zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Sasa hiyo USS eldridge kutokana na vita kuchachamaa kipindi hicho wamarekani wakawa wanatafuta silaha za kila aina kummaliza adui sasa wanadai kabla mbinu hii haijatumika vitani ilibidi ifanyiwe majaribio ndani kwa ndani ndio yakafanyika majaribio haya mawili
La kwanza lilikuwa july 1943 ambapo meli hiyo hiyo USS Eldridge iliweza kufanywa majaribio ya kisayansi na isionekane kwa macho... kwa ufupi ikayayushwa!! (Wavuvi waliona meli ikitoweka ikabaki moshi wa kijani tu )
Sasa walipoona wamefanikiwa kufanya meli iyayuke/isionekane ili adui asiione kwenye uwanja wa vita wakajaribu kufanya majaribio ya kuiteleport kwa kuihamisha kutoka eneo A kwenda eneo B kwa kutumia hizo sheria za kisayansi za QUANTUM TELEPORTATION (unified field theories) zilizoimarishwa na Albert Einstein
Kuendana na maelezo ya morris jessup mtu aliyeiibua SIRI hii na kuuawa miaka michache baadae meli hiyo ilitoweka kweli kutoka philadelphia na baada ya sekunde chache ikatokea upande wa New york yaani meli iyayuke pale bandari Dar alafu ionekane mpendae huko pemba sekunde chache baadae!!!!
Mwandishi anasema licha ya jaribio hili kufanikiwa ila wanajeshi waliokuwepo kwenye meli wengi walipata madhara mfano kuna watu walikutwa wamebanwa katikati ya vyuma.... Wengine wamekufa, wengine meli ilipoyeyuka hawakurudi, wengine waliopona walirukwa na akili na baadae wengi wao kufa vifo vya kiutatanishi (inasemekana walifuatiliwa na kuuawa ili wasitoe siri)
Story hii ilivuja kupitia mmoja wa wanajeshi aliyeitwa miguel ailende aliepona kwenye tukio hilo ambaye kabla naye hajasakwa alitoa siri zote alizoziona kwenye meli kwa mwandishi huyu morris Jessup ambaye naye kwa kuandika makala hii na kutoa kitabu aliishia kufa kifo cha kutatanisha!!!
Sasa nimeleta kisa hiki kwa wana JF ili wajuvi wa mambo mtusaidie je upi ni ukweli kuhusu the philadelphia experiment??
Je tukio hili ni la kweli au limeongezwa chumvi na wamarekani ili waoagopeke??
Je kweli waliweza kuiteleport meli??
Je huenda bado wanayo hyo teknolojia au waliachana nayo baada ya kufeli vibaya??
Je kama teknolojia hiyo ikiwepo sahvi itabadilishaje mambo kwenye uwanja wa kivita??
NB: Teleportation sio jambo la kufikirika linawezekana sema kwa vitu vidogo na iko proven na wanasayansi kuwa unaweza ukakihamisha kitu dar ukakifikisha morogoro bila kusafirisha physically.... Na wanasayansi wa japan wameweza kuteleport element chache kutoka ardhini zikatokea upya huko kwenye satellite yao angani!!
Naomba kuwasilisha
CC Malcom Lumumba Elungata Kiranga hearly Mshana Jr Habibu B. Anga Palantir Da'Vinci Kudo900 Kipanga boy izzo Eiyer Ziroseventytwo na wanajukwaa wote
NB: uzi niliupost JF intelligence ila baada ya mods kuushikilia kwa "miaka" kadhaa nimeona nikubali yaishe niulete huku jukwaa pendwa