Katika kipindi hiki kifupi kama miezi mitatu hadi sita, upepo wa kisiasa hausomeki. Matukio tunayoyaona mengine si tu siyo ya Kitanzania lakini yanakinzana na hata mila, utamaduni, umoja wetu kitaifa na hata imani yetu.
Mengine ni aibu hata kuyasema maana ni laana kwa Taifa letu. Viongozi kwa sana wako kimya, kimya kizito. Kuna nini?
- Watoto wadogo wanabakwa na kulawitiwa.
- Watu wanauwawa kama majuzi Mohammed Kibao wa Tanga.
- Watu wanatekwa na kutupwa maporini
Wakati huo huo mikeka ya teuzi na tengua ni kila baada ya mwezi mmoja. Sasa inaelekea gundi inayotuunganisha Watanzania inazidi kuwa nyepesi.
Mwalimu alisema ili tuendelee, tunahitaji vitu vinne; Watu, Ardhi, Siasa safi na Uongozi bora!
Tunakosea wapi?