Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mara baada ya kupiga Kura, Dkt. Stergomena Tax, amesema ameridhishwa na hali iliyopo kituoni hapo ambapo alisema “Natoa wito kwa Wananchi wenzangu kufika kwenye Vituo vilivyoandaliwa ili waweze kupiga Kura na kutumia haki yetu ya kikatiba na kuwachagua viongozi ambao tunaona tumeridhika nao.”
Naye Mkuu wa Wilaya Magu, Joshua Nasari amewahakikishia Wananchi Usalama katika vituo vyote wilayani hapo.
Naye Afisa Msimamizi Kata ya Itumbili, Bi. Lina Amata ameeleza kuwa, zoezi la upigaji kura limeenda vizuri na hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza.