Upinzani Tanzania msirudie kosa walilofanya wenzenu wa Namibia

Upinzani Tanzania msirudie kosa walilofanya wenzenu wa Namibia

Tatzo hawa upinzan wa tz kama TLP kile cha mzee wa ubwabwa nk hamna vyama pale ni kupotezana maboya tu. Kingine tamaa na usaliti ndani kwa ndani kwa wapinzani wa hapa kwetu. Hawana mshikamano dhabiti. Mwisho kurubuniwa

Hizi nazo ni changamoto kubwa. Kurubiniwa na kusalitiana imekuwa Kama fashion kwa siasa za upinzani. Hii ukatisha moyo Sana wananchi wanaowaunga mkono.
 
Ilikuwepo UKAWA ambapo wapinzani wote walishirikiana na CHADEMA. Too bad sahizi walio strong ni ACT na CHADEMA ila wote wenyeviti wake ni kama mapandikizi ya CCM. Hamna upinzani imara, watu wanafocus na Ruzuku tu.

Kweli kabisa. Hii ni changamoto kubwa.
 
Zito na Mbowe hawawezi kuungana maana zito kwa mbowe ni msaliti.

Vinginevyo Chadema ichague viongozi wengine wenye sura mpya ,mawazo tofauti na mtizamo tofauti .
Vyama vingine kwa mfano vinaamini Chadema ni chama cha Wachagga. Sasa uta wa aunganisha vipi hapo ?

Ni ama pawe na mabadiliko ndani ya vyama au vibaki kuwa vyama vya upinzani milele.

Hakuna mtanzania anaweza kukubali chama kilichochafuliwa kuwa ni cha kikabilza kiingie madarakani . Usalama na haki ya wote itakua mashakani.

Lakini pia Mbowe akitafakari kubwa anataka kujenga Taifa bora la Kesho lenye demokrasia ya kweli na ya mfano au anataka kuwa kama CCM kutlinda kwa nguvu zote hata kwa kuua misingi ya kidemokrasia .
Tofauti ya CCM na chadema ni ipi maana vyama vyote vinaua demokrasia ya ndani kwa utetezi kuwa ni kulinda chama kisife mikonii mwao . Huu ni upumbavu wa Nchi za kiafrika . Vyama hata vikifa lakini upinzani wa hoja udumu ndilo jambo la msingi .
Kenya hakuna KANU na maisha ya amani yanaendelea . Kenya wangengangana kulinda KANU wangepoteza maisha ya watu wengi na bila shaka leo nchi ingekuwa kwenye vita kubwa.

Mtu anayengangana kulinda chama kingine nyume na demokrasia kiuhalisia mtu huyo ana ukabila,Udini na ubinafsi .
Siku pakikosekana vyama vingine CCM watatawala kwa kuegemea ukabila ili kupata uungwaji mkono .
Siku ukabila ukaisha watatawala kwa kutumia Udini ili kupata uungwaji mkono . Hapo ndipo amani itakapotoweka maana kila mmoja atajijengea kwa misingi itakayombeba kwa wakati huo.
Demokrasia ni muhimu kuanzia ndani ya vyama .
Madudu yanayofanyika ndani ya CCM na figisu na vitisho kwa sasa vimeegemea kwenye Udini sana yote ni kwa sababu ya kuona chama ndicho kila kitu hata Mwenyezi Mungu na sheria za nchi hazifuatwi.

Kwa sasa kuna watu wa dini fulani ni waoga hata kujipambanua kama ni Chadema kwa namna wanavyotushwa kuwa awamu ya dini fulani waiunge mkono hata kama wanakosea .
Chama ni mafalsafa tu kwenye makaratasi jambo la msingi ni kuwa na kiongozi bora anayelinda na kufuata katiba ya nchi .
Bila shaka Tundu Lisu anafaa kurejesha utawala wa sheria unaosimamia haki .
RIP . Ally Kibao.

Kweli kabisa mkuu. CHADEMA ibadilishwe uongozi wa chama na kuleta sura mpya zinazoaminika na mabazo zitaleta uhamasishaji mpya wa upinzani.
 
Namibia ipo kwenye uchaguzi kwa Sasa. Uchaguzi huu ulikuwa ni mgumu Kwa chama tawala Cha SWAPO ila vyama vya upinzani baadala ya kuungana vikaamua kila mmoja kupambana pekee yake mwisho wa siku SWAPO inaongoza kwa matokeo ya Sasa kwa Asilimia 48 ya kura za urais mpaka Sasa. Vyama vya upinzani vina kura Asilimia 52 ila vimegawana baina yao.

Hivyo basi, Kama vyama vya upinzani vitashiriki mwaka 2025, vianze kutengeneza umoja kwa Sasa ili visigawane kura, bila kuungana CCM itazidi kuwaonea na mwisho wa siku mtabaki kulalamika na hakuna atakayewasikiliza.
Tatizo la Tanzania ni tofauti na huko Namibia,Kule Namibia uchaguzi unafanyika kwa haki na huru na ndiyo maana wapinzani wamepata wingi wa kura kiasi hicho lakini Tanzania kuna maigizo tu ya uchaguzi wagombea wa upinzani wanaenguliwa kibabe,wagombea wengine wanauawa na kujeruhiwa yaani full vitisho na hatimaye wasimamizi wa uchaguzi wanatangaza matokeo batili na kukipa ushindi ccm na ndiyo maana unasikia ccm wameshinda kwa zaidi ya 99% na wapinzani wote wameambulia chini ya 1% sasa hapo wapinzani hata wakiungana itawasaidia nini!
Kinachotakiwa kwanza ni kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa haki na usawa kwa vyama vyote.
 
Nadhani Kuna wimbi la mabadiliko linakuja, SA tuliona, Botswana, Msumbiji na Sasa Namibia. Nadhani kwa Tanzania CCM imejikita kwenye vyombo vya Dola kiasi kwamba ni vigumu kukiondoa.
Hapana CCM imejichimbia chini inawatu wengi sana kwenye mashina
 
Raia wetu nao ni changamoto, wanaojifanya ya kwamba siasa haiwahusu wao ni Mpira na muziki basi.
Msitulaumu raia ili kuficha upuuzi na uzezeta wenu wa kisiasa. Unasahau namna gani kuwa raia tuliwahi kuiunga mkono chadema mpaka ikafikisha wabunge karibu 50 wa kuchaguliwa? Chama mlikigeuza wenyewe mlipokikodisha kwa kada wa ccm ili agombelee ueais. Unataka wananchi tuendelee kuunga mkono ujinga wa viongozi wenu walafi wa pesa?
 
Itisha tamasha la muziki halafu itisha mkutano wa siasa uone wapi watu wataenda. Ndio maana CCM kwa kulijua Hilo huwa wanaleta wasanii.
Kwahiyo hiko ndio kipimo cha watanzania kutojihusisha na siasa kwa maana ilitakiwa watu wajae sana kwenye mikutano ya kisiasa kuliko kwenye mikusanyiko ya burudani?
 
Hapana CCM imejichimbia chini inawatu wengi sana kwenye mashina
Juzi kati kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa nilipita sehemu maeneo napoishi nikakuta muziki mkubwa mara nikaona picha ya mgombea wa chadema kwa maana alikuwa anatarajiwa kufanya kampeni zake hapo. Nikashangaa kumbe chadema imesimamisha mgombea sikuwa nikijua na huyo mgombea ndio mara ya kwanza kumuona tena katika picha tu.
 
Hivyo basi, Kama vyama vya upinzani vitashiriki mwaka 2025, vianze kutengeneza umoja kwa Sasa ili visigawane kura, bila kuungana CCM itazidi kuwaonea na mwisho wa siku mtabaki kulalamika na hakuna atakayewasikiliza.
Utakuwa unazo sababu zako za kukomalia kuungana huku!

Waungane wakati hawana polisi na mitutu ya bunduki itasaidia nini?
 
Tatizo la Tanzania ni tofauti na huko Namibia,Kule Namibia uchaguzi unafanyika kwa haki na huru na ndiyo maana wapinzani wamepata wingi wa kura kiasi hicho lakini Tanzania kuna maigizo tu ya uchaguzi wagombea wa upinzani wanaenguliwa kibabe,wagombea wengine wanauawa na kujeruhiwa yaani full vitisho na hatimaye wasimamizi wa uchaguzi wanatangaza matokeo batili na kukipa ushindi ccm na ndiyo maana unasikia ccm wameshinda kwa zaidi ya 99% na wapinzani wote wameambulia chini ya 1% sasa hapo wapinzani hata wakiungana itawasaidia nini!
Kinachotakiwa kwanza ni kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa haki na usawa kwa vyama vyote.
Hakuna chama tawala kinachowasaidia wapinzani wake kushinda.

Upinzani kwa sasa wamejaa wenyeviti wapumbavu watupu.

Hivi Mbowe anatosha kuleta mageuzi ya siasa za kupambana na CCM kwa sasa.
Mbowe anaweza siasa laini laini kama za Kikwete na siao hizi za kitalebani za Kizanzibari na mapanga Shaa za Cuf iliyojivika jina la CCM ya awamu ya sita. Hii CCM ni ile cuf iliyochangamka na kukimbia Zanzibar na kuibukia Tanganyika chini ya Kizimkazi.
Hii haina Kuremba ipo kulipa kisasi cha ubaya waliofanyiwa Cuf na majeshi kutoka Tanganyika . Fuatilieni mtaona hata wetu wanaowatukana sana Maaskofu kwenye Mitandao na hata kuvuruga uchaguzi . Wengi sio wetu wa CCM ya kawaida . Ni waCCMD mapinduzi daima

Kaeni kwa kutulia .
Upinzani hauna nguvu . Tena upinzani unabahati viongozi wa dini wanajitahidi kuwasadia vinginevyo walishaishiwa pumzi kabisa . ACT angalau waislam wenye hofu ya Mungu wanawasemea kidogo na chadema wakristo wenye nia njema na Taifa hili pia wanajaribu kuwasemea.

Bila wanazuoni wenye moyo wa chuma kama Shehe Ponda na Padri Dr.Kitima kusimama na wapinzani upinzani ungesahaulika.

Kwa sasa angalau wetu wanawaamini viongozi wa dini kuliko wanasiasa ukizingatia kuwa wanasiasa hawapo kupigania maslahi ya wanyonge walio wengi nchini.
 
SWAPO ni moja ya vyama vikongwe barani Africa kimelea uhuru Naminia 1990 lakini unaona tayari kinakwenda hapa Bongo CCM ipo tangu 1955 lakini bado tunakichekea chekea.
CCM itolewe na hawa vichwa maji akina zitto, mbowe , lissu ambao hawajui wanapigania nini? Wabweke kura tutaipigia CCM
 
Nadhani Kuna wimbi la mabadiliko linakuja, SA tuliona, Botswana, Msumbiji na Sasa Namibia. Nadhani kwa Tanzania CCM imejikita kwenye vyombo vya Dola kiasi kwamba ni vigumu kukiondoa.
Umeeleza vizuri ila maneno mawili ya mwisho umeharibu.
 
Hizi nazo ni changamoto kubwa. Kurubiniwa na kusalitiana imekuwa Kama fashion kwa siasa za upinzani. Hii ukatisha moyo Sana wananchi wanaowaunga mkono.
Kabisa, wakichaguliwa baadae wanaunga mkono juhudi na kuhamia Ccm Kisha kugombea tena ubunge ule ule waliojivua.
 
Back
Top Bottom