Uchaguzi 2020 Upinzani kujitoa kushiriki Uchaguzi Mkuu 2020 siyo uoga wala ujinga, kitakuwa ni kitendo cha ushujaa na uzalendo

Uchaguzi 2020 Upinzani kujitoa kushiriki Uchaguzi Mkuu 2020 siyo uoga wala ujinga, kitakuwa ni kitendo cha ushujaa na uzalendo

Sawa kabisa!
Vyama vikuu vingeungana na kuhamasisha ya kudai tume huru ya uchaguzi, this is the right time kufanya hivyo wasusie uchaguzi na wadai tume huru basi. Watu wengi watawaunga mkono hata mimi nitaunga mkono na huo utakuwa mwisho wa udhalimu huu. Hakika JK na Ben walitukosea sana sisi Watz.
 
Wapinzani wetu nao wanataka vyeo hata kwa njia haramu. Hapo ndipo tutasubiri sana kuleta mabadiliko ya kweli
Kwa hili uko sahihi kabisa, maandalizi ya uchaguzi mwingine mpya huanza rasmi baada ya kumalizika uchaguzi uliopo kwa wakati huo.

Ila kumbuka toka mwaka 2015 walizuiliwa kufanya shughuli za kisiasa hasa kukuza na kuimarisha vyama vyao kupitia mikutano ya hadhara kwa kisingizio kwamba "muda wa siasa umekwisha sasa ni muda wa kunyoosha nchi" ila chama tawala (Ccm) wao hawakuhusika na hilo katazo hivyo waliendelea kufanya siasa kwa miaka yote mitano mfululizo.
 
Kwa huzuni sana, lengo la CCM ni kuwafanya wapinzani wakuu hao wasusie uchaguzi. Ndio lengo kuu maana kina lipumba watabaki na itahesabika vyama 14 vimeshiriki uchaguzi.
 
Niseme ukweli, japo mchungu, kuwa upinzani tulionao hauwezi kujitoa maana wapinzani wengi nao wanapigania vyeo si mabadiliko. Wanasema siasa inalipa! Wako tayari kushiriki uchaguzi wanaouita uchafuzi, batili na haramu ilimradi waambulie udiwani, ubunge na kura za urais za kuongezea ruzuku za vyama vyao. Wengi (si wote) wanagombea maslahi yao binafsi, si maslahi ya umma!

Mara kadhaa nimewahi kuwashauri kwamba tupiganie tume huru kwanza, katiba mpya kwanza, wagombea huru kwanza na mifumo mingine mipya kwanza ndiposa tuingie kwenye uchaguzi, lakini wapi. Ni dhahiri kuwa bila uwanja sawa wa kisiasa, bila kuwa na refa (tume huru) asiyeegemea upande wowote ni kushiriki kwa hiari uchafuzi, ubatili na uharamu. Wasilalamike!

Kenya na Malawi walimwengua rais aliyepitishwa na tume za upendeleo kwasababu walibadili mifumo ya uchaguzi na kuruhusu matokeo kuhojiwa mahakamani. Lakini wapinzani wetu wanataka vyeo kwanza na marupurupu yake!

Nawaomba baada ya uchaguzi wakae kimya, wasilalamikie dosari zozote zitakazojitokeza, maana wamekubali kushiriki uchaguzi chini ya tume na mifumo mingine wanayodai batili na haramu. Ukikubali kushiriki kula chakula unachojua kina sumu na haramu, usilalamike utakapoanza kuharisha!
 
Niseme ukweli, japo mchungu, kuwa upinzani tulionao hauwezi kujitoa maana wapinzani wengi nao wanapigania vyeo si mabadiliko. Wanasema siasa inalipa! Wako tayari kushiriki uchaguzi wanaouita uchafuzi, batili na haramu ilimradi waambulie udiwani, ubunge na kura za urais za kuongezea ruzuku za vyama vyao. Wengi (si wote) wanagombea maslahi yao binafsi, si maslahi ya umma!..
Usiwapotoshe mkuu, itakula kwao chief
 
Nasema itakuwa ni ushujaa na kutanguliza maslahi ya taifa, itakuwa ni njia pekee sahihi na muafaka ya kuonesha kutokubaliana na uchaguzi huu batili uliojaa hila, fitina na nia ovu.
Too late, halafu itawagharimu sana. Na itakuwa salama kwa nchi maana vyama vingine ndiyo hivyo vimekuwa na makando makando yakuwa na mkono wa beberu nyuma yake.
 
Nafikiri mngechukua njia ingine ya kumshauri na kupunguza yale mlokuwa mwazungumza dhidi yake majukwaani nina imani kungekuwa na suluhu.

Ndo maana akaamua kama hali itakuwa hivyo basi hakuna siasa...
Ndio ni maoni yako, lakini ni ya kishoga!.
 
Nasema itakuwa ni ushujaa na kutanguliza maslahi ya taifa, itakuwa ni njia pekee sahihi na muafaka ya kuonesha kutokubaliana na uchaguzi huu batili uliojaa hila, fitina na nia ovu.

Kama tume itakataa kuwarudisha wagombea ubunge zaidi ya 150 wa upinzani hususani ACT na CHADEMA waliowaengua kwa sababu moja ama nyingine basi upinzani ukubali tu kuwa kujitoa kushiriki uchaguzi ndiyo njia pekee sahihi na muafaka.
Sasa mtu anafika bei unakuja kulete propaganda huku.watu wameshaakuwa wajesiriamali wanaachia nafasi kwa kisingezio mara hoo nimeenguliwa
 
Nafikiri mngechukua njia ingine ya kumshauri na kupunguza yale mlokuwa mwazungumza dhidi yake majukwaani nina imani kungekuwa na suluhu.

Ndo maana akaamua kama hali itakuwa hivyo basi hakuna siasa.

Na alisema kabisa kwamba chini ya utawala wake asingependa kuona watu wanaingilia juhudi zake.

Wapinzani mkubali mmekosa mbinu nzuri ambazo twaita kwa kiingereza Constructive ideas and strategies.

Hizi zinajenga na sio kubomoa urafiki na maridhiano.

Nasisitiza, haya ni maoni yangu.
Sasa hicho ni nini? Constructive ideas anazokubali jiwe ni kusifu na kuabudu tu, hujaunga mkono juhudi no matter lugha gani umetumia utashughulikiwa.

Umesahau figisu walizofanyiwa KKKT baada ya ule waraka wao? Wakaambiwa hawajasajili katiba etc. Ule waraka ulikuwa siyo constructive?
 
Back
Top Bottom