Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Wendawazimu huwa wana kawaida moja!. Kurudia kitu kile kile kwa mtindo uleule wakitegemea matokeo tofauti.
Itakuwa ni ajabu sana kwa vyama vya upinzani kushiriki uchaguzi wowote kuanzia sasa na hata uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 chini ya tume hii ya uchaguzi.
Wahenga walisema kenge huwa halisikii mpaka damu ilitoke masikioni na mdomoni ndo ajue kuwa sasa hapa mambo si shwari.
Nimeshangaa kuona kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akisifu kwenye tweet yake namna mgombea wa chama chake huko Kigoma kwenye jimbo lililowazi la Dr Mpango kuwa nchi imerudi around 2012 ambapo tume ilikuwa fair.
Asichokielewa Zitto ni kuwa kwa sasa tume inataka kujikosha baada ya udhalimu wa kutisha iliyoufanya kupora haki ya uchaguzi ya wananchi mwaka 2020
Kitu kingine ni kuwa sasa hivi CCM hawana cha kupoteza, na wanatafuta legitimacy kwa wananchi kwa angalau kuongeza idadi ya wapinzani bungeni, maana hili bunge la sasa bado lina sura ya chama kimoja, wapinzani 19 walioingia mle wameingizwa kwa kuvunja sheria , kiufupi ni bunge ambalo lipo pale huku kukiwa na uvunjifu mkubwa wa sheria ambazo bunge hilohilo ndilo lililozitunga!
Hivi ukiwa mpinzania, Utashirikije uchaguzi chini ya tume ambayo ilifanya yafuatayo mwaka 2020 kuisaidia CCM
1. Kuengua wapinzani bila sababu za msingi
2. Kubania rufaa za wapinzani mpaka siku chache tu kabla ya uchaguzi ili wasidante kampeni?
3. Kushindwa kuzuia uovu wa kukataa kuapishwa mawakala wa vyama vya upinzani na hara walioapishwa kuzuiwa kyingia katika vituo vya uchaguzi?
4. Kushindwa kuchukua hatua kwa vitendo vya kuingiza kura feki vituoni
5. Kufumbia macho na kushiriki uvurugaji wa ratiba ya kampeni ya wagombea wa upinzani
6. Uwepo wa viashiria vya matokeo yaliyopikwa waziwazi
7. Hata upangaji wa majina ya vyama kwenye karatasi ya kupiga kura uliiprendelea CCM, utaratibu uliozoeleka ni kuweka majina ya vyama vya wagombea kwa kufuata "alphabetical order", lakini mwaka 2020 kanuni hiyo ikapindishwa kwenye nafasi ya uraisi na kuiweka CCM na wagombea wake waiwa wa kwanza kwenye karatasi
8. Mlimsikia Mkurugenzi wa NEC, Dr Mahera akiponda ajenda za uchaguzi za vyama vya upinzani huku akipigia chapuo kijanja" positions" za CCM
Katika mszibgira haya, kuna busara gani kwa vyama vya upinzani kushiriki chaguzi chini ya Tume ya aina hii!
Huu ni wakati wa vyama vya upinzani kuungana na kuongoza juhudi za wananchi Kudai Tume huru ya Uchaguzi na katiba mpya. Hivyo vitu viwili ndo vinabeba future ya Upinzani na Usitawi wa nchi hii na wala siyo mafanikio ya muda mfupi kama hizi chaguzi ndogo!
CCM ni wajanha, wako tayari kuwaachia waoinzani washinde hizi chaguzi ndogo zote zitakazofuata ili kuhalalisha haramu yao ya mwaka 2020, na ili kupunguza kelele za kutaka tume huru na katiba mpya
Upinzani uwe Smart, usiwape CCM nafasi hiyo!
TAZAMA VIDEO HIZI JINSI UCHAGUZI ULIVYOVURUGWA
1.
2.
3.
4.
5.
6.