Upinzani kushiriki uchaguzi wowote ule chini ya Tume hii ya Uchaguzi ni uwendawazimu

Upinzani kushiriki uchaguzi wowote ule chini ya Tume hii ya Uchaguzi ni uwendawazimu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Wendawazimu huwa wana kawaida moja!. Kurudia kitu kile kile kwa mtindo uleule wakitegemea matokeo tofauti.

Itakuwa ni ajabu sana kwa vyama vya upinzani kushiriki uchaguzi wowote kuanzia sasa na hata uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 chini ya tume hii ya uchaguzi.

Wahenga walisema kenge huwa halisikii mpaka damu ilitoke masikioni na mdomoni ndo ajue kuwa sasa hapa mambo si shwari.

Nimeshangaa kuona kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akisifu kwenye tweet yake namna mgombea wa chama chake huko Kigoma kwenye jimbo lililowazi la Dr Mpango kuwa nchi imerudi around 2012 ambapo tume ilikuwa fair.

Asichokielewa Zitto ni kuwa kwa sasa tume inataka kujikosha baada ya udhalimu wa kutisha iliyoufanya kupora haki ya uchaguzi ya wananchi mwaka 2020

Kitu kingine ni kuwa sasa hivi CCM hawana cha kupoteza, na wanatafuta legitimacy kwa wananchi kwa angalau kuongeza idadi ya wapinzani bungeni, maana hili bunge la sasa bado lina sura ya chama kimoja, wapinzani 19 walioingia mle wameingizwa kwa kuvunja sheria , kiufupi ni bunge ambalo lipo pale huku kukiwa na uvunjifu mkubwa wa sheria ambazo bunge hilohilo ndilo lililozitunga!

Hivi ukiwa mpinzania, Utashirikije uchaguzi chini ya tume ambayo ilifanya yafuatayo mwaka 2020 kuisaidia CCM

1. Kuengua wapinzani bila sababu za msingi
2. Kubania rufaa za wapinzani mpaka siku chache tu kabla ya uchaguzi ili wasidante kampeni?
3. Kushindwa kuzuia uovu wa kukataa kuapishwa mawakala wa vyama vya upinzani na hara walioapishwa kuzuiwa kyingia katika vituo vya uchaguzi?
4. Kushindwa kuchukua hatua kwa vitendo vya kuingiza kura feki vituoni
5. Kufumbia macho na kushiriki uvurugaji wa ratiba ya kampeni ya wagombea wa upinzani
6. Uwepo wa viashiria vya matokeo yaliyopikwa waziwazi
7. Hata upangaji wa majina ya vyama kwenye karatasi ya kupiga kura uliiprendelea CCM, utaratibu uliozoeleka ni kuweka majina ya vyama vya wagombea kwa kufuata "alphabetical order", lakini mwaka 2020 kanuni hiyo ikapindishwa kwenye nafasi ya uraisi na kuiweka CCM na wagombea wake waiwa wa kwanza kwenye karatasi
8. Mlimsikia Mkurugenzi wa NEC, Dr Mahera akiponda ajenda za uchaguzi za vyama vya upinzani huku akipigia chapuo kijanja" positions" za CCM

Katika mszibgira haya, kuna busara gani kwa vyama vya upinzani kushiriki chaguzi chini ya Tume ya aina hii!

Huu ni wakati wa vyama vya upinzani kuungana na kuongoza juhudi za wananchi Kudai Tume huru ya Uchaguzi na katiba mpya. Hivyo vitu viwili ndo vinabeba future ya Upinzani na Usitawi wa nchi hii na wala siyo mafanikio ya muda mfupi kama hizi chaguzi ndogo!

CCM ni wajanha, wako tayari kuwaachia waoinzani washinde hizi chaguzi ndogo zote zitakazofuata ili kuhalalisha haramu yao ya mwaka 2020, na ili kupunguza kelele za kutaka tume huru na katiba mpya

Upinzani uwe Smart, usiwape CCM nafasi hiyo!

TAZAMA VIDEO HIZI JINSI UCHAGUZI ULIVYOVURUGWA
1.


2.


3.



4.



5.



6.
 
Tatizo ni upinzani wenyewe hasa chedema
Mbona hawana muafaka wa wale 19 wabunge
Sisi tunamwamini Madam President acha nchi isonge
 
Upinzani wanatuchelewesha sana siye wananchi...!!
 
Tatizo la upinzani kila chama kina vision yake, ndio maana wakati mwingine hashiriki ili kurekebisha kasoro zinazojitokeza kila wakati wa uchaguzi, wengine wanashiriki wajaribu bahati yao, wanaviziana wao kwa wao, hii inasababishwa na tamaa ya madaraka ( kuongoza kambi rasmi ya upinzani bungeni).

Napata shaka pia wanapoungana wakati wa uchaguzi mkuu, kwa hii tabia wayoonesha ACT sasa hivi inaonesha wazi hujiunga na wenzao ili kuwatumia kama ngazi kufikia pale wanapopataka, lakini huwa hawana nia ya dhati ya kuungana na wenzao ili kufikia malengo ya pamoja wanayojiwekea, kwa mtindo huu CCM itatawala sana.
 
Zitto hajawahi kuwa mpinzani ndiyo wale wale kina Kitila na Katambi...ni wa kuchunga sana huyu jamaa tunapokusanya nguvu zetu watanzania kudai Tume huru na Katiba mpya mwezetu ni tumbo kwanza.
 
Marehemu alishindwa vibaya mno kusimamia haki kama katiba na sheria zinavyotamka!

Nafikiri atakuwa kaweka record Africa ya utawala usiofuata haki na usawa!!
 
Marehemu alishindwa vibaya mno kusimamia haki kama katiba na sheria zinavyotamka!!
Nafikiri atakuwa kaweka record Africa ya utawala usiofuata haki na usawa!!
Yule mtu alikuwa aibu yetu sote. Alikuwa muongo, mkatili, muonevu, mkurupukaji, kiufupi vetting ilifeli sana pale
 
Marehemu alishindwa vibaya mno kusimamia haki kama katiba na sheria zinavyotamka!!
Nafikiri atakuwa kaweka record Africa ya utawala usiofuata haki na usawa!!
Kafa sasa! Nendeni mkachukue jimbo la muhambwe sasa!

Bavicha mna shida sana aisee
 
Yule mtu alikuwa aibu yetu sote. Alikuwa muongo, mkatili, muonevu, mkurupukaji, kiufupi vetting ilifeli sana pale
Kaondoka sasa! Nendeni mkachukue jimbo la muhambwe!

Kwa mentality hizi mtaishia kuitwa wapinzani hadi mnakufa.

Na nyie ni wapumbavu sababu hamjui shida iko wapi.

Magufuli kashajifia na kama shida alikuwa Magufuli nendeni mkagombee muhambwe mchukue jimbo.
 
Jimbo la nini; watanzania kwa sasa wanataka Tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya!! Hayo ma uchaguzi si agenda yao kwa sasa!!
Si msema Jiwe alikuwa ndio tatizo ndio sababu ya kufeli kwenu na yule belgji?

Ndio huyo sasa kafa nendeni mkabebe jimbo la muhambwe kwa kuanzia kisha muwaoneshe dunia kwamba jiwe akikuwa kikwazo sana katka harakati zenu.

Mimi ntaendelea kuwaita wapumbavu maana hamjui mnataka nini.
 
Jimbo la nini; watanzania kwa sasa wanataka Tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya!! Hayo ma uchaguzi si agenda yao kwa sasa!!
Unataka uletewe kama sadaka?

Wabongo kama Wacongo kabisa.

Bolingo nangai bolingo nangai huku tunapenda vitu vizuri ila hatuko tayari kuvitafuta. Tunataka tupewe kwenye sahani.
 
Wendawazimu huwa wana kawaida moja!. Kurudia kitu kile kile kwa mtindo uleule wakitegemea matokeo tofauti.

Itakuwa ni ajabu sana kwa vyama vya upinzani kushiriki uchaguzi wowote kuanzia sasa na hata uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 chini ya tume hii ya uchaguzi...
Hivi tume hii si ndiyo ilikuwepo kabla ya uchaguzi ule wa 2020? Basi tumekuwa wendawazimu muda mrefu loh!!
 
Wendawazimu huwa wana kawaida moja!. Kurudia kitu kile kile kwa mtindo uleule wakitegemea matokeo tofauti.

Itakuwa ni ajabu sana kwa vyama vya upinzani kushiriki uchaguzi wowote kuanzia sasa na hata uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 chini ya tume hii ya uchaguzi...
zito ni mwanasiasa makini sana kama ukiona anaingia kwenye uchaguzi manake Tume imetenda haki na inaendesha uchaguzi kwa weledi kama si hivyo basi asingeshiriki lakini kama chama cha siasa haitashiriki uchaguzi itakua inafanya nini hasa?

Mimi naamini Zito ana akili kuliko wewe uliepost hii hoja yako dhaifu, zito anajua mengi kuliko wewe lengo la chama chochote cha siasa ni kushika madaraka sasa nafasi ya kushika madaraka inajitokeza halafu mnasusa kushiriki bila hoja za msingi.

Tuwaache wapinzani wanaotaka kutupa karata zao kwenye uchaguzi wafanye hivyo tusiwakatishe tamaa.
 
Hakika ulichokiandika kinaonesha namna gani wewe na wasusia Uchaguzi wenzako ni wendawazimu. Hivi Chadema inamaana hamumtambui hata Mbunge wenu wa Nkasi ambaye ametokana na usimamizi wa Tume hiyo hiyo.
 
Back
Top Bottom