1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
Namibia ipo kwenye uchaguzi kwa Sasa. Uchaguzi huu ulikuwa ni mgumu Kwa chama tawala Cha SWAPO ila vyama vya upinzani baadala ya kuungana vikaamua kila mmoja kupambana pekee yake mwisho wa siku SWAPO inaongoza kwa matokeo ya Sasa kwa Asilimia 48 ya kura za urais mpaka Sasa. Vyama vya upinzani vina kura Asilimia 52 ila vimegawana baina yao.
Hivyo basi, Kama vyama vya upinzani vitashiriki mwaka 2025, vianze kutengeneza umoja kwa Sasa ili visigawane kura, bila kuungana CCM itazidi kuwaonea na mwisho wa siku mtabaki kulalamika na hakuna atakayewasikiliza.
Zito na Mbowe hawawezi kuungana maana zito kwa mbowe ni msaliti.
Vinginevyo Chadema ichague viongozi wengine wenye sura mpya ,mawazo tofauti na mtizamo tofauti .
Vyama vingine kwa mfano vinaamini Chadema ni chama cha Wachagga. Sasa uta wa aunganisha vipi hapo ?
Ni ama pawe na mabadiliko ndani ya vyama au vibaki kuwa vyama vya upinzani milele.
Hakuna mtanzania anaweza kukubali chama kilichochafuliwa kuwa ni cha kikabilza kiingie madarakani . Usalama na haki ya wote itakua mashakani.
Lakini pia Mbowe akitafakari kubwa anataka kujenga Taifa bora la Kesho lenye demokrasia ya kweli na ya mfano au anataka kuwa kama CCM kutlinda kwa nguvu zote hata kwa kuua misingi ya kidemokrasia .
Tofauti ya CCM na chadema ni ipi maana vyama vyote vinaua demokrasia ya ndani kwa utetezi kuwa ni kulinda chama kisife mikonii mwao . Huu ni upumbavu wa Nchi za kiafrika . Vyama hata vikifa lakini upinzani wa hoja udumu ndilo jambo la msingi .
Kenya hakuna KANU na maisha ya amani yanaendelea . Kenya wangengangana kulinda KANU wangepoteza maisha ya watu wengi na bila shaka leo nchi ingekuwa kwenye vita kubwa.
Mtu anayengangana kulinda chama kingine nyume na demokrasia kiuhalisia mtu huyo ana ukabila,Udini na ubinafsi .
Siku pakikosekana vyama vingine CCM watatawala kwa kuegemea ukabila ili kupata uungwaji mkono .
Siku ukabila ukaisha watatawala kwa kutumia Udini ili kupata uungwaji mkono . Hapo ndipo amani itakapotoweka maana kila mmoja atajijengea kwa misingi itakayombeba kwa wakati huo.
Demokrasia ni muhimu kuanzia ndani ya vyama .
Madudu yanayofanyika ndani ya CCM na figisu na vitisho kwa sasa vimeegemea kwenye Udini sana yote ni kwa sababu ya kuona chama ndicho kila kitu hata Mwenyezi Mungu na sheria za nchi hazifuatwi.
Kwa sasa kuna watu wa dini fulani ni waoga hata kujipambanua kama ni Chadema kwa namna wanavyotushwa kuwa awamu ya dini fulani waiunge mkono hata kama wanakosea .
Chama ni mafalsafa tu kwenye makaratasi jambo la msingi ni kuwa na kiongozi bora anayelinda na kufuata katiba ya nchi .
Bila shaka Tundu Lisu anafaa kurejesha utawala wa sheria unaosimamia haki .
RIP . Ally Kibao.