaidi kutoka kwako namna hofu hiyo ya uchaguzi inavyoweza hata kuhatarisha usalama wa maisha ya watu kwa kiasi kikubwa namna hii!
 
Tumemkosa "Paskali"
 
Kuna vyombo inaelekea haviko katika control yake.
Vinajiendesha with impunity na haviwajibiki kwa lolote au kwa mtu yeyote. Kilio cha utekaji, mauaji ni cha muda sasa lakini serikali haijafanya lolote.
Huu ni mtaji tosha wa kumchafua kabisa mama.
Tatizo ni chawa ndio Wana haribu nchi yaani "Sirikali ndani" ya Sirikali .
Watu wameaacha kufuata mfumo, na hii inaonekana hata katika teuzi, hivyo nidhamu ya kazi inakuwa haipo, Bali nidhamu ya "uchawa"
Hivyo kuua nguvu za mfumo kutenda kazi zake ipasavyo.
Hii Katiba yetu inahitaji "Paskali" atumie na Busara yake ili mifumo iweze kufanya kazi nayo ni kufikiria nchi Kwanza na sio chawa Kwanza.
 
Duh...!.
P
 
Ukiwa kiongozi then huongei, hutoi maelekezo yenye msisitizo, hueleweki umesimamia wapi na unataka watu wafanye nini, hutoi warning na kuwawajibisha watu waovu, huonyeshi kuwa umekereka kutoka moyoni, hutoi mifano ya kuwawajibisha watenda maovu, huonyeshi kuwa unafuatilia mambo unayoamuru yafanyike na kikubwa husikilizi watu yaani hudeal na current issues na kusimama kwa uhodari na kufariji watu.....KAMA ni baba lazima familia ipalanganyike, kama ni MD basi meli itajiendea tu NA kikubwa watatokea watu watachukua nafasi yako, watafanya maamuzi kwa niaba yako, watavuruga then wewe tena utalaumiwa.
 
Kwa mtindo wa ati " mkalitazame hilo" as if wewe huhusiki!
 
Zunguka kote lakini mkirudi tuandike katiba mpya ndo dawa pekee iliyobaki kama tunataka kuendelea kuwa taifa Moja

Vinginevyo ni kuendelea kujlilisha upepo kuwa mambo yatajiset yenyewe

Ccm wanaamini watutumia udanganyifu utekaji, mauaji, ufisadi na ugaidi kuendelea kutawala
Lakini mbinu hizi xinaenda kushindwa

Njia pekee ya kuzuia nchi isimeguke vipande vipande ni kuleta katiba mpya yenye serikali za shirikisho
Mtake mistake


Wakati ccm wako bize kuteka na kuua wapinzani wakidhani ndo adui wa taifa je. Wamechungulia kuaona hatari ya kumeguka kwa nchi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…