Tetesi: Upinzani kusambaratika tena 2020

kwani dr Slaa alipoondoka cdm alileta athari gani mkuu mbona mambo yaliendelea...kwa ufupi watu hawana hamu na ccm kwahiyo hata hyo kijana wako unayemficha hataweza kuleta athari yeyote.
 
Tz mpinzani wa kweli alikuwa kambona makaidi babu, tumbo waliobaki ni wapinzani uchwara
 
Umesema wewe sio Mimi!!

Nimecheka sana....tehtehteh....umenifurahisha kwa jibu lako....ila jibu lingenoga zaidi kama ungeandika 'wewe wasema' au 'wewe wanena'...tehtehtehteh
 
hivi kwa akili yako ndogo kati ya CCM na ukawa nani wapo imara yule jamaa uchwara kawakata pumzi CCM mpaka wenyewe ndani kwa ndani wanashindwa kupumua.

Hivi unashindwa nini kujibu kwa uungwana??!! kwani ni lazima uandike 'jamaa uchwara'???...Hivi unadhani au unafikiri watu wazima na akili zao hawajui unamananisha nini kwa kuandika hivyo??? Kwanini watu wengine hamjipendi??? Kwanini ujiweke katika orodha ya 'kufuatiliwa' kwa jambo ambalo ungelikwepa????
 
Intelligence yetu inajua kila kitu, sisi CHADEMA ni zaidi ya ist Kwa hiyo msihofu upinzani hautakufa.
 
mkuu umeanza lini kua mpiga ramli chonganishi
 
CCM hawana ujanja zaidi ya kutumia rafu ambazo wanachezeana hata wenyewe kwa wenyewe,kwa kuwa wapinzani wamekomaa kwa rafu wanazochezewa na CCM,hata wakimtumia malaika aliyeko ndani ya wapinzani,wapinzani bado watashinda tu,Kama CCM waliweza kumtumia Lipumba na Slaa ambao kwa kipindi fulani walishawahi kuwatoa CCM makamasi,zaidi ya hao ni nani mpinzani wa kweli ambaye ana weza akatumiwa na CCM mpaka akafanikiwa kuusambaratisha upinzani?,Kama majabari hao wakiwemo akina Zitto,Rashid wa CUF walitumiwa na CCM kuuvuruga upinzani na bado walilambishwa Mchanga.
 
Kwani 2015 Upinzani ulisambaratika? pamoja na Dr lipumba kuondoka,na Dr Slaa kujiengua bado upinzani ulibaki imara ingawa vingozi wakuu hawakutafuta maoni ya wanachama.
 
Kweli gari la zamani matairi yana vipara..hakuna maarufu zaidi ya chama anatoka mtu anaingia mtu/watu
 
yaani vyama vi4 vimepigwa knock out na magu. eti wakampokea mamvi, waliuziwa yai viza mchana mchana
 
Mbona mlisema utasambaratika baada ya uchaguzi?nimeamini kila watanzania 4 mmoja in kichaa
 
Huwa sikuelewi wewe technically,mara kadhaa umeonesha kuishabikia ukawa katika bandiko zako na mara nyingine unatetea cchama cha kijani.naomba uweke wazi upande uliopo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…