Upepo wa yanga kufanya vibaya kwa sasa ndio nafuu ya simba kutoonekana madhaifu yake lakini timu yao ni dhaifu na kocha wao ni dhaifu pia!

Upepo wa yanga kufanya vibaya kwa sasa ndio nafuu ya simba kutoonekana madhaifu yake lakini timu yao ni dhaifu na kocha wao ni dhaifu pia!

Makavuli

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2024
Posts
1,425
Reaction score
1,829
Huu upepo wa yanga kufanya vibaya kwa sasa ndio imekuwa nafuu kubwa kwa timu ya Simba kutotazamwa na watu wengi madhaifu yao pamoja na kocha wao!
Kwa sasa wachambuzi na mashabiki wengi wa soka wamejikita kuijadili yanga kwa hali wanayopitia kitu ambacho kimewafanya viongozi wa Simba na kocha wao kutofatiliwa sana na kutuliza presha ya mashabiki wao lakini timu yao Ina matatizo luluki!
Kuanzia kwa kocha wao pale akuna kocha kimbinu ni mweupe sana na sishangai alipoishusha timu daraja kule afrika kusini na kufukuzwa!
Kwa sasa timu aieleweki inacheza mfumo Gani na wanataka nini,,tokea apewe timu Kila siku yeye anajificha kwenye kichaka cha kujenga timu!
Angalia sub zake anazofanya unaweza ukadhani ajawajua wachezaji mpaka sasa wakati anao mda mrefu tu na alisajili yeye!
Ukirudi kwenye performance ya timu Kila mwenye kuujua Mpira atakubaliana na Mimi Wala siitaji kueleza zaidi,,rejea mechi 6 zilizopita utapata majibu!
Aina yao ya usajili walisajili wachezaji wa kucheza ligi ya ndani na sio kimataifa,,Kuna wachezaji kama 2 ama watatu unaoweza kusema wako tiyali kucheza kimataifa ambao ni Camara, che mallon na kidogo Debora!
Uwezi kwenda michuano mikubwa unategemea ahou ama kina barua,,
Unaenda kimataifa unamtegemea mutale na wakina charabou!
Yanga hii siku ikiamka na kuanza kufanya vizuri hapo ndipo mtafutano utaanza pale msimbazi na kocha atafukuzwa kwa makubaliano ya pande mbili!
Kwa sasa awawezi kwakuwa topic iliyopo ni yanga ndio kichaka kwa sasa inawasaidia kutuliza hali ya hewa lakini mda ulifika yule aliyelala akiamka Kuna bakora zitatembea na mangungu ajiandae kisaikolojia!
Uwezo wa kikosi cha Simba umeishia hapo akuna cha ziada wanaweza kutoa na uwezo wa kocha umeishia hapo pia ndio maana Kila akihojiwa anakimbilia kwenye hoja ya kujenga timu na anakwambia vijana bado Awana uzoefu sasa sijui wakati anasajili akuwaona wachezaji Wenye uzoefu? Awezi kusema alisajiliwa kikosi kwakuwa alishakiri kwamba alishirikishwa Kila hatua kwenye usajili na aliwakubali!
Angalia mechi walizoshinda kwa penalty na sio build up ya kuona kwamba timu inatengeneza nafasi kufunga goli,,mechi dhidi ya pamba, Dodoma Jiji,bravos, na penalty nyingine zilikuwa za kuzawadiwa na marefa!
Kwa maana iyo Simba ni dhaifu sana upepo wa yanga kufanya vibaya ndio unaowabeba kwa sasa!
 
Tatizo la hizi timu za kariakoo viongozi wao wanajifanya kujua Mpira kuliko makocha Waliowaajiri.
Hersi akijua kupiga danadana na ku control Mpira na kupiga chenga basi anajiona anafaa kufundisha Hata Real Madrid .
Ukimuuliza kosa la gamondi mpaka akamfukuza ni nini Hana jibu Bali ni majungu ya Kiswahili .
Kufuatlia Mpira wa Tanzania ni matatizo tu.
 
Uwezi kumlaumu kwa kumuondoa gamond,,wewe unadhani gamond aliondolewa sababu ya matokeo? Suala la gamond alipaswa aondolewe mapema kutokana na sababu nyingine ambazo sio Kila mwajiri aweke wazi Siri za mwajiriwa wake mambo mengine ni private issue ili kulinda heshima yake,,suala la matokeo lilikuwa ni nyongeza tu ya kuchochea moto kwenye petroli!
 
Walikaa nae chini kutatua matatizo?
Wanasema Ana utovu wa nidhamu kwa kugombana na marefa je wameshamwona mourinho au klopp au anchelotti au Alex Ferguson?
 
Sio Upepo, hili neno ulilolitumia Upepo linawadanganya Kwa Yanga hii Shida ni 'MEMKWA'..
 
images (3).jpeg
 
BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE ALITUTAJIA MAADUI.

1. UMASIKINI
2.UJINGA.
3. MARADHI.

Akasema Hawa ni maadui wa kweli kweli katika hili Taifa.

LEO 2024 BAADA YA MIAKA 60 TUMEKUWA NA MAADUI WENGI ZAIDI.

2024 maadui wameongeseka Zaidi kuliko wale watatu wa 1961.

1.Umasikini na ufukara.
2.Ujinga na upumbavu.
3.Magonjwa na Maradhi.

4.Mmomonyoko wa Maadili.
ushoga, usagaji Kamali, sugar mamy, sugar Dady mashangazi
AJIRA.
5. Rushwa na Upendelo

6. USimba na u yanga.
7. Mitandao ya kijamii Tiktok, x, nk
8. Manabii wa uongo na Mashehe Uchwara.
9. Ajali nyingi mno.
10. Gharama kubwa za maisha, ujenzi holela nk

MAMBO NI MENGI SANA VIJANA WA KITANZANIA WANAWAZA MAMBO YA HOVYO SANA SIMBA NA YANGA ZINATAWALA MIKEKA NK.

OKOENI TAIFA LENU LEO.

IPO SIKU HILI TAIFA LITAZIDIWA NA SOMALIA KIUCHUMI.

MKIFIKA MBINGUNI MTAHOJIWA NA MUNGU MLILIFANYIA NINI TAIFA LENU NIMEMALIZA.
 
Back
Top Bottom