Upinzani kwa Tanzania ni kazi ngumu na ya hatari

Upinzani kwa Tanzania ni kazi ngumu na ya hatari

kamjabari

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2017
Posts
1,144
Reaction score
1,668
Ukisha kuwa na fikra mbadala nchini mwetu basi utachukiwa sana na wakalia kiti cha enzi na vibaraka wao.

Utafanyiwa fitina, manyanyaso, dhihaka na ubaya wa kila aina ndiyo maana kila mtawala wa CCM akingia madalakani chakwanza huanza ku-dill na Wapinzani.

Ona sasa Hoja ya KATIBA MPYA iliyo ibuliwa na kutetewa na Wapinzani inavyo pigwa rungu, CCM hawataki kabisa habari hii maana wana amini itawatoa kwenye himaya.

Lakini umuhimu wa katiba mpya wanaujua vyema Ila wanapotosha watu ,na vibaraka wao wana fwatiliza na kupiga mbiu hiyo hiyo kwa masilahi yao binafsi ya watu wasio zidi hata Mia moja nchi yenye watu zaidi ya milioni sitini (60 million).

Sasa tuna ona na ACT nao wame wasaliti Wapinzani na wananchi wenzao na kukomaa na tume huru ya uchaguzi kwamba eti ndio kipao mbele ili hali katiba inayo weza kusimamia tume ya uchaguzi na taasisi zote nchini waki iweka nyuma.

Tuseme ACT lao moja na CCM Ila imejificha kwenye gamba Kama Kobe?

#Kamjabari
 
Tume huru ya uchaguzi bila katiba mpya ni sawa na kuziba mashimo ya panya kwa mikate!

Maana Tanzania uchaguzi ni mfumo sio tume tu.Nguvu ya Rais na wateule wake, polisi, TISS, Jeshi, Tume, Tamisemi na wengineo lazima viangaliwe kwa pamoja kupitia katiba mpya kwa kuwa vinahusika na uchaguzi mkuu.

Sasa bila katiba mpya hawa TISS,Polisi,Jeshi,wakurugenzi wa halmashauri na kadhalika ambao pia huusika na chaguzi watadhibitiwa vipi?

Hiki kinachoitwa kuwa ni Tume huru ya uchaguzi ni changa la macho kwa wajinga ambao ndiyo wengi kwenye hii nchi.

ACT wazalendo ni tawi la kijasusi la CCM ambalo CCM hulitumia kuvuruga vyama vya siasa hapa nchini ili kitimiza nia zao ovu.
 
Upo sahihi mkuu ,na ndiyo maana wengine tunamshangaa Zitto na ACT kupambania kitu ambacho wanajua wazi ni hadithi za abunuasi.
 
Ni Kweli Upinzani ni Kazi ngumu Sio TZ bali Ulimwenguni Kote....! Mifano ipo. Nelson Mandela alikaa jela 27 years.
Lakini hapa Kwetu Tumeshindwa kuunda upinzani Wa Kweli.
Fikiria Uchaguzi 2015, Wapinzani wote Chini Ya Ukawa Wakamkabidhi kijiti Lowasa..Lowasa ambaye walitumia muda Wao wote Kumnanga kabla..!
Ukitafakari Utaona hawa Waliopo ni Wapigaji na Vikundi vilivyopo vimekaa Kimaslahi.
 
Upo sahihi mkuu ,na ndiyo maana wengine tunamshangaa Zitto na ACT kupambania kitu ambacho wanajua wazi ni hadithi za abunuasi.
ACT wazalendo ni tawi la kijasusi la CCM la kuua vyama vya upinzani ili kufanikisha hila pamoja na maovu yao.
 
Ukitaka kujua upinzani si lelemama waulize wakongwe waliotoka CCM kwa mbwembwe na matarumbeta kwenda CDM yaliyowakuta...

Mwaka tu wakaomba poo warudi CCM..
Bwashee kuna wengine walijaribu kugombea uenyekiti wa chama wakaambiwa sumu haionjwi kwa ulimi. Ulitegemea wafanyeje?
 
Bwashee kuna wengine walijaribu kugombea uenyekiti wa chama wakaambiwa sumu haionjwi kwa ulimi. Ulitegemea wafanyeje?
Upinzani hakuna fursa za pesa nje nje za kifisadi , so mtu aliye zoea ccm ni vigumu kudumu upinzani .

Hayo mengine ya propaganda za ccm kuhusu madalaka, ni mbwembwe tu za ccm kuwa hadaa wananchi. Hivi mtu anatoka nje ya nchi Leo anaomba uraia Kisha maramoja anaomba nafasi ya ju kabisa ya uongozi na tunajua historia yake aliko toka utafanyaje?
 
Wa kulaumiwa ni Nyerere. Yeye kabla ya nchi kupata uhuru alikataa upinzani. Alitaka asisumbuliwe akijenga ujamaa wake. Na mpaka leo CCM wanafata fikra za Nyerere kuwaona wapinzani kama maadui.
 
Bwashee kuna wengine walijaribu kugombea uenyekiti wa chama wakaambiwa sumu haionjwi kwa ulimi. Ulitegemea wafanyeje?

..na CCM walikorudi wanaweza kugombea Uenyekiti wa chama bila kupata misukosuko zaidi ya iliyowakuta walipokuwa upinzani?
 
Back
Top Bottom